Issue yake ni kukosa kuambiwa ukweli au mzigo wa responsibility wa kulea mapacha kabla wa kwake hawajaanza kuja au hataki kabisa kuwaona hao watoto?
Kuna ukweli kabisa wa watarajiwa kushindwa kuwa wakweli pale linapoingia suala la kuwa na watoto kabla ya ndoa. Kwa upande wa akina dada, wengine huwa na uoga kuwa je nikisema ndio utakuwa mwisho na huyu baba au vipi? Kwa upande wa akina baba, sina uhakika kama na wao wanakuwa na hisia hizi hizi au they just choose not to say...labda na wao watatusaidia mawazo. Ila kwa wawili watatu ninaowafahamu, they were proud of their watoto na kuwasemea point black! Hata hivyo, 'dhambi' si inakuja mdada akiwa na mtoto na siyo mkaka, so why the worry?
Cha msingi, nafikiri yanazungumzika..aongee vyema na huyo dada kujua sababu za yeye kutokuambiwa ukweli. Lakini mwisho wa siku uamuzi anao yeye mwenyewe, kama anaona hilo kwake yeye ni kosa kubwa ambao halina mjadala, basi asonge mbele! Kuliko baadaye ndio liwe la kukumbushia kila anapoudhiwa na huyo mwenzi wake.