Mi kuombwa sina tatizo, tena huwa nafurahia kutoa kama ninacho lakini kuomba siwezi na sitaki!!!
Hata hivyo, kwa vitu vidogo vidogo kama vile vya jikoni, ukiniomba na kama ni kitu cha kuhitaji kurudisha basi nirudishie mara utakavyomalizia shughuli zako vinginevyo nitakususia jumla kwa sababu sina desturi ya kupiga hodi nyumba au milango ya watu!!
Kwa mfano mtu unaenda kuomba kisu, na unajua kabisa mtu hawezi kuwa na kisu zaidi ya kimoja; halafu unaomba lakini kurudisha hadi mwenyewe akifuate tena... wtf?!
Trust me, kama nitafuata mara ya kwanza, halafu ukachukua tena na ukabaki nacho, kitakachofuata hapo ni mimi kwenda kununua kingine ili nikuachie "kisu chako"!