Siri hii hapa ya kutajirika kwa vijana wa kitanzania

MTAKATIFU GIOVANI

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
342
Reaction score
112
Nimemaliza kufanya utafiti wangu siku mbili zilizopita, nafikiri ni vizuri baadhi ya mambo machache nikayaweka hadharani ili wale vijana wetu wenye nia ya dhati ya kujikwamua kimaisha waweze kuitumia. Ukiwa una kianzio cha tshs. 80,000/= na ukaamua kurudi kijijini kulima, na kwa kuanzia ukaanza na heka moja ambayo ukajitahidi kuihudumia vizuri pamoja na mifugo michache kama sungura kuku, bata, njiwa n.k. Mwaka unaofuata ukaongeza heka tano zaidi na mifugo kama mbuzi, ng'ombe, kitimoto(kwa wale ambao imani yao haiwazuii) na mwaka unaofuata ukaongeza heka kumi zaidi ukawa na jumla ya heka kumi na sita, utafiti umeonyesha ndani ya miaka mitano huyu kijana atakuwa na fuso moja, gari ndogo ya kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi yeye na familia yake. Zao ambalo linashauriwa kuanza nalo ni ufuta, lakini ni muhimu kulima chakula kidogo na mboga. Nakaribisha mjadala kwa ajili kuboresha zaidi.
 
Mkuu unayoyaongea kweli kabisa kuna rafiki angu kafika apa mbeya mwezi wa tano wa kumi kalima nyanya kwa garama ya milioni moja juzi kamalizia kukusanya milioni tano
 
Ni wazo zuri ila sio "realistic" na "achievable" kwani kwa sasa garama ya kuhudumia shamba kwa heka inategemea na eneo shamba lilipo, mfano kuna sehem kama huku wilaya ya kilombero kukodi tu shamba ni kuanzia elfu 40 hadi laki 1 kwa heka. na hapo bado garama zingine kama kulimisha, kungolea, dawa, kuvuna na e.t.c kwa iyo hiyo elf 80 haitoshi kabisa, labda kuanzia laki na nusu hadi laki 2 kwa eka. Shukran
 
mkuu hujasema ni jinsi gani unaweza kufanya hiyo mifugo ikaoongezeka na pia ni jinsi gani hizo hekari zikaaongezeka, je nilazima kuyafanya hayo nikiwa kijijini/ je nikiwa mjni alafu nikawa na shamba kibaha haiwezekani.? Je ni vijiji vyote huo ufuta unaweza kuota ( aina za hali ya hewa). hujazungumza kuhusu soko la hiyo bizaa.

Ukiamua kutoa ushauri kuhusu maswala muhimu katika maisha ni bora kuandika kwa undani ili kuwa faida kwa wengi, umesema mtaji wa sh 80000 lakini hujasema hiyo pesa ni kwaajili ya nini, je kununulia shamba au kukodisha shamba, je ni pesa ya vifaa vya kilimo ( pembejeo) au mbolea na mbegu. hujasema kuwa ni utafiti umefanya au ni wewe mwenyewe ndo umefanya kwa vitendo, na je ni applicable kwa kila mtu?

Ninavyo amini mimi ni kuwa biashara ya kilimo inaweza kumtoa mtu kirahsi sana LAKINI ina hitaji umakini wa hali ya juu sana tofauti na ulivyo shauri wewe kirahisi rahisi hivyo. kama ingekuwa rahisi hivyo unafikiri ni nani angekimbialia mjini kwenda kuuza maji.

Nimekuwa nikiwaambia rafiki zangu kuwa siku naamua kuacha ajira ya weledi ninayofanya, nakwenda kufanya kazi ya kilimo, lakini si aina ya kilimo ulicho ainisha wewe, sio kilimo kwanza wala sio kilimo cha uti wa mgongo sera zinazo tumika na zilizotumika kuwadanganya wananchi wala hazina mashiko katika uhalisia.
 
Mkuu hiyo ni kweli kabisa kuna rafik yangu alikuwa mjini sasa kila siku alikuwa ananipigia simu kuniomba pesa na kulalamika maisha magumu.

Nikamshauri arudi kwao mbeya alime mpunga nikampa laki 750,000 .lak 5 awekeze kwenye mpunga na 250,000 ufugaji wa kuku. Ilikuwa mwaka juzi.

Sasa hivi ana million 10 kwenye account ya benk na ameapa kutorud mjin tena .

Tatizo la vijana kutaka kukaa mijin tu waonekane wanaishi Dar litawacost
 

Red: quite interesting...
 
umesema ukiwa na 80,000,haujasema shamba,mbegu,mbolea wafanyakazi kawapataje?
 
80000 Acha bana hvo haiwezekani..garama yakulima shamba naukapata angalau n kuanzia milion nakuendelea..hapo faid utaon
 
na kuna kauli moja huwa inaumiwa sana ujanja sio kuzaliwa mjini ujanja ni unaishi vipi mjini

 
taarifa yenyewe ni ndefu sana kiasi kwamba nikiitoa kama ilivyo wananchi wataingiwa na uvivu wa kuisoma, lakini kwa kifupi ni kwamba nimetaja zao moja tu ufuta kama mfano, yapo mazao mengine mengi tu kulingana na eneo unalotaka kwenda kama ndugu yangu mmoja alivyosema kuwa hata nyanya zinalipa.
 
Ukweli ni kwamba sio kila mtu ni mkulima. hivyo hayo mawazo yaweza kufanikiwa kwa mtu ambaye anaupenda ukulima. kwa anaeuchukia hawezi vumilia miezi ya kusubiria mavuno huku huna hata senti moja mfukoni.
 
:mvutaji:
umesema ukiwa na 80,000,haujasema shamba,mbegu,mbolea wafanyakazi kawapataje?
mtaji wa masikini ni nguvu zake, wewe ndiyo unaanza unataka vibarua, mbolea ya kisasa, kukodi shamba etc. kwa mtindo huo huwezi kujikomboa. lazima ujitolee, na wakati mwingine uende kufanya vibarua kwenye mashamba ya wenzako ili kuongeza pesa kidogo ya kujikimu.
 

True kilimo ni njia nzuri ya kufikia mafanikio,lakini tusizuie hekima zetu kuuona ugumu wa kilimo,kujitoa mhanga na kuwa mvumilivu!
 
Ukweli ni kwamba sio kila mtu ni mkulima. hivyo hayo mawazo yaweza kufanikiwa kwa mtu ambaye anaupenda ukulima. kwa anaeuchukia hawezi vumilia miezi ya kusubiria mavuno huku huna hata senti moja mfukoni.

Ndio maana hapa hajalazimishwa mtu ni ushauri tu.

Pia kipindi unasubiria mavuno unaweza kuwa unafanya vibarua au shughuli nyingine ndogo ndogo za kuingiza kipato mara nying shughuli za shamba ufanywa asubuh sana au jioni
 

Utafiti Huu umeufanya mkoa gani na umezingatia rutuba za ardhi na kadhalika na je umeangalia MV ya sehemu yenyewe etc etc


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unazungumzia kijiji gani mkuu?mimi nililima ekari 10 za maharage na mahindi mvua zilikata nikaambulia debe nne za maharage na mabua ya mahindi ya kulishia mifugo nilijuta na kuapa sitorudia kulima kilimo cha kutegemea mvua!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mkuu kuna maswali muhimu sana wadau wanauliza na yanahitaji majibu kutoka kwako...

Itakuwa jambo la busara sana kama utatuwekea hapa huo utafiti wako ninaouamini utakuwa mzuri sana kwa maelezo ya kina, kuna watu ambao tupo interested tutasoma tuu ma kufanyia kazi (ndo jukumu zima la kufanya research)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…