Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Unajua kutetea nakuifanya upya ndoa yako.wewe niwatofauti lakini usijali kwani ninyi ni mwili mmoja ndoto zako nizake na zake ni nizako pia. Hakika wewe niwapekee kama nimapenzi ya mungu utatimiza tu ndoto zako

Sent using Jamii Forums mobile app
Wow wow Nimependa hapo "Kama ni mapenzi ya Mungu utatimiza tu ndoto zako" asante mpendwa.Hii amani niko nayo hata naonaga bado wakati wa Mungu haujafika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una watoto wadogo, ni bora ungewafungulia acc yao maana unasema huhitaji kwa ajili ya shule maana bado wadogo that's wrong
Hata wewe kuna wakati ulikuwa mdogo kwa hiyo fanya hima usisubiri wakue ndio uanze kuhangaikia mikopo.
Weka sasa wafaidi baadae.

Kama unaona yako hayaendi bora uweke kwa ajili ya watoto.

Yeye ni hustler mwache ahangaike wewe weka zako
 
Too good to be true
 
Asante mpendwa.ndoto zangu nilishamuambia hata kabla hatujaingia kwenye ndoa.sina nia mbaya kushare hapa kwamba nahitaji kubadilika hapana maana ndani yangu kweli nina amani na ninachofanya.nimelileta kama wanandoa tulione kwa pamoja na walio kama mimi.kama ni kubadilika ningeshabadilika maana ukimwambia mtu ni wachache sana wanaona its ok wengi wanakimbilia Negative tu.kuleta hapa tuko wengi wanandoa na wasomi .nimeleta nikutane na waoniona positive na walio kama mimi.otherwise nasema tena Asante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yaani nilivyoona unashukuru kwa kupata mume ambaye sio mlevi nimeacha kusoma kabisa.....
 
 
Najua hutumii vibaya ila angalia future ya watoto I mean waandalie usisubiri kumekucha
All the best
 
Mpendwa ananisaport but mimi akinipa pesa namwambia no.yaani nikichukua hela kutoka kwake ujue kweeeli nahitaji hizo hela.but mara nyingi anipata naongea nae mpaka anaielewa kwamba aendelee kupanua biashara zaidi na hata idea zingine za biashara hii yangu itafanyika tu online hivyohivyo but kwa sasa afanye yeye.na nakuwa na amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You are the real defination ya Mke mwema.Unaongozwa na upendo wa dhati na siyo upendo wa vitu.Mungu aendelee kukubariki.
 
M/Mungu naomba nipatie mke kama uyu!!

[emoji125] [emoji125]

Sent from my iphone 6s using Jamii Forum Mobile app
 
Uko na maximum care juu ya familia. Na ndio kitu kinatakikana japo kuna haja ya kujifunza baadhi ya shughuli za kibiashara ili uwe na experience na kipato zaidi.
 
Dah kwa madini haya mm naomba hata unifanye mchepuko wako.....najua sitoki patupu wahenga walinena mgagaa na upwa hali wali mkavu!
 
Wala si ujinga! nadhani hiyo unayofanya ndo dhana ya mwili mmoja.Yaani chake, chako! endelea tu na lifestyle yako kama unafeel amani moyoni mwako.Kila lakheri.
 
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] dahhhh Mimi ilinitokea aiseeee nilimpenda mwanaume alikuwa nakazi akaja akasimamishwa kazi mpaka akiumwa ni juu yangu kuanzia chai ya asubuhi ,mchana,jioni nimimi maji anayooga Mimi akienda kutafuta Kazi ela ya nauli ni kwangu Jamani kiukweli nilimpenda sana ikaja tokea kanipa mimba nililia kwababu Mimi mpaka babu akatupangia pakukaa kitanda,kijiko,uma,madumu ya maji ,godolo majiko ,vyakula ikawa Na mimba yangu mwanaume anaondoka anaenda kutafuta riziki akirudi hana kitu Mimi niliweka moyoni mpaka kesho hakuna ndugu yangu hata mzazi wangu aliejua nilikuwa nalala njaa siku hamna chakula natoka naenda nyumbani najifanya naenda kusalimia maana najua nikiondoka nabebeshwa vitu kiukweli babu yangu ananipenda sana nakumbuka Na mimba mwanaume aliondoka siku 3 yupo kwao mlandiz ameniachia 2000 tu Jamani nilikuwa kimya nikitoka nacheka namajirani nikiingia kwangu nalia nikichoka nalala nilinunua unga nilikuwa nikisikia njaa nakologa uji nakunywa mpaka anarudi siku naenda kujifungua hana ela alikimbia aibu alinitelekeza Na mtoto toka siku nazaaa nikaludi akaja akaomba msamaha akidai aibu alikimbia familia isingemuelewa hana ela namimi nimefanyiwa operation kubwa ,Jamani baada ya kupata Kazi mwanaume alinitelekeza Na mtoto Wa miez 3 nililudi nyumbani kwababu sitasahau mpaka unaingia kaburini Watoto Wa babu mashangazi walinitesa nawananitesa Mwanangu namimi tulikuwa tunanyimwa chakula baba mtoto ukimtafuta anakutukana,mtoto akiumwa anamwambia naakifa utamla nyama Jamani kiukweli alisahau yote niliomfanyia mpaka Leo Mwanangu anamiaka 8 ata ada ya mtoto au hata pencil hajui ya baba yake bola uwekeze

Kwa mwanao sio mwanaume jamani[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] huyu Dada namhurumia Jamani akumbuke kunakifo hivi mungu akimchukua Watoto hujawawekea misingi kuna ndugu pia wakija kufilisi Mali utalia Na nani pia kumbuka uyo mwanaume ni binadamu akija kubadilika utaishije imeandikwa alaaniwae amtegemeaye mwanadamu katika bible Dada jisimamie Mimi sio baba mtoto tu nishakuwa Na uhusiano mwingine mwanaume anashida unajitoa Jamani mwisho Wa siku akipata kwake huna thamani ila wakiwa Na shida niwapole sana katika hao wawili sitopenda mwanaume eti mpaka nimsaidie ni ngumu akomae nahali yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…