Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana mpendwa kwa ushauri wako.sio kwamba biashara yake haiendelei hapana inaendelea vizuri sana but ni mimi ndo nataka ifanikiwe zaidi na zaidi tena zaidi .Asante sanaHongera kwa kufanya hivo
Upendo amani ni kitu cha muhimu sana
Mshauri afanye uchunguz kwa nin biashara yake haendi mbele
Kila wakati mnatop up mtaji....mtafute MTU wa mahesabu awashauri
.....pia ndoto zako ziweke wazi ili mfanye kwa pamoja
Hutakiwi kufanya kitu cha pekeako as uko kwenye ndoa
Kila LA kheri my.....pia jitahd kuepuka makundi mabaya ya kina Dada/mama ili uendelee na moyo huo huo
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wapendwa.Naomba kwa wale wanandoa mnisaidie hapa kama ni kawaida kwa wanandoa ama ni nini?.
Namshukuru Mungu tulipata kuoana na mume wangu ,kweli Maisha ni mazuri tunafurahia ndoa yetu na watoto wetu pia. Namshukuru Mungu pia amenipa mume ambaye sio mlevi wala mpenda starehe yaani inshort hela hachezei anafanyia vitu vya maana sana.
Kuna wakati tulifungua joint account ilivyofika kiwango tulikuwa tunataka tukakubaliana akazitoa na akafanyia kazi nzuri sana kwa uaminifu. Na pia mara nyingi nikiwa na hela ambazo najua sizitumii kwa muda huo nampa anafanyia biashara zake baadaye nikihitaji anazirudisha.
Kabla na baada pia ya kuolewa nina ndoto nyingi za mimi kufikia level fulani na nilimshirikisha pia na akalifurahia.
Sasa tatizo linakuja kwamba kweli mpaka leo karibia miaka minne sasa hakuna kitu nimefanya katika kuachieve ndoto zangu, nimepiga kihatua kidogo sana, Hela naweka akiba inafikia kabisa kiasi nataka kutimiza malengo yangu but najikuta tu nimempea mume wangu bila yeye kuniambia nimsaidie.
Yaani niko hivi sipendi kuona mume wangu hana amani au akiwaza wapi apate hela au akiniambia hasara aliyopata katika business muda mwingine nachukua card yangu ya bank naenda kutoa hela zote nampa kwa kumwambia hii hela siko na kazi nayo na naona niweke huko kwa business yako so zitumie tu kule usirudishe. (But lengo langu ni kutaka tu ajisikie vizuri pamoja na hasara aliyoipata hela nyingine imekuja) Na ukimpa anapeleka pale kwa uaminifu kabisa.
Hela ya matumizi akinipa kweli namrudishia sijui kwanini but naona tu kwanini nichukue hela wakati mahitaji madogomadogo ya nyumbani naweza toa hela na vile bado hatujaanza kusomesha so mahitaji sio mengi si bora hiyo hela aendelee kuizungusha kwa biashara.
Basi naona tu hivyo na nakuwa na amani. Weekend hii ilikuwa nikachukue frame ya kufanyia kabiashara kangu (hili hata sikumwambia kwamba nimeshapata frame) but juzi akaniambia habari ya kiwanja alichokiona mjini sehemu nzuri sana na kina title na alipokuwa anaongea anaonesha kabisa kwamba we real need that land.
Hakuniambia toa hela wala nini but mimi "emoj mwenyewe nikamwambia niko na pesa nikaenda bank nimetoa hela zote hadi za mtaji wa biashara yangu ninayofanya online nimempa. Nimebakiwa tu na 100k za kuniweka hadi mwisho wa mwezi nianze upya kusave .
Wapendwa jamani hii ni kwangu tu ama ni kwa wanandoa wote???.
Sifanyi chochote kuachieve my dreams but niko na Amani sana ndani ya moyo wangu kwasababu my husband is so happy napenda tu kumwona ana furaha sitaki kabisa apate stress kisa hela au kisa mambo yake hayaendi vizuri.
Namuombea sana na pale naweza kutoa pesa natoa sana na pale pa kumencourage namuencourage sana na kwa mimi hakuna kitu mimi nimejifanyia and am happy.hii itakuwa ni nini??? [emoji23][emoji23][emoji23].
Sent using Jamii Forums mobile app
Mke hasa stahili yake kukatiwa kadi isiyo na chini ya US $ 20,000 kwa matumizi ya kawaida.
Na email alerts zinazoonyesha kila kinachonunuliwa kwa uwazi zaidi.
Na wakati tunafua tukikuta noti hatusemi.Mungu angenipa mke kama huyu,ningemtukuza milele.Sisi wa kwetu wanasachi mpaka suruali uliyovaa jana.Hongera mummy
Mume na mke waaminiane 100%.Kila mwanaume atakuona unachokifanya kipo sawa ila kiukweli kuna kiasi cha kumsaidia mwanaume na sio kwa kiwango kama hicho chako.
Punguza roho nzuri ambapo hatakama utakuwa unampa hakikisha wewe kama wewe una akiba yako ya kutosha na sio ya kusema umpe yote halafu usubiri mwezi ugeuke uanze kuweka upya kuna leo na kesho mumy emoj.
Wanaume sio viumbe wa kuwaamini kwa 100%.
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
sorry una umri gan?
Kule ujerumani wana ndoa za mikataba, watu wanaweza wakafunga ndoa za mkataba wa miaka mitano, baada ya hapo wanaweza kuachana au kuendelea.Yaani mume angekua anatafutwa kila baada ya miaka mitano kama Raisi au mbunge walahi ningegombea kuwa mume wako.
Salute[emoji120] [emoji120] [emoji120]Hongera kwa kuwa na amani kama ulivyosema. Ila kwa maisha mnayoishi kwa jinsi ya maelezo yako inaonyesha Hamna malengo ya pamoja kila MTU ana mambo yake hii inaonyesha hata kwenye maongezi yako ".....biashara zake,!? ....... nilikuwa sizitumii nikaamua kumpa!? ........nk" Hamko pamoja kabisa.
Unaakiba kwa bank au yenye ana akiba kwa bank ila kila MTU hajui hiyo!!!!? Unataka kufungua biashara na umepata fremu yeye hajui!!!!?
Hapa kweli hata wewe ni sababu ya kutokuwa na maendeleo unayoyatamani kama familia, na bado hamja anza majukumu yakusomesha watoto yakianza maisha yatakuwa magumu kwenu aisee.
Ushauri wangu kaeni mpange mambo yanu pamoja na kuweka vipaumbele na kila mmoja ashiriki kuhakikisha mambo yanatokea kweli. Mimi pesa zangu ni za mke wangu na za mke wangu ni zangu, ndioooo!
Hapa ndivyo familia inavyotakiwa kuishi kama baba na mama au mke na mume. Mambo yake ni mambo yangu, na mambo yangu ni yake pia anajua passwords zangu za kila mahali nami pia na mambo yanaenda kulingana na mipango na malengo yetu.
Kaeni chini wekeni malengo sio kila MTU anakuwa na malengo yake wakati ni ya familia.
Kila la kheri
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata huku kwetu wapo.huyu mke anahitaji kuheshimiwa kwa kweli anamoyo wa aina yake
Hahahaa,mimi nipo dada ang,kwenye ule uzi nlipigwa cha mbavu na boss lady...nkaona nitulie.haha nilikuona jana kwenye uzi wa le boss lady sema sikuwa na mzuka wa kucomment nikawa napita tu!upo mdogo wangu!
Hahahaa,mimi nipo dada ang,kwenye ule uzi nlipigwa cha mbavu na boss lady...nkaona nitulie.
Teh,pamoja dada,hahahaa nilikuona hha!