Siri ya Mafanikio Kupitia Manifestation -1: Manifestation ni Nini?

Unakuta mbongo anasubiria connection ili atoboe au apate kazi.
Connection haikufuati bali we ndo unaitafuta
It's true, mafanikio it's all about connections, kuwa connected, manifestation inakufungulia njia za connections unakuwa connected. Hata kwenye siasa, ili ufanikiwe kisiasa ni lazima uwe na manifesto nzuri, neno manifesto, limetokana na manifestation.
P
 
Ee Bana Paskali wiki ijayo mida ya saa 👍
Hizi ni ngoma za Jumapili hadi Jumapili, huwa naziandika Jumamosi usiku, kisha Jumapili nikitoka church, napiga brunch, kisha natulia kidogo kucheza na vijukuu kisha ndio nashusha jf mida ya mchana mchana.
P
 
matumizi ya numbers ni numerology, ni kama mambo ya aastrology na palmistry ni mambo ya ubashiri, au Kiislamu shirki, hizo unazoziita nguvu za universe, sio za universe bali ziko ndani yako.
P
Matumizi ya number yapo pande zote kwenye Nuru na Giza inategemea unaegemea upande upi.
Shetani kaiga kila kitu toka kwa Mungu
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la Leo.
View attachment 3012705
Lengo la vyombo vya habari, ni kuihudumia jamii, ukikutana na jambo fulani zuri, linawezeza kuisaidia jamii, unaliandika ili kushea na wengine. Leo nawaletea topi ngumu kidogo ya jambo linalohusu kupata mafanikio kwa kutumia kitu kinachoitwa Manifestation.

Angalizo: Hii topic sio imani ya dini yoyote, hii ni kwa ajili ya watu “open minded”

Kuna watu wa aina mbili, “open minded” na closed minded”.

Open minded ni wale wanaofikiria wenyewe, akiambiwa jambo lolote, kabla ya kuliamini, unalifikiria kwanza kisha kulikubali na kuliamini.

Closed minded ni wale ambao, wakiambiwa jambo, wanaamini moja moja, hawahitaji kufikiria.

Hii topic ni ya watu wanao fikiria, lakini wale waliofikirishwa na kuziamini dini zao, hapa sii mahala pao, ili tusije kuleta mabishano ya kiimani za dini. Samo bandiko hili huku umeshikilia imani ya dini yako!.

Manifestation ni kulidhamiria jambo kwa dhati ya moyo wako, hiyo dhati ya dhamira yako, na juhudi yako kulifanikisha, inazifungua nguvu zilizoko ndani yako na kulitimiza hili jambo lako na linakuwa.

Leo nawaendeshea somo la manifestation kama lilivyoandikwa na mwandishi Ingrid Clarke katika kitabu cha 7 Pillars of Manifestations, yaani nguzo 7 za manifestations.

Nguzo hizo ni
  1. Foundation: Msingi wa Manifestation
  2. Laws: Sheria za Manifestation
  3. Vibrations:Mitetemo ya Manifestation
  4. Intention: Kuweka Nia
  5. Visualization: Kuona kwa jicho la ndani
  6. Affirmations: Kukuamini ni kweli
  7. Process: Utekelezaji wa Manifestation.
Manifestation ni nini?

Katika bandiko langu kuhusu psychic powers, nilisema kitu chenye nguvu sana katika mwili wa mwanadamu ni nia, “will power”, wazungu wanasema “where there is a will, there is a way”, msemo huu hata Waswahili tunao, unaosema, “penye nia, pana njia”.

Manifestation ni kitendo cha kutumia mawazo yako, kufungua milango ya nguvu zilizo ndani yako, kufanikisha mambo yako.

Dini zote zinatufundisha tumeumbwa na Mungu, na kuelezwa huyo Mungu yuko kule juu mbinguni, peponi, ahera, hivyo ukifa bila dhambi utaingia mbinguni na kumuona Mungu. Ukifa na dhambi utakwenda motoni kwa shetani kwenye jehanum ya moto wa milele. Hivyo wengi wakisani wanatazama juu wakijua ni kweli Mungu juu mbinguni kule mawinguni.

Ukweli ni kuwa mbinguni na motoni ni hapa hapa duniani, kuna ulimwengu mbili, ulimwengu wa mwili “physical world” na ulimwengu war oho, “spiritual world”

Mungu alimuumba binadamu kwa kufinyanga udogo, kisha akampulizia pumzi ya uhai, “life force”, hivyo mwili wa binadamu una sehemu mbili, mwili wa nyama, “physical body” na mwili wa roho “spiritual body”. Mtu anapokufa, japo wanaita amekata roho, kinachokufa ni mwili wa nyama tuu ambao unazikwa na kurejea kuwa mavumbi, lakini roho inatoka, na kurejea kwake, “sote ni wa Mungu, na kwake tutarejea”, hata ile siku ya mwisho ya ufufuko wa miili, miili inayofufuliwa ni miili ya roho, hii miili ya nyama, ukifa, ndio mwisho wake, hivyo wanaochoma, wako right, na wanaozika kwa heshima zote, masanduku ya gharama na kujengea makaburi, ni kujifurahisha tuu nafsi zao, mtu akiisha kufa, ile mwili hauna issue tena!.

Sasa ile pumzi, roho ambayo Mungu amempulizia binadamu, ni roho ya Mungu, hivyo kila binadamu anao u Mungu ndani yake!. Ile dhana kuwa Mungu yuko mbinguni ameketi kwenye kiti cha enzi, ni kweli, ila pia Mungu yuko ndani yako, kupitia roho yake, nah ii ni ile kanuni ya omnipresence of God.

Manifestation ni kitendo cha kumtumia Mungu aliyeko ndani yako, kumtuma akunyooshe mambo yako!.

Hivyo sisi Binadamu tuna nguvu, powers za kufanya mambo mengi, lakini wengi hawajijui kuwa wanazo. Wale wahubiri wa miujiza ya uponyaji, ni wanatumia uwezo wao kukumanifestia, kinachokufanya ni imani yako na nguvu zilizo ndani yako na sio nguvu za huyu muhubiri.

Kwa vile tumepewa nguvu hizi bure, kuzitumia pia ni bure, unachotakiwa kufanya ni kuamini tuu!, baada ya kusoma kuhusu manifestation nikaona ni jambo jema, let me share na watu humu, wazitumie nguvu zilizo ndani yao kufanya mambo makubwa na kujiletea maendeleo.

Hivyo hii topic ya manifestation, itakupa fursa ya kutumia nguvu ya mawazo yako kufungua nguvu zilizomo ndani yako, “the power of your mind” kukuletea mafanikio kwenye maisha yako, kwa urahisi kabisa, kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho ni imani tuu, kuamini wewe unaweza, umeumbwa na nguvu na uwezo wa Kimungu uliomo ndani yako, na unaweza kuufungulia na kuutumia kujipatia mafanikio na kujiletea maendeleo .

Nguvu ya manifestion ni kutumia tuu mawazo, kutengeneza ndoto za mafanikio, na kutumia nguvu iliyomo ndani yako kuifanya ndoto yako iwe kweli, hivyo kutimiza ndoto yako.

Mfano wewe unataka kupata fedha nyingi, uwe tajiri, kupitia manifestation, unawaza tuu jinsi ya kupata pesa, kisha unaamini utapata pesa, unaweka juhudi kwenye kutafuta pesa, kisha nguvu za Mungu zilizomo ndani yako, zitakufungulia milango ya shughuli za kupata pesa, utapata pesa na kuuaga umasikini.

Upataji pesa kupitia manifestation, sio kuamini tuu na kulala kitandani, kisha ukiamka asubuhi, unakuta umeletewa pesa chini ya mto!, no!, upataji mafanikio kupitia manifestations, kuna misingi yake, 7, kuna sheria zake, kanuni zake na utaratibu wake wa utekelezaji, lazima ufanye bidii kukipata kile unachotaka.

Tukutane wiki ijayo, nitakapo kuletea hiyo misingi 7 ya manifestations, kitu muhimu ni kukumbuka tuu kuwa kila binadamu amekuja hapa duniani akiwa mtu na ataondoka mtupu, kupata na kukosa, ni juhudi tuu na maarifa kama haya.

Wasalaam

Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu nguvu za kufanya mambo
Asante
 
Alaumiwe Mungu, katupa nguvu zote kisha anawafunulia wachache uwezo wa kutambua nguvu zilizomo ndani yetu. Kwani kuna tatizo gani leo Mungu akatufunulia kila mtu tukaona yote waonayo wengine tusiyoyaona?

Kuna mtu kasema tufanye kazi, kuna watu wanasema kazi ni utumwa, wote tunatafuta pesa lakini pesa ni chache watu tuko wengi.

Lini tuta balance maokoto, Yani Mo na mimi tupate sawa kama ni TSH 1000 kwake na kwangu hivyo hivyo, bila kuwasahau wajukuu wa Matonya mitaani.

Katoliki walitufundisha Mungu baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu, na tuombapo eti maombi yetu yapitie kwa Yesu Kristo bwana wetu, sana huyu umsemaye aliyemo ndani mwetu kupitia roho mtakatifu ni yupi tena kaka?

Mnatuchanganya, sana au walimu wa katekisimu ndio walituchanganya?

Minifestatioon ni Kujiongeza kwa maana nyingine, Majambazi tuansema yanatenda dhambi, wakati yamejiongeza, dhambi ni nini?

Mnatuvuruga sana mkuu, anyway ngoja niwe nanunua mikeka kila siku natumia Mungu anayeishi mwilini mwangu nione kama atasaidia, au Miungu wetu wamezeeka au wamelala?

Tukienda makanisani ku wa revive tunapigwa damn.
 
Ni kweli kabisa, na ndizo zinazotumiwa na wahubiri wengi wa wokovu kuwaaminisha waumini wao kuwa wao ni powerful, hivyo waumini wanammanifestia kiongozi wao na kupeleka maokoto ya sadaka wakijua ni wanamtolea Mungu, na kiukweli wanakamuliwa haswa.
P
Kaka Pascal na hii ya kanisa unaloabudu (nami pia) la Roman Catholic la kusema usipolipa zaka na michango mingine hatutakuzika pindi unapokufa wewe na familia yako imekaaje?
Ningetamani siku upandishe uzi hapa
 
Hiyo ni dhulma kubwa sana kwa waumini na sio mpango wa Mungu!, ila roho ikiisha acha mwili, mwili hauna issues tena, yale maziko ya kanisa hayaongezi chochote bali ni faraja tuu kwa wafiwa, tungekuwa tunatembelea mwili kuufunua seven days baada ya kuzika, wengi wange opt for cremation!, uzikwe na kanisa, usizikwe, uchomwe, uzame , upotee, it makes no difference.

P
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la Leo.
View attachment 3012705
Lengo la vyombo vya habari, ni kuihudumia jamii, ukikutana na jambo fulani zuri, linawezeza kuisaidia jamii, unaliandika ili kushea na wengine. Leo nawaletea topi ngumu kidogo ya jambo linalohusu kupata mafanikio kwa kutumia kitu kinachoitwa Manifestation.

Angalizo: Hii topic sio imani ya dini yoyote, hii ni kwa ajili ya watu “open minded”

Kuna watu wa aina mbili, “open minded” na closed minded”.

Open minded ni wale wanaofikiria wenyewe, akiambiwa jambo lolote, kabla ya kuliamini, unalifikiria kwanza kisha kulikubali na kuliamini.

Closed minded ni wale ambao, wakiambiwa jambo, wanaamini moja moja, hawahitaji kufikiria.

Hii topic ni ya watu wanao fikiria, lakini wale waliofikirishwa na kuziamini dini zao, hapa sii mahala pao, ili tusije kuleta mabishano ya kiimani za dini. Samo bandiko hili huku umeshikilia imani ya dini yako!.

Manifestation ni kulidhamiria jambo kwa dhati ya moyo wako, hiyo dhati ya dhamira yako, na juhudi yako kulifanikisha, inazifungua nguvu zilizoko ndani yako na kulitimiza hili jambo lako na linakuwa.

Leo nawaendeshea somo la manifestation kama lilivyoandikwa na mwandishi Ingrid Clarke katika kitabu cha 7 Pillars of Manifestations, yaani nguzo 7 za manifestations.

Nguzo hizo ni
  1. Foundation: Msingi wa Manifestation
  2. Laws: Sheria za Manifestation
  3. Vibrations:Mitetemo ya Manifestation
  4. Intention: Kuweka Nia
  5. Visualization: Kuona kwa jicho la ndani
  6. Affirmations: Kukuamini ni kweli
  7. Process: Utekelezaji wa Manifestation.
Manifestation ni nini?

Katika bandiko langu kuhusu psychic powers, nilisema kitu chenye nguvu sana katika mwili wa mwanadamu ni nia, “will power”, wazungu wanasema “where there is a will, there is a way”, msemo huu hata Waswahili tunao, unaosema, “penye nia, pana njia”.

Manifestation ni kitendo cha kutumia mawazo yako, kufungua milango ya nguvu zilizo ndani yako, kufanikisha mambo yako.

Dini zote zinatufundisha tumeumbwa na Mungu, na kuelezwa huyo Mungu yuko kule juu mbinguni, peponi, ahera, hivyo ukifa bila dhambi utaingia mbinguni na kumuona Mungu. Ukifa na dhambi utakwenda motoni kwa shetani kwenye jehanum ya moto wa milele. Hivyo wengi wakisani wanatazama juu wakijua ni kweli Mungu juu mbinguni kule mawinguni.

Ukweli ni kuwa mbinguni na motoni ni hapa hapa duniani, kuna ulimwengu mbili, ulimwengu wa mwili “physical world” na ulimwengu war oho, “spiritual world”

Mungu alimuumba binadamu kwa kufinyanga udogo, kisha akampulizia pumzi ya uhai, “life force”, hivyo mwili wa binadamu una sehemu mbili, mwili wa nyama, “physical body” na mwili wa roho “spiritual body”. Mtu anapokufa, japo wanaita amekata roho, kinachokufa ni mwili wa nyama tuu ambao unazikwa na kurejea kuwa mavumbi, lakini roho inatoka, na kurejea kwake, “sote ni wa Mungu, na kwake tutarejea”, hata ile siku ya mwisho ya ufufuko wa miili, miili inayofufuliwa ni miili ya roho, hii miili ya nyama, ukifa, ndio mwisho wake, hivyo wanaochoma, wako right, na wanaozika kwa heshima zote, masanduku ya gharama na kujengea makaburi, ni kujifurahisha tuu nafsi zao, mtu akiisha kufa, ile mwili hauna issue tena!.

Sasa ile pumzi, roho ambayo Mungu amempulizia binadamu, ni roho ya Mungu, hivyo kila binadamu anao u Mungu ndani yake!. Ile dhana kuwa Mungu yuko mbinguni ameketi kwenye kiti cha enzi, ni kweli, ila pia Mungu yuko ndani yako, kupitia roho yake, nah ii ni ile kanuni ya omnipresence of God.

Manifestation ni kitendo cha kumtumia Mungu aliyeko ndani yako, kumtuma akunyooshe mambo yako!.

Hivyo sisi Binadamu tuna nguvu, powers za kufanya mambo mengi, lakini wengi hawajijui kuwa wanazo. Wale wahubiri wa miujiza ya uponyaji, ni wanatumia uwezo wao kukumanifestia, kinachokufanya ni imani yako na nguvu zilizo ndani yako na sio nguvu za huyu muhubiri.

Kwa vile tumepewa nguvu hizi bure, kuzitumia pia ni bure, unachotakiwa kufanya ni kuamini tuu!, baada ya kusoma kuhusu manifestation nikaona ni jambo jema, let me share na watu humu, wazitumie nguvu zilizo ndani yao kufanya mambo makubwa na kujiletea maendeleo.

Hivyo hii topic ya manifestation, itakupa fursa ya kutumia nguvu ya mawazo yako kufungua nguvu zilizomo ndani yako, “the power of your mind” kukuletea mafanikio kwenye maisha yako, kwa urahisi kabisa, kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho ni imani tuu, kuamini wewe unaweza, umeumbwa na nguvu na uwezo wa Kimungu uliomo ndani yako, na unaweza kuufungulia na kuutumia kujipatia mafanikio na kujiletea maendeleo .

Nguvu ya manifestion ni kutumia tuu mawazo, kutengeneza ndoto za mafanikio, na kutumia nguvu iliyomo ndani yako kuifanya ndoto yako iwe kweli, hivyo kutimiza ndoto yako.

Mfano wewe unataka kupata fedha nyingi, uwe tajiri, kupitia manifestation, unawaza tuu jinsi ya kupata pesa, kisha unaamini utapata pesa, unaweka juhudi kwenye kutafuta pesa, kisha nguvu za Mungu zilizomo ndani yako, zitakufungulia milango ya shughuli za kupata pesa, utapata pesa na kuuaga umasikini.

Upataji pesa kupitia manifestation, sio kuamini tuu na kulala kitandani, kisha ukiamka asubuhi, unakuta umeletewa pesa chini ya mto!, no!, upataji mafanikio kupitia manifestations, kuna misingi yake, 7, kuna sheria zake, kanuni zake na utaratibu wake wa utekelezaji, lazima ufanye bidii kukipata kile unachotaka.

Tukutane wiki ijayo, nitakapo kuletea hiyo misingi 7 ya manifestations, kitu muhimu ni kukumbuka tuu kuwa kila binadamu amekuja hapa duniani akiwa mtu na ataondoka mtupu, kupata na kukosa, ni juhudi tuu na maarifa kama haya.

Wasalaam

Paskali
Rejea za mwandishi kuhusu nguvu za kufanya mambo
Hongera na shukrani sana Mwanabodi Paskali kwa mada nzuri..
 
Asante mkuu. Nakubali sana kuwa kuna uungu ndani yangu ila kwa kweli siamini kama mimi ni yule God. Swali langu japo linaweza kuwa nje ya Mada.. Kwa hiki unachosema ina maana tunakosea pale tunapofanya worship kwa Mungu? Je vipi kuhusu ushirika na Roho Mtakatifu? Mie nikiabudu kuna namna nahisi inayonifanya nijione one with God. Nisaidie maoni yako tafadhali
 
Bro Pascal naomba nikuulize,
Katika manifestation, je vibration ni nini? Naipataje? Maana naweza kuwa na vingine vyote ikakosekana hiyo vibration.
Pia mimi zamani kabla sijasoma haya mambo sijui ya law of attraction nilikua nikivisualize kitu kinatokea. Tangu niyasome niki visualize havitokei😆😆😆 I don't know what's wrong. So siku hizi I don't practice visualization anymore
 
Vuta kumbukumbu vizuri hiyo zamani ulikua na tabia(matendo) gani, na sasa hivi unatabia gani,

Kwasababu haya mambo yanakanuni zake, na hizo kanuni huwezi kuzitenganisha na kanuni. za Mungu, kinachotofautisha ni kwamba alie anzisha na kuita law of attraction hakutaka kuihusianisha na imani yoyote inayomuhusu Mungu. Ila kanuni ni zile zile.

Huu ni mtizamo wangu, akija mleta mada atakujibu vyema kabisa kulingana na context ya uzi wake.
 
Bro Pascal naomba nikuulize,
Katika manifestation, je vibration ni nini? Naipataje? Maana naweza kuwa na vingine vyote ikakosekana hiyo vibration.
Pia mimi zamani kabla sijasoma haya mambo sijui ya law of attraction nilikua nikivisualize kitu kinatokea. Tangu niyasome niki visualize havitokei😆😆😆 I don't know what's wrong. So siku hizi I don't practice visualization anymore
vibration = thoughts/ mawazo
 
Back
Top Bottom