Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la Leo.
Lengo la vyombo vya habari, ni kuihudumia jamii, ukikutana na jambo fulani zuri, linawezeza kuisaidia jamii, unaliandika ili kushea na wengine. Leo nawaletea topi ngumu kidogo ya jambo linalohusu kupata mafanikio kwa kutumia kitu kinachoitwa Manifestation.
Angalizo: Hii topic sio imani ya dini yoyote, hii ni kwa ajili ya watu “open minded”
Kuna watu wa aina mbili, “open minded” na closed minded”.
Open minded ni wale wanaofikiria wenyewe, akiambiwa jambo lolote, kabla ya kuliamini, unalifikiria kwanza kisha kulikubali na kuliamini.
Closed minded ni wale ambao, wakiambiwa jambo, wanaamini moja moja, hawahitaji kufikiria.
Hii topic ni ya watu wanao fikiria, lakini wale waliofikirishwa na kuziamini dini zao, hapa sii mahala pao, ili tusije kuleta mabishano ya kiimani za dini. Samo bandiko hili huku umeshikilia imani ya dini yako!.
Manifestation ni kulidhamiria jambo kwa dhati ya moyo wako, hiyo dhati ya dhamira yako, na juhudi yako kulifanikisha, inazifungua nguvu zilizoko ndani yako na kulitimiza hili jambo lako na linakuwa.
Leo nawaendeshea somo la manifestation kama lilivyoandikwa na mwandishi Ingrid Clarke katika kitabu cha 7 Pillars of Manifestations, yaani nguzo 7 za manifestations.
Nguzo hizo ni
Katika bandiko langu kuhusu psychic powers, nilisema kitu chenye nguvu sana katika mwili wa mwanadamu ni nia, “will power”, wazungu wanasema “where there is a will, there is a way”, msemo huu hata Waswahili tunao, unaosema, “penye nia, pana njia”.
Manifestation ni kitendo cha kutumia mawazo yako, kufungua milango ya nguvu zilizo ndani yako, kufanikisha mambo yako.
Dini zote zinatufundisha tumeumbwa na Mungu, na kuelezwa huyo Mungu yuko kule juu mbinguni, peponi, ahera, hivyo ukifa bila dhambi utaingia mbinguni na kumuona Mungu. Ukifa na dhambi utakwenda motoni kwa shetani kwenye jehanum ya moto wa milele. Hivyo wengi wakisani wanatazama juu wakijua ni kweli Mungu juu mbinguni kule mawinguni.
Ukweli ni kuwa mbinguni na motoni ni hapa hapa duniani, kuna ulimwengu mbili, ulimwengu wa mwili “physical world” na ulimwengu war oho, “spiritual world”
Mungu alimuumba binadamu kwa kufinyanga udogo, kisha akampulizia pumzi ya uhai, “life force”, hivyo mwili wa binadamu una sehemu mbili, mwili wa nyama, “physical body” na mwili wa roho “spiritual body”. Mtu anapokufa, japo wanaita amekata roho, kinachokufa ni mwili wa nyama tuu ambao unazikwa na kurejea kuwa mavumbi, lakini roho inatoka, na kurejea kwake, “sote ni wa Mungu, na kwake tutarejea”, hata ile siku ya mwisho ya ufufuko wa miili, miili inayofufuliwa ni miili ya roho, hii miili ya nyama, ukifa, ndio mwisho wake, hivyo wanaochoma, wako right, na wanaozika kwa heshima zote, masanduku ya gharama na kujengea makaburi, ni kujifurahisha tuu nafsi zao, mtu akiisha kufa, ile mwili hauna issue tena!.
Sasa ile pumzi, roho ambayo Mungu amempulizia binadamu, ni roho ya Mungu, hivyo kila binadamu anao u Mungu ndani yake!. Ile dhana kuwa Mungu yuko mbinguni ameketi kwenye kiti cha enzi, ni kweli, ila pia Mungu yuko ndani yako, kupitia roho yake, nah ii ni ile kanuni ya omnipresence of God.
Manifestation ni kitendo cha kumtumia Mungu aliyeko ndani yako, kumtuma akunyooshe mambo yako!.
Hivyo sisi Binadamu tuna nguvu, powers za kufanya mambo mengi, lakini wengi hawajijui kuwa wanazo. Wale wahubiri wa miujiza ya uponyaji, ni wanatumia uwezo wao kukumanifestia, kinachokufanya ni imani yako na nguvu zilizo ndani yako na sio nguvu za huyu muhubiri.
Kwa vile tumepewa nguvu hizi bure, kuzitumia pia ni bure, unachotakiwa kufanya ni kuamini tuu!, baada ya kusoma kuhusu manifestation nikaona ni jambo jema, let me share na watu humu, wazitumie nguvu zilizo ndani yao kufanya mambo makubwa na kujiletea maendeleo.
Hivyo hii topic ya manifestation, itakupa fursa ya kutumia nguvu ya mawazo yako kufungua nguvu zilizomo ndani yako, “the power of your mind” kukuletea mafanikio kwenye maisha yako, kwa urahisi kabisa, kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho ni imani tuu, kuamini wewe unaweza, umeumbwa na nguvu na uwezo wa Kimungu uliomo ndani yako, na unaweza kuufungulia na kuutumia kujipatia mafanikio na kujiletea maendeleo .
Nguvu ya manifestion ni kutumia tuu mawazo, kutengeneza ndoto za mafanikio, na kutumia nguvu iliyomo ndani yako kuifanya ndoto yako iwe kweli, hivyo kutimiza ndoto yako.
Mfano wewe unataka kupata fedha nyingi, uwe tajiri, kupitia manifestation, unawaza tuu jinsi ya kupata pesa, kisha unaamini utapata pesa, unaweka juhudi kwenye kutafuta pesa, kisha nguvu za Mungu zilizomo ndani yako, zitakufungulia milango ya shughuli za kupata pesa, utapata pesa na kuuaga umasikini.
Upataji pesa kupitia manifestation, sio kuamini tuu na kulala kitandani, kisha ukiamka asubuhi, unakuta umeletewa pesa chini ya mto!, no!, upataji mafanikio kupitia manifestations, kuna misingi yake, 7, kuna sheria zake, kanuni zake na utaratibu wake wa utekelezaji, lazima ufanye bidii kukipata kile unachotaka.
Tukutane wiki ijayo, nitakapo kuletea hiyo misingi 7 ya manifestations, kitu muhimu ni kukumbuka tuu kuwa kila binadamu amekuja hapa duniani akiwa mtu na ataondoka mtupu, kupata na kukosa, ni juhudi tuu na maarifa kama haya.
Wasalaam
Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu nguvu za kufanya mambo

- Foundation: Msingi wa Manifestation
- Laws: Sheria za Manifestation
- Vibrations:Mitetemo ya Manifestation
- Intention: Kuweka Nia
- Visualization: Kuona kwa jicho la ndani
- Affirmations: Kukuamini ni kweli
- Process: Utekelezaji wa Manifestation.

- Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?
- "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!
- Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu Kiongozi Tunayemtaka!. Mdomo Huumba!.
- "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia