SoC01 Siri iliyopo nyuma ya Biashara ya 'kujiuza' - Athari na hatua za kuchukua

Stories of Change - 2021 Competition

MoseeYM

Senior Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
144
Reaction score
199
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africa sana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE

Homa ya Ini.

Wataalamu wa afya wanadai kuwa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi zaidi ya mmoja ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya Ugonjwa wa homa ya ini (Hasa kirusi B na C ),ambavyo huchangizwa na jasho au majimaji.Kwa hivyo 'wanaojiuza' na 'wanunuaji' wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.ikumbukwe kuwa njia ya kupata ugonjwa huu ni rahisi kuliko hata VVU ,kwani hata jasho huweza kuwa kisababishi.

UVICO-19

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Dunia imekuwa ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana kupitia semina na mafundisho mbalimbali yanayohusu vijana.
 
Upvote 23
Uchunguzi wangu wa hizi siku mbili tatu umeonesha kuwa maeneo ambako biashara hizi zimekuwa zikifanyika 'wahusika' wamepungua.
Inawezekana ni kutokana na hofu ya UVICO-19.
 
mkuu.
Unaweza kuwwka vielelezo vya kimaandiko namna walivyoikuta na kuiacha?
Ngj nijaribu kumsaidia swali anavyosema waliiacha inamaana toka enzi hzo hawaja na mbinu kuwasaidia hawa viumbe kuacha hiyo bizness. Ulichoandika ni kizuri Lakin kuisha haiwezekan kwn ndo kwnz inazidi kuota mapembe ila wakuimaliza hii biashara ni sisi wanaume na sio wengine...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu nimekuelew sana.

Kama nilivyosema hapo juu hii biashara imekuwa na madaraja.

kundi la wanaojiuza hadharani,inawezekana kabisa hatua madhubuti zikachukuliwa na ikapungua ama kuisha kwa sababu madhara yake ni makubwa.

Tofauti na wale ambao hawafanyi hadharani

Nakubaliana kabisa na wewe kuwa kubadilika kunaanzia kwa wanunuzi.
Ingawaje nafahamu ya kuwa wakupinga hii hoja ni wengi.
 
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africa sana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE

Homa ya Ini.

Wataalamu wa afya wanadai kuwa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi zaidi ya mmoja ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya Ugonjwa wa homa ya ini (Hasa kirusi B na C ),ambavyo huchangizwa na jasho au majimaji.Kwa hivyo 'wanaojiuza' na 'wanunuaji' wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.ikumbukwe kuwa njia ya kupata ugonjwa huu ni rahisi kuliko hata VVU ,kwani hata jasho huweza kuwa kisababishi.

UVICO-19

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Dunia imekuwa ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana.

Mpaka sasa dunia ingeweza kutatua ajira haya yote tokea kipindi cha maisha ya mwanadamu yasingekuwepo.
 
Sawa mkuu nimekuelew sana.

Kama nilivyosema hapo juu hii biashara imekuwa na madaraja.

kundi la wanaojiuza hadharani,inawezekana kabisa hatua madhubuti zikachukuliwa na ikapungua ama kuisha kwa sababu madhara yake ni makubwa.

Tofauti na wale ambao hawafanyi hadharani

Nakubaliana kabisa na wewe kuwa kubadilika kunaanzia kwa wanunuzi.
Ingawaje nafahamu ya kuwa wakupinga hii hoja ni wengi.
Wapingaji ni sis wanaume tunaonunua ila wanasema kwl hii biashara kuisha ni ngumu sana kwnza ni worldwide na pia hata watu wazito,vibopa wanasaidia isiishe imagine malaya wanakamatwa lakn unaskia wametolew na mtu fulani apo ndo ujue kuisha ni majaliwa maybe mpk Yesu arudi

Nimekuelewa sana mkuu.
Ahsante kwa mawazo mazuri.

Imani yangu ni kwamba tatizo lolote lililopo kwenye jamii ,lenye visababishi vinavyojulikana inawezekana kupambana nalo.Kuliko tatizo lenye visababishi visivyojulikana kirahisi.

Nadhani watu wa afya au hata mafundi wananielewa .Wanafahamu ugumu unaokuwepo pale tatizo lilalobidi kutatuliwa halitoki na sababu za tatizo hazieleweki.Lakini pia kwa upande mwingine wanaelewa urahisi wa kutoa suluhu ya tatizo ambalo sababu zinajulikana.
 
'Buletproofs' zinaweza zisiwe msaada kwenye magonjwa mengine kama Hepatisis B.

Kwenye 'Tasnia' huko kuna stori ipo binti alikutana na babaake.
Mahali popote pa KAZI, ajali kazini hazikosekani

haTa kwenye Ndoa watu wanaambukizana ukimwi.

haTa maabara madaktar wanaambukizwa ukimwi
 
Hahahaha ,

Ahsante kwa mchango wako mkuu.

Natamani nione hizo "bulletproof" unazozisema zikoje na watumiaji wanatumiaje .maana magonjwa kama Hepatisis B,huambukizwa hata kwa njia ya mgusano kupitia majimaji (Mfano Jasho nk).Sina hakika sana kama huko kwenye 'tasnia' migusano ya aina hiyo inayopelekea kuambukizana Hepatisis B haipo.

By the way ,nilishawahi kumpoteza rafiki yangu kutokana na huu ugonjwa .Ingawa sifahamu kama alikuwa na ni 'Mzee wa tasnia'.Hii ilinipelekea kuanza kufuatilia kuhusu huu ugonjwa

Takwimu za WHO 2019,zilionesha kuwa kuna watu milioni 296 duniani wanaishi na huu ugonjwa ,kundi la wenye VVU linatajwa kuwa miongoni mwa makundi ya wenye huu ugonjwa.Hatari iliyopo ni kwamba uelewa wa jamii kuhusu huuu ugonjwa bado ni mdogo,watu wanafariki kwa kansa ya ini kutokana na huu ugonjwa.Lakini pia dalili zake kwa waliopata maambukizi mapya huchukua muda mrefu mpk kuonekana.Ashukuriwe Mungu chanjo ya huu ugonjwa ipo,japo uelewa kwa jamii ni mdogo kuhusu huu ugonjwa.
 
Bila shaka inawezekana hata wanaoambukizana kwenye ndoa,wanautoa kwenye 'tasnia'

Kwa hio 'tasnia' imeleta magonjwa hata kwenye ndoa.
 
SERIKALI
tumeishauri tumeshindwa itujengee kasino ipate kodi eti wapimwe haitaki

Umelewa na umenyoa vuzi nawembe zooote para parakweli kondom hua hazifiki kwenye kingo

Ili ukimwi uishe inatakiwa kilamtanzania awe tajiri
 
Mkuu.
Sidhani kama kuhalalisha hiyo itakuwa sawa.

Yaani wajenge kipi bora? Kujenga kasino wakati kuna watu wanapoteza maisha kutokana na kukosa zahanati karibu..

Kujenga kasino na kuwasaidia wahusika kwa kuwapa mitaji au ajira kipi bora?.

Unaweza kunielewa vzr ,siku ukikutana na wahusika ukawauliza kama wanaEnjoy kufanya hiyo biashara.
 
Wakati unasema haiwezekani pesa zinazojenga madaraja yetu madawati zinakuwa zimekusanywa kutoka madanguroni, Norway, Canada huko nk...tuitengeneze kua fursa ajira kwamabinti ili wajipatie kipato halali nchi isonge nawao wasonge

Vip kuhusu kunyoa kipara kipara hukuona ulemstarii mzee
 
Hiyo statement sikuielewa.
Ndio maana sikuijibu
 
Wakati unasema haiwezekani pesa zinazojenga madaraja yetu madawati zinakuwa zimekusanywa kutoka madanguroni, Norway, Canada huko nk...tuitengeneze kua fursa ajira kwamabinti ili wajipatie kipato halali nchi isonge nawao wasonge

Vip kuhusu kunyoa kipara kipara hukuona ulemstarii mzee
Ukirejea kwenye Maada hapo juu.utagundua kuwa nimeelezea nchi zilizoamua kuhalalisha na impact yake imekuwaje.
Kama uliiona hiyo sehemu,utagundua kuwa kitu unachosema kwamba 'madanguro' yangejenga madaraja hakipo na hakiwezekani.Labda kama kuna ushahidi kuhusu hilo.

'Madanguro' sidhani kama inaweza kuwa fursa ya Ajira.ikumbukwe nimebainisha hapo juu yanayofanyika kwenye hayo madanguro' ,hii ina maana kwamba kuruhusu madanguro ni kuruhusu na hayo mambo yaendelee

Labda siku moja itokee nchi ikaruhusu madanguro,bangi ,dawa za kulevya nk.
Kwa vile imeonekana vinatumiwa na wengi.ili tuone itatusaidieje.

Hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa kuruhusu 'madanguro' au bangi au dawa za kulevya.
Niliyoyaandika kwenye maada ni uchunguzi nilioufanya kwa kipindi kirefu kwa kuona na kuhoji wahusika.Naelewa pande mtazamo wa pande zote mbili ukoje,kwa serikali na 'wahusika'.Unfortunately,hata tukihalalisha na kuweka sheria,sisi hatutokuwa wa kwanza kufanya hivyo.Kuna nchi kama Senegal na Uholanzi zilihalalisha zamani sana na kuwekea sheria.Lkn bado waliyoyatarajia hayakuwepo.
Nadhani ,ungesema kuwa nguvu kubwa iwekezwe kwenye malezi ya watoto .kwa sababu ya kizazi kilichopo 'kina shida' ingefaa zaidi.kuliko kuhalalisha 'starehe' maana ile 'haiwezi kuwa kazi'.
 
Hahahaha ,

Ahsante kwa mchango wako mkuu.

Natamani nione hizo "bulletproof" unazozisema zikoje na watumiaji wanatumiaje .maana magonjwa kama Hepatisis B,huambukizwa hata kwa njia ya mgusano kupitia majimaji (Mfano Jasho nk).Sina hakika sana kama huko kwenye 'tasnia' migusano ya aina hiyo inayopelekea kuambukizana Hepatisis B haipo.

By the way ,nilishawahi kumpoteza rafiki yangu kutokana na huu ugonjwa .Ingawa sifahamu kama alikuwa na ni 'Mzee wa tasnia'.Hii ilinipelekea kuanza kufuatilia kuhusu huu ugonjwa

Takwimu za WHO 2019,zilionesha kuwa kuna watu milioni 296 duniani wanaishi na huu ugonjwa ,kundi la wenye VVU linatajwa kuwa miongoni mwa makundi ya wenye huu ugonjwa.Hatari iliyopo ni kwamba uelewa wa jamii kuhusu huuu ugonjwa bado ni mdogo,watu wanafariki kwa kansa ya ini kutokana na huu ugonjwa.Lakini pia dalili zake kwa waliopata maambukizi mapya huchukua muda mrefu mpk kuonekana.Ashukuriwe Mungu chanjo ya huu ugonjwa ipo,japo uelewa kwa jamii ni mdogo kuhusu huu ugonjwa.
Ayo magonjwa ya kugusana ayakwepeki.
Ata KWENYE football au mwendokasi ikitokea unapata TU so lazima kwenye sex TU.
 
Ukirejea kwenye Maada hapo juu.utagundua kuwa nimeelezea nchi zilizoamua kuhalalisha na impact yake imekuwaje.
Kama uliiona hiyo sehemu,utagundua kuwa kitu unachosema kwamba 'madanguro' yangejenga madaraja hakipo na hakiwezekani.Labda kama kuna ushahidi kuhusu hilo.

'Madanguro' sidhani kama inaweza kuwa fursa ya Ajira.ikumbukwe nimebainisha hapo juu yanayofanyika kwenye hayo madanguro' ,hii ina maana kwamba kuruhusu madanguro ni kuruhusu na hayo mambo yaendelee

Labda siku moja itokee nchi ikaruhusu madanguro,bangi ,dawa za kulevya nk.
Kwa vile imeonekana vinatumiwa na wengi.ili tuone itatusaidieje.

Hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa kuruhusu 'madanguro' au bangi au dawa za kulevya.
Niliyoyaandika kwenye maada ni uchunguzi nilioufanya kwa kipindi kirefu kwa kuona na kuhoji wahusika.Naelewa pande mtazamo wa pande zote mbili ukoje,kwa serikali na 'wahusika'.Unfortunately,hata tukihalalisha na kuweka sheria,sisi hatutokuwa wa kwanza kufanya hivyo.Kuna nchi kama Senegal na Uholanzi zilihalalisha zamani sana na kuwekea sheria.Lkn bado waliyoyatarajia hayakuwepo.
Nadhani ,ungesema kuwa nguvu kubwa iwekezwe kwenye malezi ya watoto .kwa sababu ya kizazi kilichopo 'kina shida' ingefaa zaidi.kuliko kuhalalisha 'starehe' maana ile 'haiwezi kuwa kazi'.
Malenzi ya watoto tumeshashindwa mambo yabadilike na tu ukubali ukweli

Globalisation imetumaliza
 
Back
Top Bottom