Siri ya Mafanikio Kupitia Manifestation -1: Manifestation ni Nini?

Mkuu shukrani sana...

Unauwezo mkubwa sana wa kuchakata na kuwasilisha maada...
Open minded wengi tunajichanganyaga hapa kwenye imani.
kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho ni imani tuu, kuamini wewe unaweza, umeumbwa na nguvu na uwezo wa Kimungu uliomo ndani yako
 
 

Attachments

Nitasoma baaae andiko hili zuri
 
Hiki ni kitabu kwa hisani ya GoldDhahabu ,
 

Attachments

Na hizo nguvu za manifestation ndio pia zinatumiwa na watu kuwatawala wengine. Hakuna mtu awaye yeyote anayetaka ujue una nguvu. Ile kutokujua kama una nguvu ndio zinakuwa dormant na hivyo unakuwa maskini.
Wazungu ndio hii formula wanaitumia kuwatawala wengine. Wanafanya kwa ku-divert nguvu za mtu kwenye mambo yasiyo na msingi, mfano shuleni badala ya kuwafundisha watoto kuwa Wana nguvu ya kufanya kila kitu wanawafunza ziwa Victoria sijui limegunduliwa na nani wakati ni uwongo mtupu.
Mambo ni mengi lakini Asante kwa bandiko zuri
 
Ni kweli kabisa, na ndizo zinazotumiwa na wahubiri wengi wa wokovu kuwaaminisha waumini wao kuwa wao ni powerful, hivyo waumini wanammanifestia kiongozi wao na kupeleka maokoto ya sadaka wakijua ni wanamtolea Mungu, na kiukweli wanakamuliwa haswa.
P
 
Ujanja mpya wa kudanganya watu ni kwaambia hiki kitu ni kwa ajili ya open minded, na watu wa imani ni closed minded.

Mimi huwa naamini kinyume chake.

Brother Paskali nilidhani utatumia vitu nje ya dini kujenga hoja badala yake umetumia ideas za biblia za uumbaji kujenga hoja za kupuuza mambo ya imani. Hii pia ni ushahidi wa closed mindedness ya watu wanaopuuza imani. Karibu wote huwa wanatumia biblia kitabu cha imani kama pivot ya kuegemeshea hoja zao.


Ukweli ni kwamba mwanadamu aliumbwa. Pili aliumbwa na uwezo mkubwa sana ( A little lower than angel Psalms 8).

Watu wengi wa dini potoshi wanamuhamasisha mwanadamu kuwa watampa vitu qmbavyo kiukweli Mungu tayari ameshampq nq kumjengea uwezo wa kuvipata. Tulitakiwa tuwe tunaomba vitu vilivyo nje ya uwezo wetu. Hii imepelekea kuwa na watu wenye uwezo mdogo kuliko mchwa. Yaani mchwa anaweza kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa njaa wakati wasukuma wenzetu shinyangq vijijini wakivuna wanakula kila kitu ili wapewe mahindi ya msaada.

Nilichojifunza mambo mengi watu wanayotumia kupingia dini ni hayohayo ya dini na ya Mungu ambayo hata watu wa biblia hawatambui.
 
Ujanja mpya wa kudanganya watu ni kwaambia hiki kitu ni kwa ajili ya open minded, na watu wa imani ni closed minded.

Mimi huwa naamini kinyume chake.
Mkuu matunduizi, hoja za open mindedness na closed mindedness sio hoja za uongo au kuwadanganya watu, viongozi wengi wa dini huwakamata wafuasi wao kwa kuwashika minds zao kuwazuia kuwaza, ukihudhuria makanisa ya wakovu with open mind, unazishtukia kamba zote za maigizo ya uponyaji to make believe, huku closed mind wanaamini kila kitu!
Mimi ni Mkristu Mkatoliki die hard ila pia ni open minded, hivyo kuweza kutenganisha maagizo ya Mungu na maagizo ya binadamu, wale ma Kaizari wa Vatican, na kuendelea kuwa Mkatoliki nikimpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumuachia Kaizari yale ya Kaizari.
Ukweli ni kwamba mwanadamu aliumbwa. Pili aliumbwa na uwezo mkubwa sana ( A little lower than angel Psalms 8).
Its not that, binadamu aliumbwa na uwezo wa Kimungu, ana conscious, uwezo wake ni mkubwa kuliko malaika!, malaika ni mtumishi tuu wa kutumwa, hana conscious bali ni mtumwa wa Mungu.
Watu wengi wa dini potoshi wanamuhamasisha mwanadamu kuwa watampa vitu ambavyo kiukweli Mungu tayari ameshampa nq kumjengea uwezo wa kuvipata.
Hili ndio lengo la uzi huu, kumjulisha binadamu kuwa ana uwezo wa ki Mungu ndani yake.
Tulitakiwa tuwe tunaomba vitu vilivyo nje ya uwezo wetu.
Tuna uwezo wa kila kitu!, hatuna haja ya kuomba chochote kwa yeyote, bali kuutumia uwezo ulio ndani yetu kutupatia chochote tunachotaka.
Hii imepelekea kuwa na watu wenye uwezo mdogo kuliko mchwa. Yaani mchwa anaweza kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa njaa wakati wasukuma wenzetu shinyanga vijijini wakivuna wanakula kila kitu ili wapewe mahindi ya msaada.
Ni kweli
Nilichojifunza mambo mengi watu wanayotumia kupingia dini ni hayohayo ya dini na ya Mungu ambayo hata watu wa biblia hawatambui.
Hakuna anayepinga dini bali hapa ni kuwafungua watu macho, wajitambue kuwa wana uwezo wa Kimungu ndani yao, na chochote watakacho, wanauwezo wa kukipata.

P
 
Kaka yangu Pascal, unatakiwa ujue kuwa hakuna mtu kwenye hii dunia anayetaka mwenzake ajitambue. Kwa hiyo unapoweka mada kama hii hapa jukwaani tegemea ukinzani wa moja kwa moja au wa siri. Refer #26 hapo juu
 
Kaka yangu Pascal, unatakiwa ujue kuwa hakuna mtu kwenye hii dunia anayetaka mwenzake ajitambue. Kwa hiyo unapoweka mada kama hii hapa jukwaani tegemea ukinzani wa moja kwa moja au wa siri. Refer #26 hapo juu
Dini zilipaswa kuwafundisha waumini wake kujitambua ili kuwajenga kiimani, lakini its the other way round, dini zinawahadaa na nyingine zinawapumbaza kabisa, hivyo wanashinda na kukesha makanisani huku wanakamuliwa sadaka.

Huwezi amini kuna watu mpaka leo, hawaijui dhambi ya asili ni nini, wanaamini ni kumega tunda!
p
 
Dini zimekuja juzi juzi tu duniani lakini pana elimu nyingi za kale kabla ya hizi dini zikieleza mambo haya ya sheria za asili.
Do and don't do.
 
Usipotaka kuyajua maandiko bure utayajua kwa kuyalipia kwa mitume na manabii
 
Ee Bana Paskali wiki ijayo mida ya saa 👍
 
你(Haya mambo ya number 369 ili kutumia nguvu za universe ili kupata utakacho.
matumizi ya numbers ni numerology, ni kama mambo ya aastrology na palmistry ni mambo ya ubashiri, au Kiislamu shirki, hizo unazoziita nguvu za universe, sio za universe bali ziko ndani yako.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…