Siri: Kama hutaki kutumbuliwa fanya haya

Siri: Kama hutaki kutumbuliwa fanya haya

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Hii ni siri nawaibia viongozi na watendaji wote mlioaminiwa na kupewa madaraka katika nyadhifa mbali mbali za Kitaifa, ukuu wa idara au mashirika, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Wakurugenzi n.k.

Kama ni miongoni mwa watajwa hapo juu zingatia haya machache ili uendelee kusalia katika nafasi au cheo chako vinginevyo utatumbuliwa kwahiyo usije kusema hukujua kabla kwa sababu siri nakupa.

1. Fanya kazi kwa kujiamini. Jambo la kwanza na muhimu ni kuishinda hofu ya kutumbuliwa kwa kufanya kazi kwa kujiamini maana kujiamini ndio msingi wa mafanikio kwenye kila jambo.

2. Zingatia misingi ya kikatiba na sheria katika kufanya maamuzi. Ruhusu sheria ikuongoze kwenye kila hatua unazochukua katika uongozi wako. Kamwe usifanye maamuzi kwab utashi binafsi kinyume na katiba ya nchi kwa kuhisi maamuzi hayo yatamfurahisha mheshimiwa Rais, utatumbuliwa!!

3. Katika utendaji kazi wako ruhusu kazi ndio iongee zaidi sio maneno. Usiwe mropokaji kama mkuu wa mkoa wa mbeya (Albert Chalamila) kujifanya unajua sana kuisemea serikali wakati sio jukumu lako bali jikite kwenye eneo lako la kazi ili kuleta matokeo chanya katika majukumu uliyo kabidhiwa.

Pia epuka kuwa muongeaji kupita kiasi na kupenda kuonekana sana kwenye makamera kila wakati kama Suleiman Jafo bali fanya kazi yako kwa bidii na matokeo ya kazi hiyo ndio yatakufanya uonekane.

4. Ongoza kwa hekima na busara. Usitumie ubabe na kujifanya ngangari kama Cornel Magembe( Dc wa Ukerewe) bali ruhusu busara itawale katika maamuzi yako ili usiumize wananchi au watu unao waongoza.

Pia usifanya maamuzi kwa mihemko kama Jerry Muro (DC wa Arumeru) maana mihemko na busara ni vitu viwili ambavyo havitangamani.

5. Usijikweze. Kamwe usijikweze wala kuwadharau wa chini yako kama Asia Abdallah (DC wa Kilolo) bali fanya kazi yako kwa unyenyekevu na kuheshimu kila aliye chini yako.

6. Usifanye kazi kwa kusubiri tamko kutoka juu. Kama kuna jambo chini ya ofisi yako linaenda ndivyo sivyo, chukua hatua za haraka usingoje tamko la mheshimiwa Rais kama suleiman jaffo maana utaishia kutumbuliwa.

7. Kuwa mtenda haki, usionee watu. Umeaminiwa na kupewa madaraka hayo kuongoza watu hivyo kuwa mtiifu kwao, usiwaonee au kuwanyanyasa kama afanyavyo Ole Sabaya( DC wa Hai) maana mama yetu hapendi uonevu, ana penda haki bin haki.

8. Usifanye kazi kwa kuvizia ili uendane na serikali ya awamu ya sita bali fanya kazi kulingana na majukumu uliyo kabidhiwa. Kitendo chochote cha kufanya kazi kwa kuvizia kuendana na kasi ya mheshimiwa Rais kitakufukuzisha kazi bali wewe simamia utawala wa sheria na kuheshimu haki za unao waongoza.

9. Usifanye maamuzi kwa kukurupuka bali fanya maamuzi kwa kufuata sheria inavyosema. Kamwe usijichukulie maamuzi yako mkononi kama Kenan kihongosi (dc wa arusha) ya kujichukulia sheria mkononi na kuadhibu watu kwa fimbo, makofi au adhabu nyingine kinyume na sheria za nchi.

10. Epuka unafiki na kufanya kazi kwa kujipendekeza kama kigwangala kwa kuwa hulka ya mama hapendi kusifiwa bali anataka kuona majukumu aliyokupa unayafanya kama inavyostahili ili kutatua kero za wanachi.

Mwenye masikio asikie, asiye na masikio aone na ashuhudie.
 
Umekuwa na usawa na haki katika ushauri wako.
Hongera sana.
[emoji1490][emoji1490][emoji1490]
 
Pia leta na siri ili upate teuzi ufanye nini
 
Poapoa ngoja niwaforwadie mawaziri wenzangu. Nitaanza na Waziri Junior.
 
Back
Top Bottom