Nimejichanga weeeee nikafanikiwa kununua ka Vits kangu cha kunisaidia kwenye misele yangu. Siku moja nipo na baba mkwe wangu nampeleka hospitali, tukiwa tunasubiri kuruhusiwa kwenye mataa pembeni kulikuwa na Range Rover anaendesha kijana kama mimi tu. Baba mkwe wangu akaniuliza, *"mkwe!* *umemuona mwanaume huyo?"* Nilishikwa na hasira nikajikuta nimemjibu *"kuwa na baba mkwe tajiri raha sana, jamaa alipewa hiyo gari kama zawadi na baba mkwe wake siku ya harusi yake"* Basi baba mkwe wangu akanyamaza kimya akawa mdooooooogo.
*Pumbavu!* *huwa sipendi dharau mimi*