Siri ya kuishi miaka mingi hapa Duniani ni kuishi Kwa matumaini

Lighton

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
2,231
Reaction score
3,737
Heri ya sikuu ya pasaka.

Siri ya kuishi miaka mingi hapa Duniani ni kuishi Kwa matumaini, kuishi Kwa kuamini kwamba kesho itakuwa Bora, kupiga moyo konde na kuendelea kupambana Kwa matumaini ya kuipambania Tena kesho.

Akija mtu kukwambiya kwamba, hakuna uhakika wa kuiona kesho, huyo mtu anapandikiza Hisia za uoga ndani yako Ili, ikaaangamize hali ya uhai ambayo ni matumaini.

Tumaini ni hali ya msukumo wa kiimani, kuamini kwamba upo mda, na nafasi ya kufanikisha kile unachokipambania. Anayefikiria hakuna muda au nafasi nyingine ya kuzaa matunda ya juhudi zake, huyo anajimaliza mwenyewe bila ya kujua. Mtu wa Aina hiyo anajilimbikizia mzigo wa mawazo ambao baadae humsababishia matatizo mbalimbali ambayo husababisha kifo chake.

Mfano wa matatizo hayo ni magonjwa Kama kisukari,presha,ajali, suicide nk.

Uoga ni Hisia mbaya, zinazotokana na hofu ambayo mtu huipata,kuhusu jambo fulani. Inaweza kuwa changamoto ya maisha ya ukosefu wa ajira na umasikini, kufeli mtihani nk.

Kila mtu hupitia hali tofauti za uoga kwenye maisha, lakini hali ya uoga, ambayo husababisha msongo wa mawazo, ni mbaya kuliko hali ya kawaida, ya kuogopa wanyama wakali.

Waathirika zaidi wa hali hii ni wale wasiokuwa na matumaini, Kwa lugha nyingine ni watu waliokata tamaa., wale wasiopiga moyo konde kuamini kwamba juhudi zao hazitaenda Bure. Kuwa na matumaini ni kuamini, huwezi kuwa na matumaini pasipo kuamini, Hapa Atheist huonekana wanafki sana.

Kuamini ni nini? Ni kuamini vile MUNGU anasema.
MUNGU Anasema nini?

MUNGU Anasema "Ombeni nanyi mtapewa,Tafuteni nanyi mtaona,Bisheni nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila aombaye hupewa,Na kila atafutaye huona na kila Abishaye hufunguliwa(Mt 7:7-8)

Njooni kwangu Ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo mizito nami nitawapumzisha, Jitieni nira yangu mkajifunze kwangu Kwa maana Mimi ni mpole na mnyenyekevu, nanyi mtapata Raha nafsini mwenu(Mt 11:28-29)

Kwa ufupi, waliokaribu na MUNGU sana, wengi wana matumaini na wengi wameishi miaka mingi na wengi wanastawi kila siku.

Sometimes mtu au watu wanaweza kuhisi wewe ni mshirikina kwasababu hupatwi sana na matatizo. Unaweza ukawa unakula mboga za majani kila siku lakini ukawa na furaha, siyo kwasababu umeridhika na maisha, hapana ni kwasababu unajua kesho utakula nyama na pilau, kwasababu pia unapambana, na kamwe juhudi zako hazitaenda Bure. MUNGU alimwambiya Adamu "utailima ardhi mpaka ikupe mazao. Never say never, binadamu amekuja Duniani kupambana na kufanikiwa, siyo kukata tamaa.

Ujumbe wa pasaka:Tujitahidi kuwa karibu na MUNGU kwa mawazo na kwa matendo, kamwe tusikate tamaa, Wala tusiwe na chuki. Destiny has no competition, Run your race and wish others well.

Jioni njema🙏
 
Well Said!
 
Back
Top Bottom