Siri ya kutokukosa hela tena (Kutokufulia) hii hapa. Soma hutajuta...

Elimu ya uchumi binafsi ipp katika kiwango kibaya sana hii nchi
 
Unazungumziaje wale watu waliofuata km ulivyosema au shauri,lkn bado wana hali ngumu kiuchumi?.
 
dudu jeupe,
Aisee nimekupata kaka na kW huu ujumbe naamin in njia mojawapo yangu Mimi kuanza mapambano upya baada y mawazo y mda mref kW namna gan nawez kutengeneza hela,be blessed brother
 
Kwa hiyo unajiona maisha umeishayapatia kwa kuwa na nyumba na flat screen. Hizo ni liabilities hazikuingiziu chochote
 
Tumtunzie nani pesa? Maisha ni haya haya fanya unachopenda. Maisha sio vita jamani!
 
Ahahahaha mkubwa naona umeamua kutuchana ..[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kweli tuko tofauti..

Nilianza ajira nikiwa na miaka 24 (2014) Ila sijawahi fikiria kujenga ndio mafanikio na Wala usiwazi kujenga.

Kwanini tusifungue biashara tukamiliki mahisa, hivi kujenga ni mafanikio nayo?

#YNWA
 
Umeongea sahihi Ila ngoja Nikupe mfano tu;

Ubahili ni nguzo ya utajiri kwa uliyezaliwa umasikinini ..
Kuna jamaa mmoja ni yatima ye alikuwa kwa kudra za Mungu na sasa ana ajira.

Aliajiriwa 2015 serikalini.

Akaanza kuwa bahili.
Ubahili wake umemfanya awe na nunue mashamba makubwaa, maana hutunza pesa mwaka mzima halafu December (likizo) huenda kununua mashamba.

Alivyofika Eka 100 aliamua kupanda parachichi, kaanza 2020.

Pia kwa ubahili wake, ameweza kupanda eneo kubwaa mara MOJA.

Anaamini sanaa kwenye kilimo na anakomaa nacho.

Hana source nyengine ya pesa na yeye anakwambia INVESTMENT IS BETTER THEN BUSINESS.

POINT YANGU NI KWAMBA:-
Wakati una source MOJA, ukiwa unatengeneza ya pili UBAHILI MUHIMU na ni nguzo ya kujenga hiyo ya pili.

#YNWA
 
Umeongea sahihi Ila ngoja Nikupe mfano tu;

Ubahili ni nguzo ya utajiri kwa uliyezaliwa umasikinini ..
Kuna jamaa mmoja ni yatima ye alikuwa kwa kudra za Mungu na sasa ana ajira.

Aliajiriwa 2015 serikalini.

Akaanza kuwa bahili.
Ubahili wake umemfanya awe na nunue mashamba makubwaa, maana hutunza pesa mwaka mzima halafu December (likizo) huenda kununua mashamba.

Alivyofika Eka 100 aliamua kupanda parachichi, kaanza 2020.

Pia kwa ubahili wake, ameweza kupanda eneo kubwaa mara MOJA.

Anaamini sanaa kwenye kilimo na anakomaa nacho.

Hana source nyengine ya pesa na yeye anakwambia INVESTMENT IS BETTER THEN BUSINESS.

POINT YANGU NI KWAMBA:-
Wakati una source MOJA, ukiwa unatengeneza ya pili UBAHILI MUHIMU na ni nguzo ya kujenga hiyo ya pili.

#

Mnakuaje mabahili halafu mnajenga liabilities?

Maana nyumba ya kuishi ni liability, itahitaji maji, umeme, matengenezo na ....
Nafikiria tuwe mabahiri huku tukitengeneza cash generating assets.

Tujenge nyumba ZA KUPANGISHA
Tununue mashamba ya kupanda mfano miti, matunda ili tuuze hizo products.
Tununue hisa...

Unakuaje bahili halafu at the end unaishia kumiliki malii zisizozalisha?

#YNWA
 
Huu ulimwengu umejawa na mashauri kibao, ila kama Mungu alikupangia utaishi hivi, hata hakuna mwanadamu anaweza weka nguvu yake kubadilisha
Mungu akupangii uwe na madeni benki.
Mungu akupangii upate pesa ya mshahara leo kesho iwe imeisha.
Mungu akupangii uishi maisha ya madeni kwasababu mshahara hautoshi.

Ni akili zako binafsi.

Tafuta Financial intelligency.

#YNWA
 
Mkuu huwezi kupata utulivu wa kufikiria maendeleo kama upo kwenye nyumba ya kupanga huku unafikiria muda wowote mwenye nyumba atakuja kukugongea mlango kudai kodi yake.
Ili kuondoa huo usumbufu ndio huwa tunaamua kukomaa kujenga nyumba ya kuishi then baada ya hapo ndio utaamua ujenge nyumba nyingine ya kupangisha au biashara nyingine.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo unajiona maisha umeishayapatia kwa kuwa na nyumba na flat screen. Hizo ni liabilities hazikuingiziu chochote
Bado maisha sijayapatia ila naamini nimejiwekea msingi mzuri.
Huwezi kupata utulivu wa kufocus maendeleo kama upo kwenye nyumba ya kupanga na unadaiwa kodi.

Kuishi kwenye nyumba yako kuna heshima yake.
Acha kuishi kwa theories kuwa real utakuja kubuma ujute.
Biashara huwa zina msimu sio kila siku zitakuletea pesa tu,kuna wakati huwa zinagoma na mwenye nyumba anataka kodi yake hapo ndipo utakapojua kuwa hujui.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu uko sahihi.
Lakini hata waliozaliwa kwenye utajiri pia ni wabahili tena zaidi ya maskini.
Mfano angalia wakina Mo dewji wanavyowafanyisha watu kazi ngumu kwenye viwanda vyao kisha wanawalipa elfu 6 kwa siku.
Huu sio ubahili?

Kwa mfano sisi watu wa kawaida wenye mishahara jamaa yako au rafiki yako akikusikitikia shida kumpa elfu 50 au laki ni kitu cha kawaida.
Au kukaa bar na kumnunulia kinywaji mtu mliyejuana siku hiyo hiyo ni kawaida.
Ila kwa matajiri hawatoagi hela kama hizi japo akaunti zao zinasoma bilioni kadhaa.
Huo ndio ubahili wenyewe sasa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nimekosa Mkopo bank kwa Kutokuwa na nyumba ama kwa hakika bora ujenge Nyumba utafungua milango.
 
Unamjua Gulam Dewji..
Baba wa Mohamed Dewji mwenye METL.

Yule mdingi ana nyumba amepanga Kati ya upanga au masaki.

Maana pia ana mdogo ake (fazal Dewji@baba mdogo wa Mohamed Dewji) sasa Kati yao mmoja yupo upanga mwengine masaki na wotee wamepanga.

Diamond platinumz pamoja na utajiri wotee alionao Ila kapanga kwa madale.

Kumiliki nyumba ya kuishi SI UTAJIRI.

Kabla ya kumiliki nyumba na/au gari hebu tengeneza MIFEREJI YA PESA KWANZA.

#YNWA
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Kwa hiyo wewe unataka kujidanganya kwamba akina Mo kwa vile wamepanga upanga ndio hawana nyumba?au unadhani hawajawahi kujenga?acha kufuata mkumbo mkuu utaingia chaka.
Unamtolea mfano Gulam Dewji au Mo Dewji kwa mfano akifukuzwa kwenye nyumba ya kupanga,akiuza godowns zake za kutunzia magari hawezi kujenga nyumba?au akifukuzwa fenicha zake ataenda kuzihifadhi kwenye godowns zake,je wewe mwenzangu na mie utafanyaje?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nar
Narudia kwenye comment ya juu kabisa.

"Tengeneza secondary/other sources of incomes"

Mimi binafsi naishi mkoani Ila Nina nyumba ya kupangisha dar@kinondoni.

Kwa mwezi nakusanya si haba.

Nataka kutengeneza nyengine G.Mboto (Bro kaniambia kasikia nyumba inauzwa pale G.Mboto).
Nikuchukua hii nikaifanyia matengenezo nitatoboa (nyumba za ule mtaa hazina miaka zaidi ya 6)

Nimeajiriwa 2014 Ila nimepanga..!!

Kwasasa mkatengeneza MIFEREJI kwanza.

Hiyo MIFEREJI ndio ijenge nyumba za kuishi na inunue gari na sio mshahara wangu.

Lengo langu ikifike wakati niachane na mshahara ukae benki miaka

Yaani najaza standing order, mshahara ukitoka benki wapeleke saving account ukatengeneze return.

Achana na hizo liabilities, tengeneza kwanza asset za kukuingizia pesa, halafu hizo assets ndio zizalishe matumizi ya hizo liabilities

Nikupe mfano:- hiyo nyumba YAKO what if ingekuwa uswahilini mfano Mwananyamala na kule chumba 50k

Tuseme nyumba ina vyumba 6.
Inamaana wewe kila mwezi una laki 3.

Ungechukua hizo laki 3, ukajichanga na madili + mishahara, unatengeneza nyengine uswahilini kwengine.

Then baada ya miaka 5 - 10 hivi una nyumba 3 tuseme total vyumba 20.

Kwahiyo kila mwezi unaingiza Mil 1.

Halafu sasa ndio ujenge YAKO ya kuishi..!!!

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…