Nar
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Kwa hiyo wewe unataka kujidanganya kwamba akina Mo kwa vile wamepanga upanga ndio hawana nyumba?au unadhani hawajawahi kujenga?acha kufuata mkumbo mkuu utaingia chaka.
Unamtolea mfano Gulam Dewji au Mo Dewji kwa mfano akifukuzwa kwenye nyumba ya kupanga,akiuza godowns zake za kutunzia magari hawezi kujenga nyumba?au akifukuzwa fenicha zake ataenda kuzihifadhi kwenye godowns zake,je wewe mwenzangu na mie utafanyaje?
Sent from my SM-C7000 using
JamiiForums mobile app
Narudia kwenye comment ya juu kabisa.
"Tengeneza secondary/other sources of incomes"
Mimi binafsi naishi mkoani Ila Nina nyumba ya kupangisha dar@kinondoni.
Kwa mwezi nakusanya si haba.
Nataka kutengeneza nyengine G.Mboto (Bro kaniambia kasikia nyumba inauzwa pale G.Mboto).
Nikuchukua hii nikaifanyia matengenezo nitatoboa (nyumba za ule mtaa hazina miaka zaidi ya 6)
Nimeajiriwa 2014 Ila nimepanga..!!
Kwasasa mkatengeneza MIFEREJI kwanza.
Hiyo MIFEREJI ndio ijenge nyumba za kuishi na inunue gari na sio mshahara wangu.
Lengo langu ikifike wakati niachane na mshahara ukae benki miaka
Yaani najaza standing order, mshahara ukitoka benki wapeleke saving account ukatengeneze return.
Achana na hizo liabilities, tengeneza kwanza asset za kukuingizia pesa, halafu hizo assets ndio zizalishe matumizi ya hizo liabilities
Nikupe mfano:- hiyo nyumba YAKO what if ingekuwa uswahilini mfano Mwananyamala na kule chumba 50k
Tuseme nyumba ina vyumba 6.
Inamaana wewe kila mwezi una laki 3.
Ungechukua hizo laki 3, ukajichanga na madili + mishahara, unatengeneza nyengine uswahilini kwengine.
Then baada ya miaka 5 - 10 hivi una nyumba 3 tuseme total vyumba 20.
Kwahiyo kila mwezi unaingiza Mil 1.
Halafu sasa ndio ujenge YAKO ya kuishi..!!!
#YNWA