Siri imefichuka ,kumbe staa wa filamu nchini na aliyekuwa miss tanzania 2006, wema isaac sepetu anadaiwa kuwa mke wa mtu, inasemekana staa huyo alifunga ndoa na mjasiriamali aitwaye yusuph jumbe mwezi wa pili mwaka 2009.
Hata hivyo inadaiwa ndoa hiyo haikufika hata mwezi wanandoa hao wakashindwana na bado haijajulikana kama waliachana kwa talaka au lah.
Staa huyo (wema) ambaye yupo kwenye mahaba niue na staa mwenzie diamond platnum, ambapo ivi karibuni wanadaiwa kutaka kufunga ndoa ambayo kwa mwanadada wema itakuwa ndoa yake ya pili.
Sasa haijajulikana kama dini yake inamruhusu kuolewa mara mbili kama ilivyo kwa wanaume wanavyoruhusiwa kuoa wake hadi wanne au lah.