Siri 6 za Ali Kiba kumuoa Mkenya hizi hapa

Siri 6 za Ali Kiba kumuoa Mkenya hizi hapa

Uliyoyasema kweli kaka. Nilisoma na huyu mrembo chuo cha United States International University (USIU) pale Nairobi darasa moja. Yupo vzr sana. Secondary alisoma star of the sea pale mombasa-shule ya wanawake watupu. Namkumbuka upole wake darasani
Mbona hukumchombeza? Au ndo domo zege? Hiv Wolpa amefika hata darasa la 7?
 
UMESAHAU SIFA YA 7 wanawake wa MOMBASA,,,, kutoa KITUNGUU..8 ...HAWATAWALIKI na MUME,,,NA HUPENDA KUWA JUU YA WAUME ZAO,,,,pia wabinafsi hawapendi NDUGU WA MUME....time will tell,,,,Mimi ni mzaliwa wa TANGA,,,na HATUOI MOMBASA,,NI KWELI WANAJUWA KUPIKA MAPOCHOPOCHO,,wana NYAMA TAMU YA ULIMI,,,WANAJIWA MAHABA,,,,,lakini wanawake wa MOMBASA NI MCHARUKO ZAIDI ya DADA ZETU WA BONGO,,,ukidanganyika na NYAMA YA ULIMI WAO,,,,na MAHABA YAO,,,hakika UMEPOTEA...
 
Nilijua kuna wachambuzi wa mambo ya soka tu kumbe hata mambo ya uoaji kuna wachambuzi.
 
Kama shule Jokate ana masters na alikuwa bright sana darasani. Sema labda utulivu ndio zero, na ile kuchezewa na watu kama Diamond kulishusha thamani yake kabisa
Jokate hiyo masters kapata wapi zaidi ya ile degree yake ya sociology?[emoji33][emoji33]
 
Jokate hiyo masters kapata wapi zaidi ya ile degree yake ya sociology?[emoji33][emoji33]
Sorry kwa kujaribu kuwadanganya, sina chochote nnachojua juu ya Jokate zaidi ya ile product yake ya malapa [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Tatizo ni kwamba mnaangalia wanawake wa kwenye social medias na celebrities halafu mnageneralise.
Shida hata huyo ambae sio maarufu nae akisha olewa na supa staa atataka nae kujionyesha ujue
 
ALIKIBA-4.jpg

Juzi alfajiri ya Aprili 19, mwaka huu, Kiba alifunga ndoa na mrembo Amina Khaleef katika Msikiti wa Ummul Kulthum uliopo mjini Mombasa, Kenya. Ndoa hiyo ilifungishwa na Sheikh Mohamed Kagera.
Hakika ilikuwa ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi hao, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mjini Mombasa mara baada ya ndoa hiyo kufungwa.

Mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, mitandaoni kulichafuka ambapo baadhi ya mashabiki wa Kiba walikuwa wakihoji ni kwa nini mkali huyo wa Wimbo wa Seduce Me ameacha warembo kibao Bongo na kwenda kwa Amina wa Mombasa? Kufuatia wengi kutaka kujua Amina ni nani au ana nini cha tofauti kilichomteka Kiba, Risasi Jumamosi lilifanya uchunguzi wake wa kushiba na kuibuka na siri sita zilizomvutia Kiba kwa mrembo huyo na kuwasahau kabisa warembo wa Bongo;
ALIKIBA-1.jpg
1: SIFA YA KUWA MKE
Uchunguzi huo ulibaini kwamba, Amina ambaye aliingia kwenye uhusiano wa uchumba na Kiba mwaka 2016, ana sifa za kuwa mke (wife material) na pia anafaa kuwa mama bora kutokana na utulivu wake na kujua malezi kwa jumla. Ilibainika kwamba, Amina ni binti mwenye maadili na aliyekulia kwenye familia iliyoshika mno Dini ya Kiislam hivyo ‘amekwiva’ kwenye eneo hilo la kuwa mama bora wa familia ukilinganisha na warembo wengi wa Kibongo ambao ilisemekana, wengi hawajatulia na hawajashika dini kwa dhati zaidi ya kuigiza tu.



2: SIYO TEGEMEZI, NI MCHAPAKAZI
Uchunguzi huo uliotumia watu wa nyumbani kwa akina Amina ulibaini kwamba, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23, siyo mtu wa kukaa tu nyumbani na kusubiri kuletewa pizza au chipsi kuku na mwanaume, bali ni mchapakazi asiyependa kuwa tegemezi, tofauti na mabinti wengi wa Kibongo ambao hubweteka na kutegemea kila kitu kutoka kwa wanaume.

3: SHULE IPO KICHWANI
Ilifahamika kwamba, Amina hakukimbia umande kwani ni msomi mwenye shule yake kichwani, akiwa amehitimu masomo ya uhasibu kwa levo ya chuo kikuu na kuwa mfanyakazi wa serikalini katika Kaunti ya Mombasa. Hii ni tofauti na baadhi ya mabinti wa Kibongo ambao wengi walikimbia umande.


4: UZURI WAKE SIYO FEKI
Ukimtazama Amina hata kwenye picha zilizosambaa mitandaoni, utagundua kuwa uzuri wake ni wa asili na siyo wa kutengeneza yaani feki kama walivyo warembo wengi wa Kibongo. Ilielezwa kuwa, kutokana na mvuto wa kipekee alionao, basi Amina amebeba maana halisi ya uzuri wa mwanamke. Hana makalio feki ya kutengeneza wala nido zake kifuani siyo za kubusti na hategemei make-up ili aonekane mzuri bali kila kitu kwake ni cha asili.


5: HASHINDI NA KUKESHA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Uchunguzi wetu huo ulibaini pia kwamba, Amina siyo mtu wa kushinda na kukesha kwenye mitandao ya kijamii kama walivyo warembo wengi ambao kazi yao huwa ni kuposti picha na video za kuwatamanisha wanaume. Katika kuthibitisha hilo, tangu aingie kwenye uhusiano na staa huyo mkubwa ambaye kwa mrembo mwingine angefanya matangazo kwenye mitandao ya kijamii hadi dunia nzima ijue, lakini Amina yeye hakuwahi kufanya hivyo.


6: ANAJUA ATAKAVYODILI NA WALIOMZALIA KIBA
Ilifahamika kwamba, Kiba ana watoto watatu ambao kila mmoja ana mama yake, lakini ilisemekana Amina alimhakikishia atakavyodili na mama wa watoto hayo na yupo tayari kuwalea bila kusababisha drama au tafrani. Sifa nyingine aliyoelezwa kuwa nayo Amina ni pamoja na kujua kutunza siri za familia kama alivyofanya kwenye uhusiano wake na Kiba tangu mwaka 2016 bila kujali skendo zilizokuwa zikimuandana staa huyo.


MASKINI MASTAA HAWA, BAHATI HAIKUWA YAO

Kabla ya kumuoa Amina, Kiba aliwahi kutajwa kutoka na warembo mbalimbali wakiwemo wanawake watatu aliozaa nao, mastaa wa Kibongo, Jokate Mwegelo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jacqueline Wolper na wengineo ambao mashabiki wao wengi waliwahurumia kwa kukosa bahati ya kuolewa na staa huyo anayejiita Pasua Kichwa


Mhanga mwingine huyu wa kukataliwa na Wanawake sasa amegeuka adui wa dada zetu wa Kitanzania, beef your game labda next time utafanikiwa kupata Mwanamke atakaye kukubali, acha kutafuta Mchawi Wanawake Dunia nzima wako sawa, kama hauna game hauwakukubali ni rahisi kihivyo tu!
 
Vipi chumbani anajua kukata mauno? Maana mmemchambua kama dagaa
 
UMESAHAU SIFA YA 7 wanawake wa MOMBASA,,,, kutoa KITUNGUU..8 ...HAWATAWALIKI na MUME,,,NA HUPENDA KUWA JUU YA WAUME ZAO,,,,pia wabinafsi hawapendi NDUGU WA MUME....time will tell,,,,Mimi ni mzaliwa wa TANGA,,,na HATUOI MOMBASA,,NI KWELI WANAJUWA KUPIKA MAPOCHOPOCHO,,wana NYAMA TAMU YA ULIMI,,,WANAJIWA MAHABA,,,,,lakini wanawake wa MOMBASA NI MCHARUKO ZAIDI ya DADA ZETU WA BONGO,,,ukidanganyika na NYAMA YA ULIMI WAO,,,,na MAHABA YAO,,,hakika UMEPOTEA...
Wa Mombasa sio mchezo...Bibi yangu alitoka huko na kuolewa Bongo....Alikuwa moto wa kuotewa mbali...ndugu za babu hawakukanyanga kwake....Ila alijua sana biashara na alisisitiza sana elimu...Babu hakudhubutu kuoa mwingine...
 
Back
Top Bottom