Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
π¦ππ₯π π¬π π πππ¦ππ
Maisha yanaweza kubadilika kwa sekunde tu, kutoka kupambania rizki mpaka kupambania uhai yaani hakuna ajuaye nyakati hizi maana kila kitu ni ndani ya dakika tu kinachukua sura mpya.
Kutoka nyumbani salama na Familia inakusubiri urejee na chochote kitu, mpaka sasa Familia inakuombea tu ubaki salama huko chini urejee na uhai pekee, kuna siku utagundua furaha ya Mwanadamu sio Pesa, ni ukweli.
Kutoka kuitwa Boss na Kibaraka wake huko chini mpaka sasa kuanza kutambuliwa nyote kama Wahanga yaani kwasasa nyote mna jina moja na hatma moja pekee katikati ya bonde la mauti na mlima wa Uhai, huenda mnapigana kusaka njia ya kuona jua tena.
Umeona maisha yalivyo? Kuna Mtu alikuwa anatamani awe na mishe tu eneo hilo, unaona maisha yalivyo? Kuna mwingine alikuwa anatamani mwenzake anaenda Mjini, lakini Allah kachora hatma ya kila Mtu. By muddy panchoπππΌππΌπ§