Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Binafsi sijaona sababu ya msingi wa wazungu kudanganya kuwa dunia ni tufe na sio tambarare ukizingatia uongo huu ili ufanikiwe unahitaji ushirikiano mkuu wa mataifa yasiopendana ikiwemo Marekani, Russia, China, India, nchi za uarabuni na europeans.

Pia wanaosema dunia ni tufe wanakupa namba kwa kila kitu cha muhimu ukiuliza, duara lina radius = approx 6.3 KM, gravity = approx 9.8 m/s2.
Tunaweza kujua kutoka Dar hadi Mbeya kuna umbali gani kwa sababu kwenye ramani ya dunia tufe kuna scale, lakini ramani ya dunia tambarare haina scale, huwezi kunavigate kwa kutumia hiyo ramani.
Ukiniuliza kati ya hawa wawili nani anania mbaya, nitasema anayesema dunia ni sahani, sababu hawezi kunipa namba yoyote inayoweza nisaidia mimi kufika sehemu au kufanya kitu chochote.

Ukiacha haya bado kuna Solar na Lunar eclipse, haya unasema Mwezi na Jua vina size sawa, haya kwanini kuna total eclipse na the ring of fire? Pia lunar eclipse inatokea je? Kwanini mwezi ghafla uanze kupoteza nuru yake?
Pia pia kama vina size sawa na kuna kipindi vipo eneo moja ilikutengeneza eclipse kwa nini havijawahi kugongana au Jua kulichoma sana mwezi kwa sababu lipo karibu na Mwezi, mimi ni mbali nalo linanichoma haswa sasa huo mwezi wenye size sawa na jua unapona je kwenye eclipse. (Kumbuka vitu kinaonekana kidogo zaidi jinsi kilinavyozidi kuwa mbali)

Haya tuassume dunia ndo centre ya universe, jua mwezi na kila kitu kinazunguka dunia kwa sababu ambazo hazijulikani, haya kwanini sayari kama Jupiter zina mwezi zaidi ya mmoja, kwa nini miezi yake inazunguka Jupiter na sio dunia???
 
Tuachane na Motive ya kudanya dunia ni duara kwasababu HAMJUI

Turejee sasa ni nani waliobaini dunia ni duara? na ni wakati gani walibaini? Na kwanini walibaini?

Kabla hatujaja kwa NASA
Kwani nani mwenye exclusive right ya kubaini umbo la Dunia?
 
Tuachane na Motive ya kudanya dunia ni duara kwasababu HAMJUI

Turejee sasa ni nani waliobaini dunia ni duara? na ni wakati gani walibaini? Na kwanini walibaini?

Kabla hatujaja kwa NASA
Unapokesea ni kungoja wengine wabaini kisha ndiyo msingi wa hoja yako isimamie hapo.

Hata wewe una akili ya kutosha kubaini umbo la Dunia na whether ina move/not........usikariri kwamba kuna watu specifically wana mandate ya kutambua hivyo vitu.
 
Unapokesea ni kungoja wengine wabaini kisha ndiyo msingi wa hoja yako isimamie hapo.

Hata wewe una akili ya kutosha kubaini umbo la Dunia na whether ina move/not........usikariri kwamba kuna watu specifically wana mandate ya kutambua hivyo vitu.
Mkuu naamini ukiumwa unakwenda Hospitali..... kwanini?

Kwenye karne hii YES kuna watu wana MANDATE ya jambo flani kutokana na ujuzi wao na vifaa vya kitaalamu ambavyo vinazidi pale ukomo wa binadamu unapoishia

Ili kujua haya yote inakubidi uende nje ya dunia..... sasa kama wewe HUTAKI kuwatambua wenye uwezo wa kwenda huko unataka kujua haya kwa kutumia akili huku ukiwa umekaa kwenu masaki au ikwiriri hayo yatakua ni matatizo yako binafsi mkuu
 
Nje ya Dunia? ......Nje ya Dunia ni wapi?

Nani huyo aliyewahi kwenda nje ya Dunia?

Kwahiyo wewe umeamua usitumie akili yako kujua kuhusu masuala haya..?

Sisi wengine tumeamua kutumia akili zetu and that's why tunataka uthibitisho toka Kwa hao mliowapa mamlaka ya kufikiria kwa niaba.


NB:- Hata kwenda Hospitali sio njia pekee ya kuponya maradhi yako,..firstly mwili wenyewe una uwezo wa kujitibu na kupambana na maradhi lakini pia kuna njia na dawa mbalimbali za kujitibu hata usipoenda hospitali......SO EVERYTHING IS BOUND TO BE QUESTIONNABLE!
 
We’re not leaving at Ancient World Mkuu........ Tunaishi kwenye dunia ya SAYANSI na TEKNOLOJIA

Hatutumii akili tu tukiwa Kaseramimba kujua kuhusu the likes of solar system etc Tunatumia akili kwa kutumia high tech and go outer space to observe the whole shit whatever we can

NB:- Naona melezo meeengi bila majibu....... Nimeuliza tu ukiumwa huwa unaenda hospital na kwanini?
Ungejibu SIENDI πŸ˜‚
 
Mimi nashikilia hapa,

Una matatizo yako binafsi

Na hayo matatizo yako binafsi hayawezi kubadilisha ukweli, Unaishi kwenye Dunia tufe inayojizungusha yenyewe huku inazunguka Jua.
 
Nguvu Gani hizo?
Coil?πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unajichanganya Sana .. Hoja ya msingi ni kwamba Jua lina move.,...hizo nyingine ni hadithi tu ambazo huna uhakika nazo umeambiwa ukaamini.

Logically ukishasema Jua lina move hutakiwi tena kusema Jua lipo stationary!

Nadhani umeelewa sasa.
Kama tu ukiwa hujui term Reference frame sawa. Na siwezi kubishana naww kama hujui maana ya hicho kitu, nimeshakupa mifano mingi tu mfano upo kwenye basi wewe seat ya nyuma je dereva atakuwa anamove from where you're? Ukielewa hapa utanielewa ila shida yako unashindana.
 
hapa naomba nijaribu kulijibu swali lako kutokana na fikra na mawazo yangu.

Faida kubwa ya Muongo ni kutaka kuaminika...!! Sijui kama nimekujibu vizuri lakini.?
Upo sawa kabisa kulingana na fikra na mawazo yako.

Sasa usitake kuaminisha watu kuwa unachohisi ndo ukweli.
 
Point yako hapa ni nn kusema mvua inavyoshesha both side za Dunia at the same time?
 
Upo sawa kabisa kulingana na fikra na mawazo yako.

Sasa usitake kuaminisha watu kuwa unachohisi ndo ukweli.
Sasa mbona wewe unataka kuaminisha watu kwamba unachohisi Ndiyo kweli?

Yani unaamua tu kuaminisha watu kwamba Dunia ni Tufe na inazunguka,...bila uthibitisho wowote na unataka uaminike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…