Naamini sana katika uwepo na uwezo wa Mungu kama mtu anaweza kufanya mawasiliano sahihi na Muumba huwa anajibu maombi na kutoa msaada. Ila wengi wetu hatujui namna ya kuwasiliana ili kupata majibu. Sio nia yangu kuzungumzia hili kwa sasa ila natoa tahadhari/angalizo:
Ulimwengu wa giza hutumia fursa zinazokuja katika maisha ya binadamu kama vile magojwa, hofu, makosa, nk ili kufanikisha agenda yake. Mfano mtu anaweza kuugua ugonjwa unaopona ila kwasababu ya hofu au uzembe wa kwenda hospitali mgonjwa akafariki. Kifo cha mtu kisichotokana na mapenzi ya Mungu Mwenyezi kina faida kwa ulimwengu wa giza sana (sitazungumzia hilo leo).
Hivyo basi wakati huu wa corona kuna vifo vingi vitatokea ambavyo vingine ni kweli vinatokana na corona na vingine ni kwasababu tu adui (Shetani na watu wake) wamepata mwanya au sababu ya kuwaaminisha watu. Nawasihi kuweni makini sana kwani pia licha ya corona kuwepo pia zipo sababu za kutengeneza vifo kwa wingi wakati huu kuliko wakati mwingine wowote kwani vinavyohitajika na kuzimu vipo vyote: kisingizio (scapegoat), makosa, hofu, nia mbaya na wenye kuhitaji kupata msaada wa shetani katika mambo yao.
Epuka makosa yoyote dhidi ya corona, chukua tahadhari zote, ondokana na hofu na sali kwa Mungu wa Kweli (bahati mbaya wengi wetu tumedanganywa kuwa mizimu, wafu na majini ni Mungu wa kweli). Hii hufanya suala zima la kupata msaada wa Mungu kutoleta matokeo chanya kwa walio wengi.