Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Wewe hujui maana ya shida.

Kwanza kwanini ulisoma?
Miaka yote hiyo alafu uje kulipwa mill1 kila mwezi?
 
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
 
Nakusikitikia mleta mada.
Mameno yako yatakugharimu.
Utaikosa hata laki mbili,na vyeti utatamani uvichome
 
Wahenga wanakuambia ata mbuyu ulianza kama mchicha.
Unaweza fanya kwa malengo na kuongeza CV yako maana watu wakozi yako wapo weng na wengn wana experience Hao sasa ndo wanalipwa mshahara unao taka ww lkn ww unaenda kujifunza kazi .
Au amua moja usiajiliwe fanya mishe zako mwenyewe
 
my ex galfrend ana diploma ya mambo hayo,alinichanganya katafuta kazi wiki 3 tu,kapata bank mshaara laki 9,wakati nna washikaji mwaka wa kumi sasa wanatafuta ajira,.wanawake mna bahati
 
my ex galfrend ana diploma ya mambo hayo,alinichanganya katafuta kazi wiki 3 tu,kapata bank mshaara laki 9,wakati nna washikaji mwaka wa kumi sasa wanatafuta ajira,.wanawake mna bahati
duuh watu wana mibahati!
Bank gani mkuu.
 
Mie ni muhitimu wa Degree ya Kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
Sorry kuuliza.

Wewe ni demu?
 
Hajui ugumu wa mtaani huyu, wahitimu wengi hua na matumaini makubwa sana kuliko uhalisia na ndio maana wanapata msongo wa mawazo,
Kipindi hicho namaliza chuo rafiki yangu mmoja alisema bila 2m take home hafanyi kazi, ajabu zaidi alianza na laki 8 kwa mchina.
Ila wachina wanaokoa??!! Ache ni tu!
 
Daah! Mwaka Jana tu nimetoka ongea na Mdogo wangu juu ya hizo Ndoto za kujitanua kwa kuwa amemaliza degree so anahitaji salary kubwa ya kuanza nayo but naona Maisha yamemnyoosha Sana hapa nyumbani tumemkatia service muhimu tumeacha apate msosi tu.Nguo, Vijihela vya out na mambo mengine atajijua Mwenyewe, Maisha ni Mwalimu Sana ujue ,so ikabidi ajiongeze atafte par t- time pahala flan pamoja na degree hiyo amekubali wanampa nauli Tsh 300. Sasa wewe na hiyo kadree kako ka makalculations yasiyo na maana endelea kuringa tu,utakuta na wwnzio kwenye interviews wakuwa na CPA,ACCA na ndio wataupata huo Take-home milioni Moja.
Hakuna ofisi itatoa shilingi 300 kwa siku labda useme ni 3000 kwa siku. Sasa huyo mdogo wako si auze matunda na juice mtaani kuliko kuchomekea ofisini bila malipo
 
Attitude is like a price tag. It shows how valuable you are (Anonymous).
**Kwa attitude hii, hutoboi. Endelea kuangalia tamthilia Hapo kwa shemeji.
1687664995452.png
 
Back
Top Bottom