Haya tuambie gravity inavuta kitu chenye mass kubwa na ndogo kwa acceleration ya ngapi mpaka vyote vinafika chini kwa pamoja?
Kumbuka umefundishwa kwamba,. Objects with larger mass are pulled with greater force by gravity compared to objects with smaller mass."
Formula ya F=ma => F=mg
Inachojaribu kusema ni kuwa ukiwa na vitu viwili sehemu moja
1) Utatumia force kubwa kwenye kunyanyua kitu kizito kuliko force utayoitumia kwenye kunyanyua kitu kidogo (a ni constant hapa 'g', so Force is directly proportional to Mass.)
2) Kama vyote vilianza safari ya kuanguka pamoja, utatumia nguvu kubwa kuzuia kitu kizito kuliko kile chepesi, yani kile kizito kitafika na force kubwa kuliko kile chepesi.
Formula ya F=G*MEarth*mass/r2
Pia inakupa story hiyo hiyo kwa vitu vyote ambavyo vipo karibu na dunia.
Ambapo G ni constant
MEarth => Uzito wa dunia ni mkubwa sana kuliko uzito wavitu vilivyopo duniani
r2 => Umbali kati ya centre ya dunia na object, radius ya dunia ni kubwa sana kuliko height ya kitu chochote kilichopo duniani.
Kwa lugha nyingine hiyo formula unaweza kuiarrange
F = mass*(G*MEarth/r2) = mass* (acceleration)
Kwa lugha nyepesi
Acceleration ya freefall = G*MEarth/r2
Gravitational constant G, na mass ya Earth haviwezi kubadilika, kitu pekee kinachoweza kubadilika hapo ni 'r'.
Kwa vitu vyote vilivyo karibu na dunia na ukubwa wake huwezi fananisha na ukubwa wa dunia, acceleration due to gravity ni constant, na kama vitaanza pamoja na vikawa na acceleration sawa basi vitafika pamoja.
Pia muhimu kujua kuwa force inayozungumziwa kwenye F=ma ni 'net force' kama kuna force nyingine yoyote ile hapo inahusika net force ni summation ya vector ya hizo forces husika.
Kila la kheri mkuu kwenye kubishana na uhalisia