Kwanini akuPM ndio umpe namna ya kufanya mazoezi,kwani ni siri unaonaje ukatoa hapa na wengine wakanufaika?otherwise kama una lako jambo
natumia cm ya mchina mkuu, kuandika inanipa taabu. nilitaka tuongee on call.
ngoja nijaribu kuandika.
MPANGILIO WA KULA KWA UFUPI
1.ASUBUHI
Chai nzito, yaani asubuhi kula kama mfalme. aina zote za vyakula unaweza kula wakati huu,tena kwa wingi.mfano tunda 1, vyakula vya wanga kama mhogo, ngano n.k. Protini kama yai tena la kienyeji ndo zuri,samaki, maziwa.
usisahau kunywa maji ya kutosha tu.
2.MCHANA
Kula kiasi tu mlo wa mchana kwani asubuhi ulikula sana. hapa unatakiwa kula kama mtoto wa mfalme.
milo hii hii ya kawaida, ugali,wali, ndizi,mboga mboga,samaki.nyama.
Epuka vyakula vya mafuta, kula kwa uwoga vyakula vya mafuta ama ukiweza wacha kabisa. mafuta yanaleta tabu sana hasa kukujazia hizo nyama za tumbo na kupunguza msukumo wa damu. ukiingia google utasoma zaidi.
3.JIONI
Mlo wa jioni mkuu wangu unatakiwacule kama masikini asiyejiweza kabisa. mlo huu unahitaji kuzingatia muda. yaani inashauriwa ule masaa mawili kabla hujalala.Mfano kula saa moja jioni kisha lala saa nne au zaidi. lakini kulala vizuri ni muhimu mno, usijinyime usingizi.
watu wengi waume kwa wake hutokwa na vitambi kwa kutokuzingatia hili. mtu jioni anakula utadhani mcheza mieleka..kuku,chipsi,mayonaiz kibao, mayai...afu anasukumia maji ya baridi hapo hapo analala..ni kosa kubwa. haishauriwi kulala bila kula lakini tule kiasi kidogo usiku .mfano unaweza kula samaki, juisi na mboga mboga tu. wakati umelala mmeng'enyo wa chakula unafanyika kama kawaida, basi ni vyema mafuta kutokana na milo ya siku nzima yakameng'enywa na kumalizika au kwa kiasi kikubwa hivyo huna haja ya kula sana.
MAZOEZI
Sasa basi ukiamka unakuwa mwepesi, chakula kimemeng'enywa vyema, mafuta yamepunguzwa pia. kinachofuata ni wewe kwenda kuyapunguza zaidi kwa kufanya mazoezi (work out) japo kidogo.
MOJA YA MAZOEZI YA KUFANYA
napata shida kuelezea, natamani ningeweka picha.ila simu yangu mchina.
1. Ruka kamba japo mara mia, na utaongeza idadi kadri unavyozoea..mimi huruka mara mia tatu kila siku asubuhi. ama kama vipi kimbia ama zunguka uwanja wa mpira mara kumi au zaidi ama kama ndo siku ya kwanza basi hata mara 5..utaongeza kadri unavyozoea. kuruka kamba hata chumbani unaweza fanya ama ukumbini.
2.kama una stop watch itasaidia sana. weka fanya zoezi moja moja katika haya yafuatayo kwa sekunde 30 kila moja kwa muda wa dakika tano tu,yaani usijipe taabu, tano tu..ni nyingi sana mkuu na zuna faida kubwa mno.
Jiweke mkao wa push ups. usinyooke, tengeneza umbo la ^ . yaani 'V' iliyobinuliwa. kisha chezesha miguu yaani mguu wa kulia unaupeleka mbele kisha wakushoto unaurudisha nyuma, haraka haraka,chap chap. unaweza kufungua mziki ukafuata mapigo. utafanya hvyo kwa 30 seconds, kisha bila kupumzika utabadili zoezi, utanyooka hivyo hivyo kama unapiga push ups lakini usikunje ngumi, mkono mzima utaufanya egemeo lako. yaani sehemu ya mkono kwenye kiwiko mpaka kwenye kiganja palale chini... huku ukiwa umenyyoka kama unapiga push up..utakaa hvyo kwa sekunde 30 pia.
bila kupumzika utabadilisha zoezi,Lala chini, mgongo uwe chini, inua miguu yote juu, kunja magoti, yaani unakua umetengeneza herufi Z, umenisoma!
kisha inuka kuanzia kiuno mpka kichwa wakati miguu bado iko kama ulivyoiweka, unakua unainuka kuifuata miguu kwa selunde 30. ukimaliza hili unarudia zoezi la kwanza la kujikunja kama v iliyobiniliwa. utafanya hivyo kwa dakika 5, nilikushauri uwe na stop watch mkuu.
MAJI
Maji mkuu ni muhimu sana, kunywa kwa uchache kama lita mbili kwa siku lakini si kwa mkupuo....yaani ukiamka mpka unalala uwe umekunywa kwa kiasi hicho.
Dakika tano tu kila siku asubuhi ni ndogo sana kwa kuziangalia juu juu. lakini kwa zoezi hilo ni nyingi mnooooo. na zina faida kubwa. kama utafanya hivyo nilivyoeleza kwa wiki moja bila kuzembea...utaona mabadiliko.
fikiria kama utaweza kufanya kwa mwezi mmoja utakua katka hali gani. anza sasa kwani unaweza. unaweza kuwa katika shape unayoitamani. kila kitu niwewe mwenyewe. Bila kusahau masharti ya kula.
kama unakunywa pombe jitahidi upunguze ama uache kabisa kwani haina faida zaidi ya kukufilisi tu. najua wadau hapa wataniponda ila ndo hivyo.
nimejitahidi kadri nilivyoweza. kama patakua panamakosa pahala basi tusahihishane kiungwana wakuu.
Shukran!