Sipendi kuona Watanzania wakidanganywa kila leo

Sipendi kuona Watanzania wakidanganywa kila leo

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2009
Posts
3,400
Reaction score
320
Sipendi kuona Watanzania kazi yao kudanganywa tu!!
Sitaki kuona raisi wetu kazi yake ni kuzurura tu!!
Sipendi kuona maisha ya watu + na watu – Tanzania!!
Sipendi kuona Tanzania ikitawaliwa na chama kimoja tu!!
Sipendi tena kimejaa matapeli na wezi wa mali za umma!!
Sipendi watanzania wanajiita wasomi, harafu wametawaliwa kifikra!!
Sipendi kuona raisi anakuwa muoga kuchukua maamuzi mazito!!
Sipendi kuona……tena hayo ni kuwawajibisha mafisadi!!
Sipendi kuona wengine wakunywa chai ya Maziwa na Boflo la siagi,!!
Sipendi kuona wengine hawaijui hata rangi ya chai wao kuisikia kwa wengine!!
Sipendi kuona …wanayajua matangazo ya ‘hai bora iwe na sukari’ tu!!
Sipendi kuona chama kilichojaa mafisadi kinaaongoza nchi tena sipendi kabisa!!
Sipendi kuona rais anaongoza nchi kwa majungu!!
Sipendi kuona watanzania hawawezi kusimamia maamuzi na fikra zao!!
Sipendi tena sitaki kuona wasomi wa Tanzania wakitishiwa nyau wanapotoa mawazo yao
Sipendi kuona Tanzania inaliwa na wachache tu,
Sipendi kuona watanzania wao ni ndiyo mzee hata kwenye kuibiwa, sitaki kabisa!!
Sipendi kuona watanzaniawanahongwa pombe na kofia ili kuwachagua wezi!!
 
napenda kuona ambayo wewe HUPENDI KUONA
 
Utafanyaje ili yote haya usiyaone tena?
Na kampeni ndo zinaelekea kuanza ..nadhani tutaambiwa barabara zitajengwa mawinguni...
Sipendi kuona pia
 
Sipendi kusikia ukilalamika wakati haupo bongo na hauoni kinachoendelea zaidi ya kusikia.
 
Sipendi kuona wengine wakunywa chai ya Maziwa na Boflo la siagi,!!
Sipendi kuona wengine hawaijui hata rangi ya chai wao kuisikia kwa wengine!!

Laweza kuwa ni suala la kuchagua tu !

Du Boflo nililisikia siku nyingi sana mkuu; ww kweli old skul
 
That person has just big stinking mouth.He doesn't know what he is taking about.Y u left the country if u want the change.U need to shut ur stinking mouth.
 
That person has just big stinking mouth.He doesn't know what he is taking about.Y u left the country if u want the change.U need to shut ur stinking mouth.
kuwa wazi tu kama umeguswa na ujinga wako
harafu jaribu kuficha upumbavu wako, hadharani lete hekima, kama huna nyamaza kimya si lazima utume post, i hope ou are nothing in mind, seek medical check up
 
Hata hii Wizara ya Miundombinu iliyotangaza kutafuta mkandarasi wa kukagua magari, ili kupunguza ajali, eti anakaribisha maoni! Ref. Daily News 26.03.10. Siyatakuwa yale yale ya kuuza stickers? nami hii sipendi!
 
Ha ha ha.Hupendi kuona hayo uliyoyataja.Je umechukua hatua zozote za kimakusudi ili kuhakikisha hayo usiyopenda kuona hayatokei?au ndio unaishia tu kusema hupendi kuyoana lakini umekaa tu.
 
Kwani mtu akiwa nje ya nchi akaona uozo na akasema hapendi kuona kuna ubaya jamani.
Sipendi kuona watu wanajifanya kupambana na ufisadi lakini ukiwasikiliza kwa nini wanataka kwenda kufanya kazi serikalini walipwe laki na nusu ni kwa vile atapata Rushwa..Hiyo sipendi kuona kabisa...
Sipendi...
 
Back
Top Bottom