Siri hii hapa ya kutajirika kwa vijana wa kitanzania

Siri hii hapa ya kutajirika kwa vijana wa kitanzania

Kilimo kwa TZ ni mchezo wa kamali maana tunategemea mvua. Kuna jamaa alikopa mamilioni benki akawekeza kwenye kilimo. Mvua zikagoma mazao yakakauka. Jamaa aliishia kuji-RIP maana benki ilikuwa inamdai pesa yake pamoja na riba. Nashauri mtu kama anawekeza ktk kilimo bora aanze na pesa yake sio kukopa!
 
chakula pekee kwa matumizi ya 1000 kwa siku,sawa na siku 80=miezi miwili na siku 20. na kilimo mpaka kuvuna kinaweza chukua zaidi miezi mitano
 
Mkuu na wachagia mada wote, ukweli upo, nakujitegemea ni vyema kama mimi hapa natamani sn kupata eneo na fedha kiasi nikafanye kazi kwa mikono yangu. Na mdau unae toa huu utafiti ni bora ukatoa mchanganuo, coz tupo mjini tunaelimu bt kazi za kuajiriwa zinazokupa mshahara wa kuweza kila kulipa daladala ya kwenda na kurudi. So tuwekane wazi maana tuko tayari kuishi ktk ukweli
 
Unazungumzia kijiji gani mkuu?mimi nililima ekari 10 za maharage na mahindi mvua zilikata nikaambulia debe nne za maharage na mabua ya mahindi ya kulishia mifugo nilijuta na kuapa sitorudia kulima kilimo cha kutegemea mvua!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
kilimo cha kutegemea mvua ni patapotea.
 
Utafiti Huu umeufanya mkoa gani na umezingatia rutuba za ardhi na kadhalika na je umeangalia MV ya sehemu yenyewe etc etc


Sent from my iPhone using JamiiForums
natarajia kuitoa taarifa yote hadharani kwa hiyo uwe mvumilivu maana inapitia kwenye mchakato wa kitaaluma na kisheria.
 
Nimemaliza kufanya utafiti wangu siku mbili zilizopita, nafikiri ni vizuri baadhi ya mambo machache nikayaweka hadharani ili wale vijana wetu wenye nia yadhati ya kujikwamua kimaisha waweze kuitumia. Ukiwa una kianzio cha tshs. 80,000/= na ukaamua kurudi kijijini kulima, na kwa kuanzia ukaanza na heka moja ambayo ukajitahidi kuihudumia vizuri pamoja na mifugo michache kama sungura kuku, bata, njiwa n.k. Mwaka unaofuata ukaongeza heka tano zaidi na mifugo kama mbuzi, ng'ombe, kitimoto(kwa wale ambao imani yao haiwazuii) na mwaka unaofuata ukaongeza heka kumi zaidi ukawa na jumla ya heka kumi na sita, utafiti umeonyesha ndani ya miaka mitano huyu kijana atakuwa na fuso moja, gari ndogo ya kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi yeye na familia yake. Zao ambalo linashauriwa kuanza nalo ni ufuta, lakini ni muhimu kulima chakula kidogo na mboga. Nakaribisha mjadala kwa ajili kuboresha zaidi.


hivi wewe unaandika ujumbe huu ukiwa wapi?mjini au kijijini?nilitegemea ungekuja hapa kutueleza ni kiasi gani umefanikiwa kwa hiyo elfu 80.kwanza ndugu. zako wako huko vijijini wana shida mpaka uvunguni.kwanini usiwapo huo ushauri na hizo elf 80 ili watoke na wao?mbona unakuwa kama li ccm?ushauri kama huu ni lazima tu utakuwa umetolewa na ma ccm,kuwafanya watu wajinga eti wanaeeza kutoka kwa kiasi kidogo huku menyewe yakikalia kuiba tu
 
Back
Top Bottom