Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Nadhani lengo la mtoa mada ni kuwachanganya wasomaji. Nawashangaa wanaoipongeza mada ingawa ni haki yao kutoa maoni yao. Bila shaka hawa ni wale bendera fuata upepo ambao hushabikia hoja halafu ikielemea mwingine nao hubadilika. Maelezo mengi tu ya kisayansi yanathibitika kwa uhalisia. Hata kama unamchukia mzungu, kama maarifa aliyokupa yanadhihirika usiyapinge kwa sababu ya chuki yako. Ni sawa na kukataa chakula na kula takataka. Maarifa yaliyopo duniani leo hii, ya yanayoonekana na ya yasiyoonekana, ya kweli na ya uongo, ni mengi sana. Na kila siku yale yasiyokuwa na majibu yanapata majibu kwa uvumbuzi. Mada hii imejaa upotoshaji wa kiwango cha juu sana ingawa sijui ni kwa lengo gani. Hata hivyo inafikirisha akili ingawa siyo ya kuiamini asilani.
 
We dapangi, unatumia bangi nini?
Mbona unapost zaidi ya mara 3 kitu hicho hicho
Mzizi wa id yako ni dabangi
 
Wewe uliyefuatilia hebu nipe mwanga wa hili, jamaa amesema dunia ni tambarare na maji yamezuiliwa kwa mabonge makubwa ya barafu. Swali, mwisho wa hayo mabonge ya barafu ni wapi na baada ya hayo mabonge kuna nini!
Hata Mi Nilijiuliza Hilo Nikashindwa. Na Kama Dunia Ni Flat, Jua Hupotelea Wapi? Tukubali Tu Kuwa Dunia Ni Round Kama Ilivyo Kwa Jua Na Mwezi. Kwa Nini Dunia Tu Iwe Flat?
 
Hata Mi Nilijiuliza Hilo Nikashindwa. Na Kama Dunia Ni Flat, Jua Hupotelea Wapi? Tukubali Tu Kuwa Dunia Ni Round Kama Ilivyo Kwa Jua Na Mwezi. Kwa Nini Dunia Tu Iwe Flat?
Mnakosa majibu ya maswali yenu kwasababu zifuatazo.

1. Kwanza hamjatulia katika kuufuatilia uzi huu kiasi cha kuuliza maswali ya Mkurupuko na kama bado hamjaliona jibu la swali hilo kwa maandishi, kwa picha na mpaka video, basi nyie ni vilazwa na hamstahili kujibiwa majibu yanayopatikana humu humu.

2. Pili mnapenda kutangulia kuelewa jambo msilolijua kabla yakuliona, na matokeo yake mnajukuta ni mashabiki ktk jambo lisilo na ushindani.

3. Tatu na lililo kuu ni kutokupenda kwenu kujifunza na hasa kwa njia ya kujisomea yale usiyoyajua.

4. Na hii itawahusu na wale wote wanaoendelea kuuliza maswali yenye majibu humu humu tena kwa lugha zote mbili ngeli na kiswahili. Hii ni dalili ya u much know, ukinbelembele, umbea na fitna za hapa na pale, coz hakuna aliyeitwa kuja kuusoma uzi huu... Na mtoa uzi hajataka kujua sisi tunaousoma tunaamini nini katika hili.

5. Woga, kiasi cha kugoma kuelewa, maana hata mkiambiwa tena na tena mpaka na ushahidi wa picha na video bado hamtasadiki coz mko kwnye ligi na hamtaki kushindwa na mshindani asiyeshindana.

Kwa wale tunaoufuatilia huu uzi naomba tusijaribu kujibu maswali yenye majibu.
 
Yaani dunia nzima na technologia zote zilizopo wangekubali kundanganywa na Nasa... Saiz mataifa kbao yana satellite zao angani na zinatuma picha ya dunia... Kwa ISS skuizi hata watu binafsi wenye hela zao wanafanya tour na kujionea kwa macho kutoka angani na kuona umbile la dunia sasa hao wanaosema dunia ni flat hawana hata uthibitisho wowote zaid ya theories.. Kazi sana...
 
NDUGI ZANGU ACHENI KUMCHUNGUZA MUNGU NAPENDA MTAMBUE KUWA MUNGU HACHUNGUZIKI.... NA NDIO MAANA HATA HAO WANASAYANSI KUNA MAMBO WANAYAFICHA NA KUWACHANGANYA WATU COZ KUNA VITU VINGI UKIVITAZAMA HUWEZI KUPATA MAJIBU MPAKA UNAKUFA. HAYA LEO MALA DUNIA DUARA, MARA TAMBALALE HIYO YOTE NI KUCHUNGUZA KAZI ZA MUNGU MLILETWA MJE KUISHI DUNIA HII YA TATU SASA HUKO MWEZINI SIJUI KWENYE JUA SIJUI MNAPIGA PICHA HAZITOKI MANATAFUTA NINI..... NA KAMWE HAMUWEZI KUUPATA UKWELI MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU YEYE NDIYE PEKEE ANAYEJUA ALIUUMBA VIPI ULIMWENGU WAKE.
 
Unafanya PHD ya hii kitu au??
 
Ukweli upo sehemu flani ngoja niutafiti na ipo siku nitapata tu data zake, huenda nikapata jibu lenye utofauti kabisa na madai ya kuwa dunia ni flat au dunia ni duara au nitapata jibu kati ya hayo mawili ama mjumuisho wa yote. Nikikamilisha utafiti nitaleta mrejesho. MOLA KWANZA.
 
Binafsi naishia kuwashangaa tu....

Jambo hili linapaswa lifuatiliwe na watu ambao siyo wavivu kabisa wa kusoma,hawa wanaokuja kuuliza maswali ambayo majibu yake yapo humuhumu kwenye huu uzi ni dalili ya masai kuingia disco.....

Unatakaje kujua jambo kama hili halafu uzi wenye kurasa 20 tu unakushinda kusoma?

NBadhani hawa ni wa kupuuzwa tu kama ulivyoshauri mkuu....
 
Hivi na wewe wakiitwa wanasayansi utaenda?wanaojiita wanasayansi wanaelezea vitu ambavyo vipo na vimeumbwa na aliyeumba,hivi kwamfano kwenye mwezi kuna maji sasa wao ndio wameyaumba hayo maji au?Wanachokifanya ni kudadisi na kugundua kwamba kuna vitu fulani ambavyo vipo tu yaani hata kama wasingegundua hivyo vitu bado vingeendelea kuwepo.Mfano maji ni mchanganyiko wa haidrojeni na oksijeni sasa kwenye jambo kama hili wanasayansi wamefanya kitu gani cha ajabu?
 
Tatizo ni kwamba majibu yenu yaliyomo humu yanazua maswali zaidi ya yaliyopo na hayo majibu mnayotoa hayajitoshelezi kisayansi ndo maana kila anaekuja anakuja na maswali zaidi.. Kuna website moja ya hao flat earth believers kwenye forum yake kuna uzi kama huu na maelezo yote mliyoyatoa humu ila kuna watu wamekuja na maswali ya kisayansi hamna majibu yamebaki mabishano.. Kwa mfano mtu akauliza kuthibitisha dhana yenu kama wanasayansi wengine wanadanganya kwa nini nyinyi msiunde chombo chenu mkakituma na mtu mnayemuamini aeende outer space afu mtupe hizo picha zenu halisi zinazoonyesha flat Earth hamna alietoa jibu zaidi ya kubisha kuwa hakuna wa kumuamini.. Watu wanachotaka ni uthibitisho.. Tumeni chombo chenu wekeni live tangu kinaondoka duniani mpka kifike anga la juu then kipige picha ya dunia then mtuonyeshe mmebaki mnalalamika nasa waongo.
 
Wewe kweli umeenda shule? , nakuwa na wasiwasi na wewe ujuwi kwenye floor ya bahari Kuna milima, mabonde, miinuko na mitelemko.
Kuna watu tambarare iliyozugumzwa hawaielewi.
Aha ha ha ha aisee huyo jamaa kweli hajitambui, eti zanzibar tungeiona walau kwa taa zake.

Nililipenda jibu lako la kwanzo kumwambia kuwa macho ya mwanadamu ya kikomo ktk kuona.
 
Hapa ndo kwa pamoja tuamini kuwa dunia ni flat.
 
Ni lini wanaoamini dunia ni flat watatuma vyombo vyao kwenda outer space na kutuonyesha umbile halisa la dunia kutoka kwenye vyombo vyao wanavyoviamni ili na sisi tuone..?
 
Hivi ukichukua taa ukiiweka juu ya kitu flat right on top of it kwa proportion ya distance ya jua na dunia si inamulika kitu kizima.. So inamaana pia tunadanganywa kua wakati nchi nyingine mchana kwengine ni usiku.. Kama dunia ni flat ilibidi jua linapokuwa katikati ya dunia basi dunia nzima iwe ni mchana na likishaondoka (sjui linaendaga wapi) kuna mda ilibidi dunia nzima iwe ni usku...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…