Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za jioni wana JF mada ya leo pia ni sensitive kidogo maana inagusa imani za watu ila kutokana na kuwepo hitaji la kuweka rekodi sawa nimeona nilete uzi huu ili tujifunze zaidi

Na sababu kubwa ya kuleta uzi huu ni kutokana na mada nazoleta humu nyingi zinatumia pia vitabu nje ya biblia kama source ya taarifa na kumekuwa na wengi wanaokuja na hoja kwamba chochote kilicho nje ya biblia sio kweli yaani quran, Midrash, Tanakh/torah, zohar, apocrypha, Pseudipigrapha zote ni batili sasa ni kutokana na hoja hiyo imenipelekea kuandaa uzi huu hivyo tuusome kwa makini na tuujadili kwa ustaarabu tu yote kwa yote kujifunza. Nitaugawa uzi huu kwa sehemu mbili ili iwe rahisi kuusoma na ningependa kabla ya kuchangia uusome wote na kuuelewa. Karibuni

unnamed (6).jpg


UTANGULIZI
1. Biblia ni mjumuiko wa vitabu vya manabii walivyoandika kuhifadhi matukio katika historia ya imani yao kwa Mungu na ilikusanywa katika karne ya 3 baada ya Yesu baada ya kuonekana vitabu vya kiimani viko vingi vinakinzana hivyo wakaamua wawe na kitabu kimoja cha kutumika na wote na ilikuwa katika kigiriki na kiebrania. Baada ya karne zaidi ya 10 kupita biblia ya mapema kabisa kutafsiriwa kuingia kwenye kilatin iliyokuwa lugha ya Roma, ilikuwa ''Vulgate'' iliyotoholewa kutoka kiebrania na kigiriki kwenda kilatin na padre Jerome karne ya 14 ila tafsiri ya kiingereza ilikuwa king james version karne ya 15 ambayo hata biblia za kiswahili na lugha zingine maelfu zimetoholewa hapo na ambacho wengi hatujui ni kwamba vitabu ambavyo leo tunaviita apocrypha vilikuwepo kwenye KJV ya kwanza ila mataifa mengi yalipotafsiri hayakuvijumuisha hivyo vitabu 14! Na leo hii ukivitumia humu JF kujenga hoja utaambiwa ni vya kishetani wakati biblia ya kwanza ya english iliviweka??

Miaka mingi ikapita ndipo yakaja matoleo mengine tofauti ila kwa karne hii biblia inayotambulika kutumika dunia nzima ni NIV yaani New International Version ya 1973, ambayo ilikuja kufanya utafiti na kutumia vyanzo mbalimbali vya nyuma zaidi na kutengeneza tafsiri yake na muhimu hapa tufahamu NIV iligundua makosa kwenye KJV na ikafuta mistari hiyo kwa kigezo kwamba mistari hiyo haikuwepo kwenye vyanzo vya mwanzo ikimaanisha viliongezwa baadae sana. Baadhi ya mistari ilioongezwa na ambayo NIV imeifuta ama kutoitambua Ni Marko 11:26, 15:28,9:44,9:46 Mathayo 23:14,18:11,17:21, Luka 17:36 Yohana 5:3-4, Matendo 8:37 n.k kwa uchache wake ila mingi zaidi iligundulika haikuepo kwenye vyanzo vya mwanzoni kabisa na kwamba vimeongezwa kinyemela.

Simply ikimaanisha biblia ya kiswahili tunayotumia hii ya chama cha biblia iliyotokana na KJV tumepotoshwa? Je wakristo tumeambiwa haya kanisani?

Je nani mkweli kati ya KJV na NIV??
images (44).jpg

VITABU VILIVYOPUNGUZWA
Baada ya biblia ya nwanzoni kabisa ya kilatin kuwa na vitabu zaidi ya 76 na version zingine hadi 84 kuna vitabu vilitolewa na kina Jerome kwa sababu mbalimbali ikiwemo kughushiwa majina, kutovuviwa na Roho mtakatifu, kukinzana na vitabu vingine vya Biblia, kuandikwa na manabii wa uongo, utata wa maandiko n.k na vitabu hivyo ni kama 4 Maccabees, Assumption of Moses, Ethiopic Book of Enoch (1 Enoch), Slavonic Second Book of Enoch, Book of Jubilees, 3 Baruch, Letter of Aristeas, Life of Adam and Eve, Ascension of Isaiah, Psalms of Solomon, Sibylline Oracles, 2 Baruch, Testaments of the Twelve Patriarchs na vinginevyo na hii ndio kitovu cha uzi huu embu basi tuchambue kwa pamoja.

51CNcfbWCqL._AC_SY400_.jpg


TATIZO LA UANDISHI
Kuna hoja zilitolewa kwamba hivi vitabu vilivyoachwa kwenye biblia yaani Pseudipigrapha na Apocrypha mfano book of Enoch, Book of Adam & Eve n.k kwamba vilitolewa kwenye biblia sababu kuna utata juu ya waandishi na kwamba kurasa zingine ziliongezwa baadae.... Ila leo hii wanatheolojia wote duniani wanakubali kuwa biblia bado ina pseudipigraphi nyingi mfano Isaya iliandikwa karne 8 kabla ya kristo yaani sura 1-39, ila kipande kuanzia sura 40-55 iliandikwa na mtu ambaye hajatambuliwa mpaka leo huko babeli na sura 56 mpaka 66 imegundulika na wanatheolojia dunia nzima kuwa ziliongezwa baadae yaani miaka mia kadhaa tokea isaya akiandike!!!

Hata Jeremia kuanzia sura ya 26 iliongezwa miaka mamia baadae!! Hivyo swali la kujiuliza kwanini basi vitabu vingine vilitolewa kwa hoja hii ilihali biblia bado ina vitabu vyenye kasoro zilezile? Mfano mingine ni waebrania, Wimbo ulio bora vyote vina utata wa uandishi na mikono zaidi ya miwili imehusika kwa gap la miaka zaidi ya 100!! Je sababu ya kupunguza vitabu vingine kwa kisingizio hiki ni halali au kuna mengine tunafichwa?
 
MAANDIKO YENYE UTATA
Kuna mistari mingine ambayo ni halali kibiblia ila imebadilishwa maeneo husika ipo mistari zaidi ya 50 kwenye agano jipya mfano Yohanna 7:53-8:11 kuhusu Yesu kuwepo hekaluni ila ghafla kipande kati ya 7:52 na 8:11 vimechomeka story ya mwanamke kahaba alietaka kupigwa mawe na ghafla mstari wa 12 unaendelea Yesu akiwa hekaluni hii inakubaliwa na wanatheolojia wote kuwa kilichomekwa na hakikuwepo kwenye maandiko orijino kama una biblia hapo kasome hiki kipande alafu utaelewa nachosema. Kanisa likaamua kuita vitabu vyenye maandiko na uandishi wa utata kuwa ni disputed books ilihali zina sifa zile zile za kuitwa pseudepigraphi na kutakiwa kufutwa kwenye biblia. Mfano Marko 16 inaishia mstari wa 8 ila 9-20 haikuwepo bali iliongezwa miaka mingi mbele na mtu asiyetambulika ila bado kipo kwenye biblia lakini kitabu cha Enoch au Yuda iskariot vimetolewa kwa hoja hiyo hiyo?? Kuna ajenda gani hapa wakuu?? Kipi tunafichwa?? Anyway disputed books kulingana na mwanatheolojia E. P. Sanders ni waefeso,wakolosai,2 wathesalonike, 1 & 2, Tito na vingine vingi.... Je kama vina kasoro kwanini vimeachwa??

VILIANDIKWA NA MUNGU?
Kuna hoja inasema vitabu vya Biblia viliandikwa kwa uweza wa Roho mtakatifu hivyo vile vilivyoachwa havikuandikwa na Roho mtakatifu sasa tujiulize GT kama kuna mistari ya Biblia imeongezwa na wanadamu mfano isaya,wimbo ulio bora,Tito,Yeremia,marko je bado hoja hii ina mashiko ilihali wanatheolojia wanakiri biblia ilichezewa kwa mifano niliyotoa hapo juu na kama si kweli viliandikwa kwa uweza wa Roho bali fahamu za wanadamu je kwanini basi ilitumika kuzuia vitabu kama Injili ya Yuda ama Thomaso?? Je hakuna agenda ya siri kwanini vilizuiwa alafu sisi tukaaminishwa tu kuwa havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu??
21vvVunMh+L.jpg

PSEUDEPIGRAPHI ZINAKINZANA NA BIBLE
kuna hoja ilitolewa kwamba vitabu vya biblia vinakinzana na Pseudipigrapha ndio maana vikatolewa kwenye bible ila cha kujiuliza GT mbona kuna taarifa zinakinzana ndani ya biblia lakini havijatolewa??

MIFANO
Mathayo 4:1-11 inasema mara tu baada ya ubatizo Yesu alienda kufunga siku 40 ila Yohana 2:1 anasema siku tatu baada ya kubatizwa Yesu alikua kwenye harusi ya Cana!!

Au mathayo 27:44 wale wezi wawili walimtukana Yesu ila luka 23:39 inasema mmoja alitukana mwingine alimtetea.

Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!

Hiyo ni mifano tu ila kuna mistari zaidi ya mamia inayopishana taarifa ila vimeachwa kwenye bible lakini pseudipigraphi zikipishana hata neno moja ndio wanajengea hoja kwamba ndio sababu havipo kwenye bible je sababu hii ilisababisha vitolewe ama kuna mengi tunafichwa?

HITIMISHO
Kwa kuhitimisha labda niseme tu kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha vitabu vingine kutolewa kwenye biblia na vingine kuachwa wakato vina kasoro zile zile..... Na hata mkuu Pendael24 alishawahi kuhoji kwamba kama tunafikiri biblia imechezewa je Mungu haoni hadi aruhusu hilo?? Na akahoji mbona Biblia inatenda ina maana kazi ya forgery inaweza kuwa na nguvu za Mungu na akanihoji je wachungaji wote hawa wakubwa hawalijui hili kiasi Mungu awaache watumie bibloa iliyochakachuliwa?? Kiukweli nilikosa majibu ila nategemea leo humu majibu yote yatapatikana

NB: Mimi nimechokoza mada tu ili kupata maarifa ya GT ila sio msimamo wangu kuwa bible ni batili au Qur'an ndio sahihi hivyo tunapojadili hoja humu tuhakikishe tunazingatia hilo pia udini na kejeli na matusi sio uwanja wake humu, nataka tujadili kwa kujifunza sio kupambana.

Karibuni kwa mjadala
 
Biblia Hii Inayotumika Sasa Ina Contradictions Kibao Ambazo Zinaweza Kukupunguzia Imani Yako.

Kwa Ujumla Huwa Nasema Naamini Kuwa ' Yupo Muumba Wa Ulimwengu Na Vyote Vilivyomo ', Awe Ni Mungu Huyu Wa Kwenye Biblia: Sawa, Awe Ni Mwingine: Sawa. Haya Mambo Ya ' Dini ' Ni Pasua Kichwa tu

Kusema Biblia ni Kitabu Kitakatifu Si Sahihi Hata Kidogo. Ni Sawa Ile Katiba Pendekezwa Kutoka Bunge Maalumu!
 
Biblia inajitafsiri yenyewe

Biblia ni ufunuo wa simulizi ya ukombozi upatikanao kwa imani katika Kristo (tazama Luka 24:27, 44-47;
Yoh 5:39). Ingawaje, ufunuo wa Mungu ni jambo la kuendelea—i.e., unajifunua katika Biblia nzima. Kanuni kadhaa hutokana na kweli hii.

1. Maandiko kamwe hayawezi kujipinga.

a. Biblia nzima inakubaliana katika ujumla wake. Kwa hiyo sehemu mbili za maandiko zinazoonekana kupingana zinapochambuliwa vema hugundilika kwamba hazipingani. Sehemu moja ya maandiko inaweza kuboresha nyingine, au kuipa usahihi zaidi lakini haitaipinga.

b. Wakati mwingine kweli mbili au zaidi hufundishwa kwa uwazi katika Biblia, lakini hutokea kukinzana. Kwa mfano Ukuu wa Mungu na wajibu wa mwanadamu ni vigumu kupatana ingawa bado Biblia inafafanua hayo mawili. Katika hali kama hizo kumbuka kwamba Biblia ni mkusanyiko ya kweli za kiungu kwa akili za mwanadamu zenye mipaka.

“Wakati kweli mbili au zaidi zinafunazofundishwa kwa uwazi katika Biblia zinakinzana kumbuka kwamba unao ufahamu wenye mipaka. Usiyachukue mafundisho katika hali ya kuzidi kile ambacho Mungu hakusema ile kubaki kuwa sahihi katika ufahamu wako. Mwache Mungu asema alichosema bila kujaribu kumsahihisha au kumfafanua Mungu. Kumbuka yeye ni Mungu na wewe ni mtu. Nyenyekeza moyo wako kirahisi kwa imani na amini alichosema hata kama huwezi kuelewa au hakiendani na ufahamu wako vizuri”.

2. Hatua ya ukombozi kwa pamoja na “shauri zima la Mungu” (Matendo 20:27) ni lazima izingatiwe kwa utaratibu maalumu ili kuelewa kwa usahihi kifungu maalumu cha maneno. Biblia ni kitabu kinachoeleza simulizi moja inayoelezea habari inayokubaliana. Ingawa ukweli wote wa Biblia haujafunuliwa kwa wakati mmoja, lakini ulifunuliwa kwa mwendelezo kwa muda mrefu. AK ni maandalizi ya Injili;

Injili zote katika Agano jipya ni udhihirisho wa Injili; Matendo ya Mitume ni upanuzi wa Injili; Nyaraka ni ufafanuzi ya Injili; na Ufunuo ni matumizi ya Injili. Maana kamili ya kifungu chochote cha maneno haiwezi kueleweka vema kama haijazingatia Biblia nzima na hatua ya historia ya ukombozi. “Kusoma Biblia kwa kuzingatia mazingira halisi ya ujumbe kama Neno la Mungu ni lazima kuhusisha maandiko yote yaliyokubaliwa kama mazingira hitimisho ya kifungu husika cha maneno”
 
Back
Top Bottom