Sir Matt Busby: Manchester United is my heaven

Sir Matt Busby: Manchester United is my heaven

Marcovicsavic

Senior Member
Joined
Nov 14, 2020
Posts
130
Reaction score
303
By Kondo R Kondo

Ukienda Signal iduna Park uwanja wa nyumbani kabisa wa Borrusia Dortimund utamkuta mtoto wa Nyumbani Marco Reus, fundi alie weka maslahi nyuma loyalty mbele, pale Signal hata wapelekwe Ronaldo na Messi the Yellow and Black wata muimba Kwanza Reus alafu wengine watafata, kwao ukizungumzia Loyalty basi una mzungumzia Marco Reus mtoto wa nyumbani,

Pita pita mitaa ya jiji kongwe na la kihistoria la Roma ambapo ndio maskani ya clabu ya Asaziano Sportiva Roma (AS ROMA) kuna stika nyingi sana za Francisco Totti kuliko mtu yoyote, si raisi wala mbunge anae fikia hata nusu ya stika za Totti jijini Roma, huyu ndio alitoa kauli ya kishujaa akisema "NAWEZA KUMSALITI MKE WANGU LAKINI SIO AS ROMA"

Watu hukumbukwa sio kwa ubora au uzuri walio nao bali uaminifu wao kwetu, ni kwa kiasi gani wali baki nasi wakati hatuna cha kuwapa ilhali walikuwepo walio onyesha nia ya kuwapa kila walicho taka..

"MANCHESTER UNITED IS MY HEAVEN" ndio bango kubwa zaidi linalo someka vema upande wa kusini mashariki mwa Old Trafford ukimaanisha "Manchester united ndio pepo yangu" kauli ya Legend Sir Matt Busby alie wahi kua Mcheji na Kocha wa Manchester United kwa nyakati tofauti,

Kauli hii ilikuja baada ya kukataa ofa nono ya kibarua cha ukocha wa real Madrid,

Baada ya Manchester united kutwaa ubingwa wa ligi mwaka 1956 alie kua Raisi wa Real Madrid wakati huo bwana Santiago Bernabeu alimpa ofa hii kwa kuchombeza kua ange mpa HEAVEN(Pepo) kama angekubari ofa ile ,

Majibu yalirudi kua "MANCHESTER UNITED IS HEAVEN"

Manchester united wamepita wachezaji bora wengi sana walio ipa klabu mafanikio ya ndani na nje ya uwanja, lakini Busby anakumbukwa kwa kipekee sana kiasi cha jukwa la VVIP la old Trafford Kupewa jina lake "SIR MATT BUSBY STAND" huku likiwa na nakshi ya kauli ya kibabae "Manchester united is my heaven"
anakumbukwa zaidi kwa uaminifu wake kwa klabu kuliko mechi alizo shinda kama kocha.

Hii hata kwenye maisha ya kwaida, tuna waenzi na kuwakumbuka zaidi wale walio chagua upande wetu licha ya kwamba haukua upande wenye mavuno zaidi,
View attachment 2713395
 
Back
Top Bottom