Man Rody
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 1,263
- 2,987
Salaam Wakuu, awali ya yote ningependa kuipongeza J.F kwa mpango huu kabambe.. bila kupoteza muda nizame moja kwa moja kwenye mada tajwa apo juu. MAFANIKIO yanaweza kuwa na maana tofauti kwa watu tofauti japo kiuhalisia jamii inatumia kipimo cha mali/fedha kama mzani wa mafanikio.
Kuna maana tofauti za mafanikio mfano kwa mlokole au Answaar watu ambao mali sio kipaumbele kwao kipimo chao cha mafanikio ni Imani yao na ukaribu kwa Mungu, au mmasai mafanikio kwake ni kuwa na ng’ombe nyingi na kadhalika.
Chanzo : Google
Hivyo maana kuu ya mafanikio ni kupata hitajio la moyo wako kwa wakati husika na kwa kiwango/idadi uliyo ridhia. Kwa mfano mwanasoka ataona amefanikiwa akifika ligi ya UEFA au LA LIGA, mwanamuziki atapima mafanikio yake kwa tuzo za GRAMMYS au watizamaji wengi wa mitandaoni. Je unaweza kua fukara mwenye mafanikio? Hadi hapa Jibu unalo wewe ndugu msomaji.
Kumekuwa na vitabu, sinema, semina nyingi sana kuhusu mafanikio na uhamasishaji juu ya fursa mbali mbali lakini ukweli ni kwamba fursa nyingi ambazo tumekua tukitangaziwa ni mbinu za watu kutengeneza fedha..wazoefu wanasema ukiona unakaribishwa kwenye fursa basi mara nyingi wewe ndie fursa kwa maana wewe ni mteja au muwezeshaji wa hiyo fursa husika.
Chanzo : Google
Sio siri kwamba kwa sasa Maisha ni magumu sana, bidhaa hazishikiki madukani na masokoni. Hali kama hii watu hutupia lawama kwa viongozi wa serikali juu ya miundombinu na sera mbovu. Ukweli mchungu ni kua hakuna wa kubadilisha matokeo maishani mwako isipokua wewe. Tukumbuke huyo kiongozi yuko madarakani kwa kuchaguliwa hivyo ni sisi ndio tulimteua. Vipi kuhusu matetemeko ya ardhi, CORONA na vita vya Ukraine na Urusi? Viongozi hawajasababisha yote haya.. Je nini kipimo cha mafanikio ya Nchi yetu ilhali tumeambiwa tumepanda kiuchumi ilhali wakati huo wananchi tuna hali mbaya na tozo zinaongezeka?
Katika malezi yetu tumeaminishwa kuelekeza nguvu kwenye elimu, kusoma mpaka chuo kikuu kisha kupata ajira jambo ambalo miaka ya hivi karibuni tunajionea wasomi wengi kuhitimu vyuo na kuongeza idadi ya warandaji mjini kwani ajira zimekua adimu na kwa kudumaa kimawazo wasomi wengi wameshindwa kubuni mipango mbadala wa kujitafutia kipato.
Chanzo : Google
Maisha ni kupanga na kuchagua.. hili naliamini kwa asilimia mia moja, chochote unachokifanya sasa hivi kina athiri muendelezo wa Maisha yako kwa mfano kula vyakula vyenye lishe bora vitarutubisha mwili wako, alikadhalika kula vyakula visivyo lishe bora utapata athari inayohusiana na hayo. Lakini pia tukumbuke siku zote njia ya mmoja haiwezi kufanana na ya mwengine ndio maana jambo moja jepesi kwa mmoja laweza kua zito sana kwa mwengine.
Kuna watu wanaamini ili afanikiwe basi ni lazima watumie njia kama utapeli, wizi wa nguvu, Uchawi na kadhalika.. kwa mapolisi na mahakimu mafanikio yao ni kumdhibiti mtu kama huyu. Hakuna maana iliyonyooka na kila mtu ataitafsiri kwa mlengwa wake. Jamii inatupa viwakilishi tofauti vya neno mafanikio na hapa ndio napalenga kwa kutoa njia pekee nayopendekeza kwako kufikia mafanikio.
Ingelikua kupata mafanikio katika Nyanja yoyote ni rahisi basi watu wote wangekua wanaishi Maisha ya raha mustarehe. NAKUSISITIZA kuendelea kutumia njia yoyote unayotumia mpaka sasa.. sipo hapa kukuambia umekua ukikosea maishani mwako na ndio maana hujafika unapotaka, Hapana mpaka leo hii kwanza nakupongeza kwa UPAMBANAJI.. nyongeza yangu ni swala moja la msingi naloliona kwa kila aliefanikiwa iwe kwa mali, dini, elimu.. kupanga na kufata RATIBA.
Mfano wa ratiba ya siku, Chanzo: Google
Ukweli mchungu binadamu wengi sana tunaishi kiholela, wachache unaowaona wamefanikiwa wanatuzidi kitu kimoja tu RATIBA na ndani ya hili neno ndio utakuta dondoo zote za wahamasishaji! Bila nidhamu huwezi fata ratiba, bila ari huwezi kufata ratiba ata siku moja. Watu wengi ratiba tunazifata kwa mazoea na sio mipaka kama inavotakiwa!
Binadamu wote tuna masaa 24 iweje mwengine awe ana uzalishaji chanya ndani ya hayo masaa, huku mwengine akiwa na hasi. Mfano mtu mmoja ni mkunga kutwa akisaidia wamama kujifungua salama, mwengine ni kibaka kutwa kwenye vilabu na sehemu za kamari akitegea kukaba watu. Hawa ni binadamu wawili waliochagua njia za kufata maishani mwao.
Chanzo : Google
Siri imejificha katika marudio ya shughuli unayofanya kila siku, ukirudia mara kwa mara kwa muda mrefu basi utaimudu kwa ufasaha. Hapa ukipanga RATIBA na ukaweza kuifata kwa ni lazima utaona mabadiliko, na hapa ndio wengi tunapofeli mfano mzuri mazoezi ya kukata uzito. Wengi tunategemea matokeo ya hapo kwa papo na ndio maana ndani ya siku chache tunakata tamaa.
Chanzo : Google
Warren Buffet, mmoja wa wawekezaji wakubwa duniani alielezea jinsi alivo panga ratiba yake ya siku na sio lazima ufate kama yeye kila kitu ila itakupa mwanga wa kuweka kila kitu katika mipango. Kingine nilichovutiwa na ratiba ya huyu mzee ni kuvunja yale masaa 24 ya siku na kila saa kua na shughuli aliopanga kufanya, je ukitathmini Maisha yako kila unalofanya sasa hivi ulipanga jana yake kwamba ungelifanya kwa muda huu?
Chanzo : Google
Kwa kumalizia nataka kusema kila binadamu ana uwezo wa ajabu na wa kipekee, kwanza kuzaliwa tu ni bahati nasibu ambayo mamilioni ya mbegu za kiume yalikua yakichuana kuingia katika mfuko wa uzazi wa mama zetu ila wewe ukafanikisha.. Chochote unachoweza fikiria kwa nadharia basi kinawezekana kiuhalisia na hakuna watu maalumu waliopendelewa ufahamu kukuzidi wewe na mimi, ukweli ni kwamba kuna watu wametuzidi mipangilio ya RATIBA na kwa sasa wamefanikiwa kwenye maeneo yao kupita sisi. TUJITAFAKARI.

Upvote
7