The celebrity
JF-Expert Member
- Jul 9, 2020
- 1,972
- 559
Kabla sijakujibu, wewe unahoja Gani kuhusu umbo la Dunia? Maana mwanzo umekuja na hoja kuwa ni tambarare lakini umeshindwa kuitolea maelezo.Yap kama ulivyosema kuna vitu vinanichanganya, ,....Kwa mfano elezea how Maji yanastick kwenye Tufe π linalozunguka.
Najua utakuja na kuingizia hoja ya gravity(ambayo probably umeikariri lakini huwezi ukaprove uwepo wake kwenye uhalisia),...
So, Apart from kile ulichofundishwa including gravity, unaweza kuelezea how Maji yanastick kwenye Tufe.?
Then, Justify kwanini Alaska na maeneo mengine yana experience midnight sun Kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili,... Kwenye model ya Dunia Tufe lnayolizunguka Jua kwa mwendo 107,000 kilometers per hour.
Nasubiri kujifunza toka kwako Mkuu,.
Kuhusu gravity, unataka niprove vipi katika uhalisia? Ni sawa naww nikuulize unaweza kuprove uwepo wa electrons, lakini application yake unaiona hata kwenye umeme unawaka lakini huwezi kunionyesha hizo electrons sivyo?
Lakini pia gravity ina-apply sehemu mbalimbali kama vile kwenye geophysical survey( identify rock type and water and mine exploration) pia kwenye trajectory hata kurusha nuclear bombs.
Kuhusu maji kustick kwenye tufe linalozunguka ni lazima nitumie uwepo wa gravity Kwa sababu ndio kitu kimojawapo (sa sijajua kwanini unataka nisitumie uhalisia uliopo maybe tuanze na mada ya gravity kwanza).
Unachotakiwa ujue gravity ina-act towards the centre of the earth kwahy maji yanastick hapo. kuhusu Dunia kuspin na maji yanaendelea kustick kumbuka rotation inatokea kwenye whole earth including atmosphere yake kwahy hata maji nayo yanaspin Kwa speed Ile Ile, mfano chukulia upo kwenye gari alafu rusha kitu juu kitarudi pale pale ulipo, kwann kisirudi nyuma? Nadhani mpaka hapo utakuwa umepata kitu kama Kuna mahali Bado panashida sema.
2.Pembe ya mhimili wa dunia ina pembe ya takriban 23.5β kutoka kwenye obiti yake - hiyo ina maana katika hatua moja ya mwaka ncha ya Kaskazini (yaani, ambapo mhimili wa mzunguko unakutana na uso wa sayari katika ulimwengu wa Kaskazini) umeelekezwa kuelekea Jua, na kisha. mwishoni mwa mwaka Ncha ya Kusini imeelekezwa kwenye Jua.
Maana yake ni kwamba kwa muda katika mwaka kuna eneo la sayari (yaani kati ya nguzo na latitudo 66.5β) ambapo jua huwa juu ya upeo wa macho kila mara, na vile vile kuna kipindi katika mwaka ambapo jua kamwe usije juu ya upeo wa macho. Vile vile hufanyika kwenye nguzo nyingine - lakini kwa nyakati tofauti za mwaka. Pete hii inayozunguka nguzo hadi latitudo 66.5β ni mduara wa Aktiki au Antaktika (kulingana na nguzo gani unayozingatia). Kwa hivyo katika mduara wa Aktiki kwa karibu miezi mitatu karibu na Majira ya joto ya Kaskazini (Juni 21) jua halitawahi kutua, na kwa kipindi hicho hicho katika mzunguko wa Antarctic jua halitawahi kuchomoza.
Tena kama utafatilia Kwa makini kuhusu hii midnight sun utaona nayo ni Moja ya proof ya kuwa Dunia ni tufe.