Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

Yericko,
Hilo la Kleist kutokuwa rais wa African Association bali katibu na la
mwanawe kutokuwa rais wa Tanganyika African Association (TAA)
sidhani kama linabadilisha historia ya mchango wa Abdul na baba
yake katika uhuru wa Tanganyika.

Muhimu ni kuwa maisha ya Kleist yamehifadhiwa kwenye kitabu:
Modern Tanzanians (1973)na kwenye Dictionary of African Biography
(DAB) (2011) na maisha ya mwanae ndiyo kitabu nimeandika na ni
mashuhuri kwenye vyuo vingi Ulaya na Marekani toka kilipochapwa
London 1998.

Kitabu hiki sasa kinakwenda toleo la nne Kiswahili na toleo la tatu
Kiingereza.

Sasa kwa nini Abdul hakuwa rais wa TAA 1950 nimejaribu kueleza
na nikakuambia kuwa kutokea 1951 hadi 1953 alikuwa katibu na
akakaimu na nafasi ya rais wa TAA na chama kilipata mafanikio
makubwa sana.

Tunaweza kuanzia hapa safari yetu nikakurejesha hadi Nansio mwaka
1953 kwa Hamza Kibwana Mwapachu, Abdulwahid alipokwenda
kumtaka ushauri kuhusu Nyerere.

Sasa Yericko hebu jiulize kwa nini Abdul na Ali Mwinyi Tambwe
walifunga safari kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kisha wakavuka
Lake Victoria hadi Nansio kwenda kupata kauli ya Hamza Mwapachu
ilhali Hamza Mwapachu hana nafasi yoyote ya uongozi katika TAA?

Nakuuliza swali hili kwa kuwa nakuona wewe umeshughulishwa
sana na nafasi ya urais katika TAA ingawa nimekueleza kuwa kwa
nyakati zile mtu hagombei uongozi kama ilivyo siku hizi.

Wakati ule katika dimbwi la ukoloni uongozi wa chama cha siasa
ilikuwa ni kubeba majukumu mazito sana na ya hatari.

Kiongozi alitazamwa kwanza katika kukisaidia chama kwa fedha
kutoka mfukoni kwake achilia hiyo hatari ya kufungwa jela.

Abdul Sykes alikuwa kijana wa kujiweza sana kifedha na hakika
alitoa fedha nyingi sana mfukoni kwake kuijenga TAA na baadae
TANU.

Turudi kwa Hamza Mwapachu.

Hamza Mwapachu ana historia ya pekee katika historia ya ukombozi
wa Tanganyika.

Dr. Kyaruzi alipatapo kusema kumwambia mmoja wa watoto wa
Mwapachu kuwa, "Kama si mipango aliyoweka baba yako na Abdul
Sykes
Tanganyika isingepeta uhuru mwaka wa 1961."

Jiulize kwa nini Nyerere alipojiuzulu ualimu alikwenda kuishi nyumbani
kwa Abdu Sykes wakati ule Abdul hana nafasi yoyote ya uongozi
katika TANU?

Yericko yapo mengi sana katika historia ya nchi yetu wewe huyajui.
Tuagane na Hamza Mwapachu.

Baada ya uhuru Hamza alikuwa Dar es Salaam lakini siku hizo
alikuwa mgonjwa.

Wakati ule Bunge likikutana Karimjee Hall.

Hamza alikuwa akija pale Bungeni akiwa kwenye "wheelchair,"
akifuatilia mijadala yote mle ndani.

Na Hamza hakuwa mbunge.
Nyerere akataka kumteua awe balozi Uingereza.

Hamza akakataa nafasi ile na Nyerere badala yake akamteua
Kassanga Tumbo.

Hebu hangaisha ubongo wako Yericko jiulize kwa nini Hamza
alikataa uteuzi ule?

Naamini umefadika na darsa hii.
Kejeli hapa si pake.

Jitahidi uwe na adabu lau ya kuvalia nguo.
Usicheze na Abdul Sykes Mungu alimjaalia uwezo mkubwa sana.

Hiyo 1953 akihangaika na TAA na kuunda TANU tayari mfukoni ana
barua ya kujiunga na Princeton University, New Jersey.
 

Yericko Nyerere,
Nimekuweka katika blog yangu wasomaji wangu wangependa kumsikiza
mtoto wa Baba wa Taifa anavyoielewa historia ya baba yake katika TANU
na uhuru wa Tanganyika:

Mohamed Said: KUTOKA JF: HAMZA KIBWANA MWAPACHU, ABDULWAHID KLEIST SYKES NA JULIUS KAMBARAGE NYERERE
 
Mkuu Yericko asante kwa hii kitu, iandikie kitabu.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…