Sipendi mikunjo ya tumbo langu nisaidieni

wakusepa

Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
83
Reaction score
5
jamani nina kitambi na tumbo kujikunja kunja wakati ninapokaa,mfano kwenye kiti au popote pale,hii hali inanichukiza sana kwan sipend hichi kitambi kwani kinanipotezea body langu.
Hvyo naomben ushaur nifanyeje jaman coz i hate myself
 
Maji vugu vugu, mdalasini na ndimu kila siku asubuhi kabla ya kula chochote
 
Pole sana wakupesa. Napenda kukushauri kuwa unaweza kufuata njia nzuri ya kuweza kuweka mwili wako ukaonekana safi kwa jinsi upendavyo mwenyewe kwa kufuata njia isiyo na maumivu wala kujitesa kwa kujinyima kula na mambo mengine kama hayo. Kilichopo ni wewe tu kuweza kuzingatia ushauri huo. Wapo wengine wengi ambao walishakuwa hivyo na kuweza kufurahia hali waitakayo wenyewe. Fuatilia products muhimu zilizoandaliwa kiasilia na zilizofanyiwa utafiti wa miaka zaidi ya 4000 na kuthibitishwa kutumika kwa afya ya mwanadamu kwa mafanikio na isiyokuwa na madhara.

MAGILIM
Inatokana na majina ya Magic-Slim, jina hili likabadilishwa na kuitwa Magilim.
Imetengenezwa kwa mimea kadhaa, mimea hiyo ni;

  • Seamen cassie
  • Cassia bark
  • Mullberry leaver
  • Fago fyrum tataricum
Ikiingia katika utumbo mdogo huyeyuka kuwa ute ute na gel husaidia kugandisha mafuta uliyokula ili yasitumike mwilini, na kufanya mwili kutumia mafuta yaliyoko wilini tu, hivyo kusaidia kupunguza mwili na uzito.
Ikiingia kwenye utumbo mkubwa inasaidia kugandisha maji ya nyongo na chumvi chumvi zake.
Ini huwa inavunjavunja mafuta na kutengeneza;

  • Maji ya nyongo
  • Nguvu ya mwili(glucose)
  • Uric acid
Magilim ukiinywa inasaidia kugandisha maji ya nyongo na mafuta, pia husaidia kwenda kwenye damu kutoa sukari na uchafu kupitia kwenye figo.
Matokeo yake mwili hukosa nguvu kwa kutoa sukari na mafuta, kugandishwa pamoja na maji ya nyongo kwenye utumbo mkubwa na mdogo.
Kufanya mwili kulazimika kutafuta nguvu kwenye hifadhi zake, sehemu zenye mafuta mfano kitambi, ------ na mikononi wanawake. Wanaopunguza unene na uzito hivyo mwili unatengeneza kemikali inayosaidia kutoa mafuta kwenye mwili na yanasafirishwa na damu kupelekwa kwenye ini pale ambapo ini huvunjavunja yale mafuta na kutengeneza vitu vitatu; maji ya nyongo, nguvu ya mwili ana uric acid. Wakati huo maji maji ya nyongo yanazidi kugandishwa na mafuta kwenye utumbo mkubwa na mdogo.

  1. Uric acid na sukari inatoka kupitia figo kwenye mkojo na kufanya mwili unazidi kutoa mafuta kwenye hifadhi zake mwilini na kufanya mtu azidi kupungua(kukonda).
Magilim inasaidia kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu na kuzuia mwili kunyonya vyakula vya wanga kwenye utumbo mdogo na kutoa sukari kwenye damu kupitia figo, huleta faida kwa wagonjwa wa kisukari na wale wanaotaka kujizuia kupata matatizo ya sukari.
Magilim ikiwa kwenye ute ute(gel) kwenye utumbo inasaidia kusafisha utumbo mkubwa na mdogo na kusafisha mfumo wote wa kusagia chakula.

KAZI YA MAGILIM

  • Kupunguza uzito na unene
  • Kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu
  • Kusafisha mfumo wote wa kusagia chakula
  • Inapunguza uwezo wa mwili kunyonya lishe
  • Kutoa sumu mwilini
  • Kutoa chunusi mwilini
  • Kutibu matatizo ya tumbo

CORDY ROYAL JELLY

Bidhaa hii imetokana na mmea wa cordy ceps sinensis na Royal jelly.
Royal jelly – Inatokana na chakula maalum cha malkia wa nyuki.
FAIDA ZA CORDY ROYAL JELLY

  • Ina vitamin A,B,C,D,E na K ni chakula kilichokamilika.
  • Inaondoa cholesterol
  • Inaimarisha mfumo wa damu mwilini.
  • Ina faty Acid
  • Inaongeza nguvu na kutoa uchovu na kutoa sumu mwilini
  • Inakufanya usizeeke haraka(anti aging)
  • Kulainisha ngozi na kufanya ngozi kuwa nzuri
  • Inafanya damu kuwa nyepesi
  • Inaimarisha usafirishaji wa damu mwilini
  • Kuweka kiwango cha mafuta na cholesterol sawa.
  • Mafuta yaliyoganda kuzunguka moyo na kwenye mishipa ya damu huyeyusha na kulainisha mishipa ya damu.

GOLDEN SIX

Golden Six imetokana na mimea sita(six golden herbs) inamaanisha mimea sita yenye thatmani.
Golden six inahusika na sehemu zifuatazo;

  1. Mishipa ya hisia
  2. Figo
  3. Kuinua kinga ya mwili na kinga ikiwa nyingi kwenye mwili inasaidia uroto kwenye mifupa(born marro), ndiyo inatengeneza cell za mwili.
  4. Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee.
Utendaji kazi wa Golden six;

  • Golden six ina kinga kubwa kwenye mwili, ukiitumia vizuri inakwenda kusawazisha kinga kwenye mwili.
  • Inarutubisha uroto kwenye mifupa nah ii hutengeneza chembechembe nyeupe za damu kwa haraka.
  • Golden six inasafisha figo kwa kuipa nguvu ya kusafisha damu, kuondoa sumu mwilini kama vile uric acid.
Uric acid ikiwa kwenye viungo husababisha kuumwa kwa viungo.

  • Kuhisi uchovu
  • Kutokwa na jasho sana
  • Kuumwa sehemu ya chini ya mgongo na pia kukosa usingizi.
Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee mfano;

  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kutoona vizuri
  • Misuli kukosa nguvu
  • Chembechembe za mwili kufa kwa haraka
  • Inajenga mishipa ya hisia na kuondoa matatizo ya kupooza
  • Kwa waliopooza na kuathirika kwenye mdomo (mdomo kupinda) katika mazungumzo inawasaidia na kurekebisha mazungumzo yao.
FAIDA ZA GOLDEN SIX

  • Stroke(kupooza)
  • Kukosa usingizi
  • Hypomnesis
  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kuumwa na viungo
  • Kusafisha damu
  • Husaidia presha ya kupanda inayosababisha mishipa kubana hii hutokana na aina Fulani ya Adrino gland ambayo hutoa kemikali, husababisha kubana kwa mishipa ya damu.
  • Matatizo ya wanawake na ukomo wa wanawake

Yeyote anayehitaji msaada zaidi labda kutaka kuuliza au ushauri anaweza kunipigia kupitia namba 0776491294 pia anaweza kuniandikia ujumbe kupitia ishealthy@hotmail.com
Gharama za MAGILIM ni Tsh. 62500/-, CORDY ROYAL JELLY 68000/- na GOLDEN SIX 38000/-
 

Attachments

  • MAGILIM.jpg
    15.2 KB · Views: 160
  • CORDY ROYAL JELLY.jpg
    15.7 KB · Views: 152
  • GOLDEN SIX.jpg
    14 KB · Views: 137
ahsante sn ntafanya mawacliano unisaidie,npate dawa
 
mazoezi na mpangilio wa kula vina msaada mkubwa..ni PM nikupe namna ya kufanya..unaweza kufanya mazoez hata chumbani tu na wala huhitaji vifaa.
madawa ni hatari unajenga huku unabomoa kule.
pia mazoezi ni tiba ya magonjwa mengi na yatakufanya uwe na shape nzuri.
 

Kwanini akuPM ndio umpe namna ya kufanya mazoezi,kwani ni siri unaonaje ukatoa hapa na wengine wakanufaika?otherwise kama una lako jambo
 
Kwanini akuPM ndio umpe namna ya kufanya mazoezi,kwani ni siri unaonaje ukatoa hapa na wengine wakanufaika?otherwise kama una lako jambo

natumia cm ya mchina mkuu, kuandika inanipa taabu. nilitaka tuongee on call.
ngoja nijaribu kuandika.
MPANGILIO WA KULA KWA UFUPI
1.ASUBUHI
Chai nzito, yaani asubuhi kula kama mfalme. aina zote za vyakula unaweza kula wakati huu,tena kwa wingi.mfano tunda 1, vyakula vya wanga kama mhogo, ngano n.k. Protini kama yai tena la kienyeji ndo zuri,samaki, maziwa.
usisahau kunywa maji ya kutosha tu.

2.MCHANA
Kula kiasi tu mlo wa mchana kwani asubuhi ulikula sana. hapa unatakiwa kula kama mtoto wa mfalme.
milo hii hii ya kawaida, ugali,wali, ndizi,mboga mboga,samaki.nyama.
Epuka vyakula vya mafuta, kula kwa uwoga vyakula vya mafuta ama ukiweza wacha kabisa. mafuta yanaleta tabu sana hasa kukujazia hizo nyama za tumbo na kupunguza msukumo wa damu. ukiingia google utasoma zaidi.

3.JIONI
Mlo wa jioni mkuu wangu unatakiwacule kama masikini asiyejiweza kabisa. mlo huu unahitaji kuzingatia muda. yaani inashauriwa ule masaa mawili kabla hujalala.Mfano kula saa moja jioni kisha lala saa nne au zaidi. lakini kulala vizuri ni muhimu mno, usijinyime usingizi.
watu wengi waume kwa wake hutokwa na vitambi kwa kutokuzingatia hili. mtu jioni anakula utadhani mcheza mieleka..kuku,chipsi,mayonaiz kibao, mayai...afu anasukumia maji ya baridi hapo hapo analala..ni kosa kubwa. haishauriwi kulala bila kula lakini tule kiasi kidogo usiku .mfano unaweza kula samaki, juisi na mboga mboga tu. wakati umelala mmeng'enyo wa chakula unafanyika kama kawaida, basi ni vyema mafuta kutokana na milo ya siku nzima yakameng'enywa na kumalizika au kwa kiasi kikubwa hivyo huna haja ya kula sana.

MAZOEZI
Sasa basi ukiamka unakuwa mwepesi, chakula kimemeng'enywa vyema, mafuta yamepunguzwa pia. kinachofuata ni wewe kwenda kuyapunguza zaidi kwa kufanya mazoezi (work out) japo kidogo.

MOJA YA MAZOEZI YA KUFANYA
napata shida kuelezea, natamani ningeweka picha.ila simu yangu mchina.
1. Ruka kamba japo mara mia, na utaongeza idadi kadri unavyozoea..mimi huruka mara mia tatu kila siku asubuhi. ama kama vipi kimbia ama zunguka uwanja wa mpira mara kumi au zaidi ama kama ndo siku ya kwanza basi hata mara 5..utaongeza kadri unavyozoea. kuruka kamba hata chumbani unaweza fanya ama ukumbini.
2.kama una stop watch itasaidia sana. weka fanya zoezi moja moja katika haya yafuatayo kwa sekunde 30 kila moja kwa muda wa dakika tano tu,yaani usijipe taabu, tano tu..ni nyingi sana mkuu na zuna faida kubwa mno.
Jiweke mkao wa push ups. usinyooke, tengeneza umbo la ^ . yaani 'V' iliyobinuliwa. kisha chezesha miguu yaani mguu wa kulia unaupeleka mbele kisha wakushoto unaurudisha nyuma, haraka haraka,chap chap. unaweza kufungua mziki ukafuata mapigo. utafanya hvyo kwa 30 seconds, kisha bila kupumzika utabadili zoezi, utanyooka hivyo hivyo kama unapiga push ups lakini usikunje ngumi, mkono mzima utaufanya egemeo lako. yaani sehemu ya mkono kwenye kiwiko mpaka kwenye kiganja palale chini... huku ukiwa umenyyoka kama unapiga push up..utakaa hvyo kwa sekunde 30 pia.

bila kupumzika utabadilisha zoezi,Lala chini, mgongo uwe chini, inua miguu yote juu, kunja magoti, yaani unakua umetengeneza herufi Z, umenisoma!
kisha inuka kuanzia kiuno mpka kichwa wakati miguu bado iko kama ulivyoiweka, unakua unainuka kuifuata miguu kwa selunde 30. ukimaliza hili unarudia zoezi la kwanza la kujikunja kama v iliyobiniliwa. utafanya hivyo kwa dakika 5, nilikushauri uwe na stop watch mkuu.

MAJI
Maji mkuu ni muhimu sana, kunywa kwa uchache kama lita mbili kwa siku lakini si kwa mkupuo....yaani ukiamka mpka unalala uwe umekunywa kwa kiasi hicho.

Dakika tano tu kila siku asubuhi ni ndogo sana kwa kuziangalia juu juu. lakini kwa zoezi hilo ni nyingi mnooooo. na zina faida kubwa. kama utafanya hivyo nilivyoeleza kwa wiki moja bila kuzembea...utaona mabadiliko.
fikiria kama utaweza kufanya kwa mwezi mmoja utakua katka hali gani. anza sasa kwani unaweza. unaweza kuwa katika shape unayoitamani. kila kitu niwewe mwenyewe. Bila kusahau masharti ya kula.
kama unakunywa pombe jitahidi upunguze ama uache kabisa kwani haina faida zaidi ya kukufilisi tu. najua wadau hapa wataniponda ila ndo hivyo.

nimejitahidi kadri nilivyoweza. kama patakua panamakosa pahala basi tusahihishane kiungwana wakuu.

Shukran!
 
Mkuu Mtanzanika ahsante kwa hiyo elimu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
shukran mazoez muhim,lakn kibongobongo ni kama mtu umemwambia asome biblia au quaran.
Kuanzia xaxa ni zoez 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…