kwanza nataka nijue, ni nini kilmsukuma necha hadi akam-dis dogo. unajua kama umepitwa kimaendeleo ni vizuri ukafurahi kuona mwenzako amefikia pale ambapo wewe ulishindwa. kitendo cha yeye kum-diss dogo kimetu-show jinsi gani upeo wa necha ulivyo finyu. hii ishu inanikumbusha miaka fulani lile kundi lao lilipovunjika, walipojitenga na wenzao wakaanza kuwaimbia nyimbo za kuwasema. nilipokuwa nasikiliza facts zao za kujitoa kule kwenye kundi walisema said fella alikuwa anawanyonya ndo maana wakaondoka. sasa nikawa najiuliza sasa kama aliyekuwa anawanyonya alikuwa ni boss wenu inangia vipi akilini mlipoondoka na kuanza kuwasema wenzenu waliobaki na kuanza kutuletea mipashu kwenye hip hip. yaani ni kama mimi niache kazi kampuni fulani kwa sababu naona nalipwa kidogo halafu baada ya kuondoka eti nianze kuwaponda wenzangu waliobaki kwenye ile kampuni eti kwa nini hawakutoka ka mie. ndo maana unaona hakuvuma kama ile miaka ya 2004 si yeye hata wale alioondoka nao wapo kimya. ila kina chege na temba bado tunawasikia wakitoa nyimbo zao on air. so we juma nature linda heshima yako. kama akikata kiuno ni yeye na fans wake, nyie mbona mnajipinda na mapanga yenu. utaishia kumponda ila yeye anaingiza dooh, JIPANGE