Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710

Kikundi gani hicho kilichosema binadamu anatokana na nyani? Weka jina usiongee bila kuwa na facts. Hakuna mwana science anaesema binadamu alitokana na nyani na hakuna mwana science anaesema dunia ni flat hayo yote mnayosema nyie ni conspiracy theories sio facts. Dunia kuwa duara anajulikana tangia enzi za zamani sio jambo jipya. Wewe sema hicho kikundi chako kilianzishwa mwaka gani?
 
-Majibu yangewezakana kabisa kuwepo lakini nisingependa tufike huko sababu tutaondoa kabisa lengo la hii Thread.

-Hongera zako wewe ambaye hukufunindishwa mwanadamu asili yake ni nyani na katika mitihani haukujibu hivyo ili usonge mbele.

-Sidhani kama kile kifaa cha Carbon 14 kilitengenezwa na mwanahistoria na sio mwanasayansi.

Yote kwa yote Mkuu naomba yaishe.

-Acha tujikite hapahapa dunia kuwa tambarare.
 
Mtoa mada elewa kuwa Quruan ilikuja miaka 600 baada ya Bible. Hata hivyo Galilei Galilaya alishatoa theory yake kuwa dunia ni duara miaka mingi nyuma.
 
Kama dunia ingalikuwa tanbarare basi ingalikuwa na mwanzo na mwisho. Hebu kwa mfano kodi ndege kubwa yenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefo kisha ondoka nayo Dar es Salaam elekea kaskazini au kusini bila kusimama wala kupinda uone kama hujarudi tena Dar. Au elekea magharibi au mashariki kisha uone kama hukurudi palepale. Lakini pia hali utakayo kutana nayo kwa safari ya kwanza ni tufauti kabisa na hali utakayo kutana nayo kwa safari ya pili. Kujiridhisha na ukweli kuwa dunia ni duara ni pale unaposafiri kwa ndega inayoruka usawa wa juu (ft 40,000au zaidi) kutoka usawa wa bahari uwe kwenye skyless weather ukichungulia dirishani utaona uduara wa dunia japo kwa mpindo mdogo. Lakini vilevile nenda ufukweni mwa bahari angalia kwa makini utaona uduara wa dunia.

Hii flatearth society ni kikundi kama kilivyo Illuminati au Freemason. Waweza kuta kimeanzishwa na wamarekani wanao amini katika nwo (new world order) anbao kazi yao ni kupinga kila ambacho hakikuanzishwa na wamarekani. Wao wana naono yao kuwa "Kilicho bora ni kile kilichotengenezwa Marekani". Hii inahusisha mpaka kwenye imani za dini. (dini bora ni ile iliyoanzishwa marekani).
 
Sasa mbon hakuna safari za ndege kati ya moscow urusi na jberg south africa ya moja kwa moja bila kupitia nchi nyingine za afrika na ulya. It means ukiwa south afrika na ukaelekea upande wa kusini tuu basi baada ya bra la barafu utakutan na urusi na ni karibu zaidi. Pa fuatilia njia walizopita watu waliyoizunguka dunia kwa ndege, mbona wnatumia northpole zaidi kuliko southpole
 
Na hapo ndo unapozidi kuingia chaka... Ndege sio basi mkuu ndo maana ukifatilia ramani ya ruti za ndege hazijanyooka kutoka kituo kimoja hadi kingine ila zinanyooka kutoka waypoint moja hadi nyingine.. Sababu ni kuwa kuna mambo mengi ya kuangalia mpaka ruti iwe official haswa hali ya hewa.. Kuna baadhi ya maeneo hutaona ruti za ndege za abiria sababu ya hali ya hewa isiyotabirika ila haimaanishi hakuna ndege inayopita kabisa..zipo ndege zinapita hayo maeneo..
Huko southpole kuna mpaka Airport za kwenye barafu kwa ajili ya ndege za watafiti mbalimbali au wanajeshi..fuatilia
 
Naona sasa uwezekano wakututoa kwenye elimu na kutuingiza shimoni..

Kuna theories nyingi mno za kujibu...
Ki utafiti..
 
Sasa usibishe kuwa kuna uwezekano wakudanganywa, haya hizo za jesi na za watafiti huwa zina uwezo wakutabiri hali ya hewa au wanatumia sababu hizo ili kificha ukweli.... Ina maana kaweza kwenda anga za mbali na anaplan yakupeleka na abiria ila kuwavusha antaktika ni issue?
 
Nimecheka sana watu tunapata shida sana bila ya kujua kuna upeo(horizons)huu ni mwisho wa ukomo wa jicho la mwanadamu lililoumbwa kuwa ROUND ,so chochote kile kinachotumia kuonea mbali kama camera nayo lazima KUTENGENEZA kwa mfano wa jicho,sasa huwezi kusema Dunia ni DUARA wakati jicho ni DUARA pia.(usikurupuke km hujanielewa kaa kimya)
 
Kitabu chako cha Dini kimeandika Uwongo ,hangaika uhangaikavyo lakini ukweli utabaki palepale , Huu ubichi ulikuwepo zamani sana sio sasa hivi kila kitu kinaonekana .Na hivyo vitabu ulivyo vitumia vyote vya wazungu waliandika kabla yakujua ukweli ,wewe leo hii ndiyo unaamka usingizini unataka ubishane kwa hoja za miaka elfu iliyopita.
 
hahaha hahahah nacheka kwa kidhungu
 
Ukilewa Sayansi utadanganywa na binadamu wenzako na kufanywa kama ndondocha kwa kuamini vitu ambavyo unapandikizwa bila kutumia akili yako, ukitumia akili za binadamu wa kawaida kutafakari utagundua kuwa dini iko sahihi kabisa kuhusu Dunia yetu.
 
Ukilewa Sayansi utadanganywa na binadamu wenzako na kufanywa kama ndondocha kwa kuamini vitu ambavyo unapandikizwa bila kutumia akili yako, ukitumia akili za binadamu wa kawaida kutafakari utagundua kuwa dini iko sahihi kabisa kuhusu Dunia yetu.
Non sense
 
 
Jina "Boko Haram" linatokana na lugha ya Kihausa likimaanisha "vitabu ni
haramu " yaani "elimu ya kimagharibi ni haramu au dhambi".
Mleta huu uzi naona wewe ni Boko Haram. halafu unatumia elimu hiyo hiyo ya magharibi kukosoa elimu ya magharibi. wenzako hizo hoja walizitumia mwaka 1600 wakati vifaa vya kisayansi hawana leo hii wana kila kitu, wanaona Dunia yote unaenda kuwabisha kwa hoja zao walizotupa. Lazima ukubali qurani ilikosea dunia sio flat
 
umejitaidi kupunguza bando lako kwa kuchukua mijadara ambayo wanajua wanacho taka kupotosha uma ili wapige pesa.au na wewe ushakuwa UFO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…