Siri ya 4th July na vifo vya waasisi wa taifa la Marekani

Siri ya 4th July na vifo vya waasisi wa taifa la Marekani

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za jioni wanajukwaa bila kupoteza muda niende kwenye mada kama kichwa cha uzi kinavyosema
1931-stock-image-by-stompstock.jpg

Kwa ufupi taifa la marekani lilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa kiingereza Julai 4,1776, ila tarehe hii ilinishangaza sana kutokana na mtiririko wa matukio ya waasisi wa taifa hili ambao walifanikiwa kushika urais tukiachana na George washington ambaye ndio alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo, na marais hao ni kama ifuatavyo

1.JOHN ADAMS
john-adams_editedjpg.jpg

Huyu alikuwa rais wa 2 wa Marekani na alitawala kati ya mwaka March 4, 1797 hadi March 4, 1801 na kufariki July 4, 1826 ambayo ndio ilikuwa maazimisho ya miaka 50 ya kutangazwa uhuru wa nchi ya marekani na alifariki kwa tatizo la moyo.

2.THOMAS JEFFERSON
thomas-jefferson_editedjpg.jpg

Huyu alikuwa Rais wa 3 wa marekani na alitawala kuanzia March 4, 1801
March 4, 1809 na kufariki July 4, 1826 siku ambayo pia ilikuwa yakuadhimisha miaka 50 ya uhuru ikimaanisha hawa wawili yaani adams na jefferson walifariki siku moja tena kwa homa za muda mrefu tu!!

3.JAMES MONROE
James_Monroe_White_House_portrait_1819.gif

Huyu alikuwa Rais wa 5 wa marekani na alitawala kuanzia March 4, 1817-March 4, 1825 na kufariki July 4, 1831 nyumbani kwa binti yake huko New york tena kwa maradhi ya kawaida tu!!

4.JAMES MADISON
james-madison_editedjpg.jpg

Huyu alikuwa Rais wa 4 wa marekani na alitawala kati ya March 4, 1809 hadi
March 4, 1817, tofauti na hao wa hapo juu Madison akiwa amebakiza siku 6 tu ili afikie 4th july ili akamilishe seti kama wenzake waliomtangulia alikuwa na changamoto ya kiafya iliyopelekea awe na matatizo ya kiakili na akiwa amezidiwa sana alipewa dawa ya kumsaidia kumsogeza masiku ila alikataa kunywa ndipo alifariki june 28 1836 ila inaonekana nia yao ilikuwa afike pia tarehe 4 kama wenzake.

Baada ya kusoma ulinganifu huu nimeona nilete mada hii kwa Great thinkers mnisaidie je vifo vya waasisi wa taifa hili yaani 3 kati ya 5 kufa tarehe 4 july na 1 siku chache kabla, je ni kwa bahati mbaya tu au kuna siri nyuma ya pazia?? Na je ni kwanni huyu madison aligoma kunywa dawa za kumsogeza hadi tarehe 4?? Je kuna conspirancy nyuma ya vifo hivi kuangukia tarehe ya kuadhimisha uhuru wa marekani??

Naomba kuwasilisha

NB Moderator JamiiForums Mod Two Reserved Invisible nawashukuru sana kwa kumoderate uzi mapema

Karibuni wanajukwaa wote
 
conspiracy theories...
kuna hii nayo

By remarkable coincidence, Jefferson and Adams died on the same day, Independence Day in 1826, the 50th anniversary of the adoption of the Declaration of Independence. Adams’ last words were, “Thomas Jefferson still survives,” though his old friend and political adversary had died a few hours before.
 
Nakumbuka kuna kipindi walimtabiria Obama atakufa lakini anadunda mpaka kustafu
Hivi majuzi tu kuna Prophecy mmoja wa kimarekani ambaye inasemekana tangu,atabiri urais wa marais USA hajawah kushindwa

Kama mwaka m1 alikuja Na kusema trump atafukuzwa lakin mpaka Leo trump ana dunda tu.
 
Asante chief,

ni kweli vifo vya hao viongozi wa marekani vilikua na utata utata sana,

Ila kwenye historia ya rais wa pili na watatu ndio inanichanganya kabisa,

John Adams ambae ndio alikua raisi wa pili alizaliwa October 30, 1735, na kufariki July 4, 1826.

Historia inasema huyu alimshinda THOMAS JEFFERSON ktk kinyang'anyilo cha kiti cha uraisi ambapo Thomas alikuja kuwa makamu wake,

tukija kwa Thomas Jefferson yeye alizaliwa April 13, 1743 na kufariki July 4, 1826 tarehe na mwaka sawa na ule aliokufa John Adams, hawa wawili ndio wananipa mshangao...japo wote walikufa wakiwa nje ya kiti cha uraisi,

ambapo unaweza kuona John Adams alimzidi Thomas Jefferson kwa miaka 8 kiUmri,

Ngoja tusubiri wajuzi waje watufungue...
 
Vilevile wote wawili Adams and Thomas Jefferson, are the only signers of the Declaration of Independence
 
Vilevile wote wawili Adams and Thomas Jefferson, are the only signers of the Declaration of Independence
hawa jamaa walikua na vitu vya tofauti kama yale ya Abraham, na taifa la marekani halipendagi kuona kiongozi anakuwa na misimamo yake ya pekee ambayo inakinzana na utaratibu wao.
 
July 4= 7 +4=11,Sept 11=9+1+1=11,,,angalia kifo cha kanumba jumlisha ni 11,Angalia tarehe akina JAY Z wanatoaga nyimbo zao jumlisha ni 11,tafuta na angalia matukio makubwa makubwa duniani jumlisha siku na mwezi utapatA 11.hii ni namba ya matukio ya hao akina..........
 
the past does not dertemine the future.....
How can u move forward if you don't know where u came from??? Hata hizi kompyuta au ndege walitumia past data,observation,experiments and research ili kuja na gadgets zote unazoziona hapa

Hata hizi theory za kiuchumi ilikuwa mmoja anasoma theory za mwanzo anazidevelop either kwa kukosoa ama kuongeza idea zake ndio leo tuna pesa,mabenki,cryptocurrency,forex etc

Kiufupi hakuna jipya chini ya jua hivyo tunahitaji taarifa za kale ili kusolve mystery za baadae!! Mfano kupitia vifo hivi tunaweza tukaprove kama ni kweli ama lah kuwa kuna watu wachache wanaweza kupanga matukio so in case mambo hayo yakijirudia watu hawawezi danganyika tena

That's how past determines the future
 
July 4= 7 +4=11,Sept 11=9+1+1=11,,,angalia kifo cha kanumba jumlisha ni 11,Angalia tarehe akina JAY Z wanatoaga nyimbo zao jumlisha ni 11,tafuta na angalia matukio makubwa makubwa duniani jumlisha siku na mwezi utapatA 11.hii ni namba ya matukio ya hao akina..........
kwenye tarehe na mwezi utapata 11 nyingi sana pengine 10 kati ya 12 kuna siku itatengeneza 11 uwezekano wa mtu kuangukia hapo ni mkubwa sana
 
July 4= 7 +4=11,Sept 11=9+1+1=11,,,angalia kifo cha kanumba jumlisha ni 11,Angalia tarehe akina JAY Z wanatoaga nyimbo zao jumlisha ni 11,tafuta na angalia matukio makubwa makubwa duniani jumlisha siku na mwezi utapatA 11.hii ni namba ya matukio ya hao akina..........
illuminant
 
Back
Top Bottom