Siri imefichuka Wachezaji wa Yanga Nahodha Cannavaro na Kessy wapigana wakigombea posho

Siri imefichuka Wachezaji wa Yanga Nahodha Cannavaro na Kessy wapigana wakigombea posho

Na bahati nzuri au mbaya hakuna mahala nimeandika kwamba unatakiwa uiamini na humu JF hatuna utaratibu wa kulazimishana tuamini ' mabandiko ' yetu. Kama una namba za Msemaji wa Yanga SC Dismass Ten tafadhali nakuomba umwambie mbona anachelewa kuikanusha au kuikubali hii taarifa? Tatizo nini?

Na mpaka kuelekea tarehe 28 October, 2017 katika ile Mzizima Derby au Dar es Salaam Derby au Ilala Derby au Tanzania's Derby au East and Central Africa Derby ya Simba na Yanga ' tutawateseni ' sana Kisaikolojia wana Yanga SC na kupelekea ' kuchanganyikiwa ' vibaya hatimaye kufungwa magoli mengi na Simba SC yangu. Kuanzia sasa hadi hiyo siku ni ' ' fitna ' tu kwa kwenda mbele. Kwa siku hizi zilizobaki wana Yanga SC ' mtanisamehe ' tu kwani nina ' Jukumu ' kubwa la kuwaharibuni ' Kisaikolojia ' hivyo Kipele kimempata Mkunaji.
Sawa tunasubiria habari kutoka vyanzo vya habari vyenye kuaminika 'vilivyotukuka' kwa kuwa wewe ni Simba huiombei Mazuri Yanga
 
Umeshasamehewa tayari baada ya kuomba radhi. Haya sasa tuendelee na suala letu la ' Kupigana ' kwa Nadir Haroub ' Cannavaro ' Nahodha wa Yanga SC na Beki Ramadhan Kessy ' wakigombea ' posho baada ya mechi yao ya Kirafiki na Rhino Rangers ya Tabora hivi karibuni. Yaani leo hii Wachezaji wa Timu ya Kimataifa wanafikia hatua ya ' Kudundana ' kwa ajili tu ya ' Posho ' ambayo nasikia ilikuwa wagawane Tsh 9,700/ kwa kila Mchezaji wa Yanga SC aliyekuwepo pale ila Cannavaro akataka awape Wenzake Tsh 3,200/ tu na zingine ' achikichie ' mfukoni. Vipi tumwombe Mo Dewji awasaidieni na atawadai kidogo kidogo / taratibu?
Kwangu huu ni udaku mkuu thibitisha kwanza huwa sijadili udaku bosi.Pia halisaidii ktk maendeleo ya Soka.
 
Habari ndiyo hiyo Mkuu na hakikisha unaichukua kama ilivyo kwani nimeileta kama nilivyopewa na sijaichuja kokote ila namsubiria tu Msemaji wao Yanga SC Dismass Ten aikanushe ili nimdhihirishie kwamba japo Mimi ni mwana Simba SC tena lia lia / kindakindaki lakini nazijua habari za ndani za Yanga pengine hata kuliko ninavyojua habari za ndani za Klabu yangu pendwa, bora na kipenzi cha Mwenyezi Mungu na Malaika wake wote Simba Sports Club.
Simba MNA KAZI kwel kwel
 
8028460605a8c45942a55252a52c13a4.jpg
Mara paap.. Kitu kitu, kakwepa, kuchukua, piga, chalii

Posho yaleta mtifuano TBR.
 
Kumbe mkuu upo kishabiki zaidi badala ya ukweli wa mambo, ndiyo kusema unavizia nafasi ya kuwa msemaji wa klabu ya simba kuchukua nafasi ya Manara, anayetakiwa kuachia nafasi kutokana maiki atumiazo kuwa na madini ambayo ni hatari kwa watu wenye vimelea vya albinos. Athari zake ni kuzeeka haraka, kuwa chizi, kukojoa wakati wote na kupoteza kumbukumbu. Nawakilisha
 
Umevurugwa wewe umeamua kupoozea kwetu.Ha!ha! pambana na hali yenu Sumba.
 
Mkuu, hukuweza kunusa habari za Mayanja kuwa replaced na Mrundi utaweza kujua habari za Yanga?
By the way, hujanusa kutimuliwa kwa Omog?
 
Wewe jamaa mbona mbeya mbeya ?

Hangaikeni kuitafutia Simbwa ubingwa huu ni mwaka wa tano mtatoka kapa.
 
Hakuna kiumbe muongo Duniani kama mleta mada, alitabili lisu kisha fariki kitambo ila majuzi tumeona picha za lisu.


Huyu mpuuzeni ni Vuvuzela
 
Habari iliyonifikia hivi punde kutoka katika chanzo changu kikubwa kabisa na ninachokiamini ndani ya Klabu ya Yanga kimenitaarifu kwamba kuna taarifa ambayo Wadau wa Michezo tunafichwa ila ukweli ni kwamba baada ya mechi ya Kirafiki ya juzi ya Yanga SC na Rhino FC katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mkoani Tabora kulitokea ' Ngumi ' baina ya Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ' Cannavaro ' na Beki wa Kulia Ramadhan Kessy.

Sababu Kuu iliyopelekea kuwa na mpambano huo wa Ndondi usio rasmi na usio na mkanda ni pale ambapo Nahodha Cannavaro alipoamua kugawa ' Posho ' kwa Wenzie kwa kadri alivyokuwa akipanga Yeye hali ambayo iliondoa uvumilivu wa Beki Kessy ambaye aliamka na kutaka ajue kimepatikana Kiasi gani ndipo baada ya kutopata maelezo ya kutosha kutoka kwa Nahodha wake akaamua kumnyang'anya zile Hela ndipo Nahodha Cannavaro alipoamua nae kujibu mapigo wakapelekea ' Kudundana '.

Mara baada ya kutokea ' tafrani ' hiyo Viongozi wa Yanga FC na ' Benchi ' zima la Ufundi liliamua kulifanya hili Siri kubwa ili Mwandishi wa Habari yoyote asiijue lakini kumbe hapo hapo wakasahau kwamba GENTAMYCINE popote pale nina ' Vyanzo ' vyangu ambavyo huwa havinifichi kitu na hatimaye leo ' nimepenyezewa ' hii.

Aidha chanzo changu hicho Kikubwa kilichopo ndani ya Klabu ya Yanga kimeniambia kwamba kwa sasa hali ya Kiuchumi / Kipesa ndani ya Timu ni mbaya sana na kwamba Wachezaji wamekosa ' morale ' na wamesikitishwa mno na taarifa wanazozisikia kutoka katika Vyombo vya Habari mbalimbali kwamba aliyekuwa Mfadhili wao Manji amerudi wakati siyo kweli na kwamba Uendeshaji wote wa Timu kwa sasa unatokana na Timu Kukopa Pesa kutoka kwa Makampuni na watakatana taratibu na kwamba si kweli kwamba Yusuph Manji amerudi Yanga rasmi.

Haya sasa nimeleta hii taarifa huku nikimsubiri kwa hamu sana Msemaji wa Yanga FC Dismass Ten aikanushe kisha niweke ' hadharani ' bomu lingine ambalo linakaribia kupasuka ndani ya Yanga na ambalo naamini Wanachama wake wakilisikia sasa hivi hapo Kaunda Jangwani ' bakora ' zitaanza kutembea na ' Kitanuka '. Hakuna kinachoendelea au kitakachoendelea ndani ya Yanga GENTAMYCINE nisijue au nisikipate hivyo wana Yanga SC popote pale mlipo acheni kuwa na viherere na kuwashwawashwa mno na masuala ya Simba SC wakati nyie ya kwenu ni mengi na yanawashindeni.

Nawasilisha.

Ulituaminisha kuwa rufaa ya simba imetua FIFA na hili pia huaminiki
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Yaan Yule kessy aliyekimbia simba ndio kaenda kugombea hela huko
 
Ww ndio uliabdika jengo la yanga litapigwa mnada ndan ya mwez mmoja
 
Back
Top Bottom