Sipendi - Special thread

Sipendi tabia za watu wanaoongea kwenye simu kwa sauti kubwa na muda mrefu ndani ya basi, tena anachoongea ni kujionesha tu. Abiria wengine yanatuhusu nini? Tena story zisizo na mbele wala nyuma alimradi tu.
 
Sipendi mtu unamtumia "pm" alafu hakujibu mpaka baada ya siku tatu au nne wakati kila siku unamuona online! sipendi,,,
 
sipendi mtu anaechukia wenzie sababu ya itikadi,Sipendi mtu anaejiona tofauti na wenzie,sipendi mtu anaekukumbuka kwa kukuomba...
 
Sipendi watu wanaoshindwa kutofautisha "r" na "l" katika kuongea na kuandika......"kiswahiri"...
Nadhani bora wajifunze "engrish"....
 
Sipendi mwanamke tumetoka out kwa mara ya kwanza mii naagiza
Safari yeye anaagiza santana.
 
sipendi tabia ya mwanamke kuchukua simu ya hawara au bwana wake kusearch na kuanza pigia watu kuwauliza we nani!!!! mkome!!!! kujidhalilisha tu
 
Sipendi mtu anafungulia redio kama yupo bar si ufungue tu kiasi cha kuweza kuskiliza mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…