Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Habari wapendwa,

Naomba kwa wale wanandoa mnisaidie hapa kama ni kawaida kwa wanandoa ama ni nini? Namshukuru Mungu tulipata kuoana na mume wangu, kweli maisha ni mazuri tunafurahia ndoa yetu na watoto wetu pia.

Namshukuru Mungu pia amenipa mume ambaye sio mlevi wala mpenda starehe yaani inshort hela hachezei anafanyia vitu vya maana sana.

Kuna wakati tulifungua joint account ilivyofika kiwango tulikuwa tunataka tukakubaliana akazitoa na akafanyia kazi nzuri sana kwa uaminifu. Na pia mara nyingi nikiwa na hela ambazo najua sizitumii kwa muda huo nampa anafanyia biashara zake baadaye nikihitaji anazirudisha.

Kabla na baada pia ya kuolewa nina ndoto nyingi za mimi kufikia level fulani na nilimshirikisha pia na akalifurahia.

Sasa tatizo linakuja kwamba kweli mpaka leo karibia miaka minne sasa hakuna kitu nimefanya katika kuachieve ndoto zangu, nimepiga kihatua kidogo sana, hela naweka akiba inafikia kabisa kiasi nataka kutimiza malengo yangu but najikuta tu nimempa mume wangu bila yeye kuniambia nimsaidie.

Yaani niko hivi sipendi kuona mume wangu hana amani au akiwaza wapi apate hela au akiniambia hasara aliyopata katika business muda mwingine nachukua card yangu ya bank naenda kutoa hela zote nampa kwa kumwambia hii hela siko na kazi nayo na naona niweke huko kwa business yako so zitumie tu kule usirudishe. (But lengo langu ni kutaka tu ajisikie vizuri pamoja na hasara aliyoipata hela nyingine imekuja) na ukimpa anapeleka pale kwa uaminifu kabisa.

Hela ya matumizi akinipa kweli namrudishia sijui kwanini but naona tu kwanini nichukue hela wakati mahitaji madogomadogo ya nyumbani naweza toa hela na vile bado hatujaanza kusomesha so mahitaji sio mengi si bora hiyo hela aendelee kuizungusha kwa biashara.

Basi naona tu hivyo na nakuwa na amani. Weekend hii ilikuwa nikachukue frame ya kufanyia kabiashara kangu (hili hata sikumwambia kwamba nimeshapata frame) but juzi akaniambia habari ya kiwanja alichokiona mjini sehemu nzuri sana na kina title na alipokuwa anaongea anaonesha kabisa kwamba we real need that land.

Hakuniambia toa hela wala nini but mimi mwenyewe nikamwambia niko na pesa nikaenda bank nimetoa hela zote hadi za mtaji wa biashara yangu ninayofanya online nimempa. Nimebakiwa tu na 100k za kuniweka hadi mwisho wa mwezi nianze upya kusave .

Wapendwa jamani hii ni kwangu tu ama ni kwa wanandoa wote? Sifanyi chochote kuachieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu kwasababu my husband is so happy napenda tu kumwona ana furaha sitaki kabisa apate stress kisa hela au kisa mambo yake hayaendi vizuri.

Namuombea sana na pale naweza kutoa pesa natoa sana na pale pa kumencourage namuencourage sana na kwa mimi hakuna kitu mimi nimejifanyia and am happy.hii itakuwa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji121]
MKUU,

HAUNA PACHA WAKO WA KUTOATOA HELA KAMA WEWE
NITANGAZE NDOA FASTA?!?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaaaaa jamani nacheka kufa hapa. Loh kumbe tunapanda abood basi nilidhani tunaenda pande zile. Poa mydear tutaenda kuoga baharini

hahahaha kule kunanuka perege tu! hahaha kweli tukadip had mabichwa yaan tuzame mwil mzimaaa
 
Ukute hiyo harufu ya perege ndo baraka zenyewe

demi hadi nimekaa kitandani ghafla! hahahahhahahhahahhha uwi jaman demi mie wewe nakufaaaaaaaaaaaaaaa! dah kweli wewe mie sikuwez!,,,, unanikumbusha frndz zangu jaman tukikutana hahaha km ni bar tunapendwa na kila mtu yaan ni vichekooo plus stress bas rahaa! dah ngj niicopy hii comment
 
Inaonekana una furaha sana maana kwa kucheka tu sikuwezi.ha haaa cheka tu mwaya. Ila mindu lazima tukadumbukie.
 
yaan mie kucheka jaman huwa sijuikuvunga! huwa sikai karibu na dadangu maana anavichekeshooo! hee! leo nimecheka jaman naogopa ht kulala huenda nikapitia hukohuko !hheheh! team mindu hahhahhaa dah we demi mbn sikuzoei tu
 
Mh! Kwahiyo ulipanga kufungua biashara bila kumshirikisha!! Mimi Nina mtazamo tofauti na wengi, unaonekana mke mwema lakini haumpi changamoto mume wako kwasababu wakati wote unakubali mawazo yake tu yako unayasitisha. Ni Kama vile una amini sana mipango ya mume na sidhani hata kama huwa unafuatilia biashara zake kwa undani.

Jaribu kumueleza mume wako mipango yako ya biashara na wewe pengine ni mizuri zaidi ya kwake. Kingine msiweke mayai yote kwenye kapu moja, siku biashara yake ikiyumba itakuaje? Halafu hakuna ndoto zako na zake, zote ni zenu.

Kingine jitahidi kuijua kwa undani biashara ya mumeo maana kuna kesho na kesho kutwa.

Mwisho ufanyajo ni kawaida kwa wana ndoa
 
Habari wapendwa,

Naomba kwa wale wanandoa mnisaidie hapa kama ni kawaida kwa wanandoa ama ni nini? Namshukuru Mungu tulipata kuoana na mume wangu, kweli maisha ni mazuri tunafurahia ndoa yetu na watoto wetu pia.

Namshukuru Mungu pia amenipa mume ambaye sio mlevi wala mpenda starehe yaani inshort hela hachezei anafanyia vitu vya maana sana.

Kuna wakati tulifungua joint account ilivyofika kiwango tulikuwa tunataka tukakubaliana akazitoa na akafanyia kazi nzuri sana kwa uaminifu. Na pia mara nyingi nikiwa na hela ambazo najua sizitumii kwa muda huo nampa anafanyia biashara zake baadaye nikihitaji anazirudisha.

Kabla na baada pia ya kuolewa nina ndoto nyingi za mimi kufikia level fulani na nilimshirikisha pia na akalifurahia.

Sasa tatizo linakuja kwamba kweli mpaka leo karibia miaka minne sasa hakuna kitu nimefanya katika kuachieve ndoto zangu, nimepiga kihatua kidogo sana, hela naweka akiba inafikia kabisa kiasi nataka kutimiza malengo yangu but najikuta tu nimempa mume wangu bila yeye kuniambia nimsaidie.

Yaani niko hivi sipendi kuona mume wangu hana amani au akiwaza wapi apate hela au akiniambia hasara aliyopata katika business muda mwingine nachukua card yangu ya bank naenda kutoa hela zote nampa kwa kumwambia hii hela siko na kazi nayo na naona niweke huko kwa business yako so zitumie tu kule usirudishe. (But lengo langu ni kutaka tu ajisikie vizuri pamoja na hasara aliyoipata hela nyingine imekuja) na ukimpa anapeleka pale kwa uaminifu kabisa.

Hela ya matumizi akinipa kweli namrudishia sijui kwanini but naona tu kwanini nichukue hela wakati mahitaji madogomadogo ya nyumbani naweza toa hela na vile bado hatujaanza kusomesha so mahitaji sio mengi si bora hiyo hela aendelee kuizungusha kwa biashara.

Basi naona tu hivyo na nakuwa na amani. Weekend hii ilikuwa nikachukue frame ya kufanyia kabiashara kangu (hili hata sikumwambia kwamba nimeshapata frame) but juzi akaniambia habari ya kiwanja alichokiona mjini sehemu nzuri sana na kina title na alipokuwa anaongea anaonesha kabisa kwamba we real need that land.

Hakuniambia toa hela wala nini but mimi mwenyewe nikamwambia niko na pesa nikaenda bank nimetoa hela zote hadi za mtaji wa biashara yangu ninayofanya online nimempa. Nimebakiwa tu na 100k za kuniweka hadi mwisho wa mwezi nianze upya kusave .

Wapendwa jamani hii ni kwangu tu ama ni kwa wanandoa wote? Sifanyi chochote kuachieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu kwasababu my husband is so happy napenda tu kumwona ana furaha sitaki kabisa apate stress kisa hela au kisa mambo yake hayaendi vizuri.

Namuombea sana na pale naweza kutoa pesa natoa sana na pale pa kumencourage namuencourage sana na kwa mimi hakuna kitu mimi nimejifanyia and am happy.hii itakuwa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Akikuacha/akifa/ukimwacha njoo kwangu nikuoe hata kesho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom