Siri ya Marekani kurudia kurudia kauli ya njama ya “virusi vya Corona kuanzia maabara Wuhan”

Siri ya Marekani kurudia kurudia kauli ya njama ya “virusi vya Corona kuanzia maabara Wuhan”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111286076269.jpg

Wakati juhudi za kupambana na janga la COVID-19 zinaendelea kwa ushirikiano kote duniani, wanasiasa na vyombo vya habari vya Marekani wamejitahidi kuzusha kauli isiyo na msingi ya “virusi vya Corona kuanzia maabara Wuhan”. Kumekuwa na swali la kwa nini wana uraibu wa kufanya hivyo, bila kujali madhara ya hatua hiyo kwa uhusiano kati ya China na Marekani na wazo la “jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja”.

Wakati Marekani inajikwamua kwenye hali mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona, kuna ukweli unaohitajika kufuatiliwa. China ina watu zaidi ya bilioni 1.4, na idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa huu haikufikia elfu 5, na pia ilifanikiwa kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo ndani ya miezi mitatu; lakini Marekani yenye idadi ndogo ya watu ikilinganishwa na ya China, watu laki 6.2 wamekufa kwa ugonjwa huo na nchi hiyo haikufanikiwa kuudhibiti hadi baada ya mwaka mmoja na nusu kupita. Ni kwa nini kuna tofauti kubwa namna hiyo? Wakati China imedhibiti kwa ufanisi kuenea kwa virusi, kwa nini Marekani inaongoza duniani kwa idadi kubwa za watu walioambukizwa na waliokufa? Ni wazi kuwa wanasiasa na vyombo vya habari vya Marekani hawapendi kujibu maswali haya, na ila tu wanaangalia kwenye chanzo cha virusi, swali ambalo jibu la kuridhisha kila mtu haliwezi kupatikana ndani ya muda mfupi, lakini kufanya hivyo kunaweza kusaidia kuhamishia kwa China lawama zinazopaswa kubebwa na wanasiasa wa Marekani kwa kushindwa kudhibiti ugonjwa huo, huu ni mkakati wao.

Je, tofauti na China, kwa nini Marekani ikiwa nchi inayoongoza duniani kwa nguvu ya jumla imeshindwa kabisa mbele ya ugonjwa huo? Sababu ya kimsingi ni kuwa eti “demokrasia ya Marekani” haifanyi kazi tena mbele ya janga la ugonjwa huo. China imekuwa ikichukulia afya ya umma na haki ya watu kuishi kwa afya kama ni jambo la kipaumbele katika sera ya taifa na haki za kibinadamu za kimsingi; lakini nchini Marekani, afya, matibabu na dawa vyote ni bidhaa, na mfumo wa huduma za afya haulengi kukidhi mahitaji ya watu, bali ni mgongano kati ya vyama tofauti, na nyenzo ya kujipatia pesa kwa hospitali, kampuni za dawa na kampuni za bima. Marekani haiwezi kuhamasisha nguvu za jamii nzima kuzuia na kudhibiti kuenea kwa virusi.

Kwa hivyo tofauti hiyo ya kimfumo ni kubwa, kiasi cha wanasiasa na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu wenye faidi nchini Marekani kushindwa kukabili, sembuse kushughulikia jambo hilo. Hawawezi kuzungumzia uzoefu wa China, lakini wanatumia nguvu zote kuhamisha lawama kwa China. Marekani inapenda kuuita mfumo wake wa siasa kuwa demokrasia, lakini utaratibu wa uchaguzi unaoongozwa kwa pesa, kampuni na matajiri unawezaje kuchagua demokrasia halisi na ya kweli?

Kwa undani, Marekani imekuwa nguvu ya uongozi duniani kwa muda mrefu. Kwa hivyo, kwa baadhi ya wamarekani, kuinuka kwa China ni jambo baya, na kama China inapata neema zaidi na kuonesha umuhimu mkubwa zaidi, hakika ina maana kuwa Marekani haitakuwa na neema na kupoteza nafasi yake ya uongozi. Wanataka kuendelea kuwa kiongozi, sio kwa Marekani, bali kwa dunia nzima. Hii ndio sababu wanaendelea na msimamo wa uhasama dhidi ya China, kutoa kauli ya njama ya “virusi vya Corona kuanzia maabara Wuhan”, na pia ni sera ya kujinufaisha wao tu ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu na nchi za magharibi. Wakati Joe Biden alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani, watu walifikiri ataachana na sera ya uhasama dhidi China tofauti na jinsi alivyofanya mtangulizi wake. Lakini kwa hali ya sasa, matumaini haya hayakutokea. Hali halisi ni kuwa sera ya uhasama dhidi ya China ilianza tangu mwaka 2011, ambapo serikali iliyoongozwa na Barack Obama ilitangaza mkakati wa “kurudi Asia tena” unaoilenga China.

China imesisitiza mara kwa mara umuhimu wa wazo la “jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja” katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona. Dunia hii ni ya watu wote, na nchi mbalimbali zinatakiwa kufanya juhudi ili kuboresha maisha ya kila mtu. Ushawishi wa China kuongezeka hakumaanishi kuwa Marekani haiwezi kufuata njia yake ya jadi. Kadri Umoja wa Ulaya unavyopata maendeleo, bara hilo pia litaonesha umuhimu wake katika kujenga dunia nzuri ya baadaye. Je, kwa nini Marekani haiwezi kuachana na mambo ya kizamani? Kwa nini inakataa kutafuta njia ya kutafuta maendeleo itakayowanufaisha kwa pamoja watu wa China, watu wa Marekani, watu wa Ulaya pamoja na watu wa Afrika, India na Latin Amerika?
 
Back
Top Bottom