Fahamu kwamba mwanamke uliye naye ana siri nyingi alizoficha zikiwemo chache ambazo hukuwahi kuzifikiria hata mara moja.
Je, ulikuwa unafahamu kuwa kila kitu mwanamke anachonunua kuanzia nguo zake, viatu na hata madawa huwa na gharama halisi ya asilimia 20 zaidi ya ile anayomweleza mwenzi wake? Kwa mfano anaweza kumwambia mwenzi wake kanunua kiatu kwa shilingi 8,000, lakini ukweli halisi wa bei ya kiatu hicho alinunua kwa shilingi 10,000! Mara nyingi wanawake hutaja bei ya chini ya vitu vyao wanavyonunua kwa waume zao ili wasionekane waharibifu wa fedha au kuepuka kuzua zogo bure na wenzi wao.
Je ulikuwa unafahamu kuwa wanawake wanakuwa wawazi zaidi kwa mashoga zao kuliko walivyo kwa wapenzi au waume zao? Kama ulikuwa hufahamu juu ya hilo, basi kwa taarifa yako ni kwamba ni rahisi sana wanawake kuaminiana kiasi cha kuelezana siri zao kama ni marafiki wanaoaminiana sana. Huweza kuwaeleza marafiki zao kuhusu hata mzozo mdogo unaotokea kati yao na wapenzi wao. Kuwaeleza kuhusu vile wanavyotendewa na wakwe na mawifi zao. Kulalamikia jinsi wapenzi wao wanavyoonekana kuthamini zaidi burudani fulani kiasi cha kutumia muda wao wote huko.
Nitaendelea kuweka siri zao nyingi hapa!