Siri ya mizunguko ya asili, nishati, mtetemo na masafa ya ulimwengu

Siri ya mizunguko ya asili, nishati, mtetemo na masafa ya ulimwengu

img_20230225_110821-jpg.3109652

Je, umewahi jiuliza imekuwaje vitu tofauti vya asili vinakuwa na umbo au muundo unao fanana? Sababu ni nini? Je Asili imetokea kama coincidence? Twende sambamba...

Picha uzionazo hapo juu zinaonyesha miundo ya mviringo na mifumo inayopatikana katika asili, kuanzia maganda ya konokono na galaksi hadi alama za vidole na ukuaji wa mimea na viumbe. Miundo hii inaweza kufasiriwa kama nyenzo za nishati ya msingi, mtetemo, na masafa yanayoongoza maisha na ulimwengu wote.
(Energy, Frequency and vibration)

- Nishati (Energy )
Kila kitu katika ulimwengu kinaundwa na nishati au chanzo, Mfano wa mviringo huo unaashiria mtiririko wa kudumu wa nguvu za uhai au "nishati ya ulimwengu," kutoka kiwango kidogo (alama za vidole) hadi kiwango kikubwa (galaksi). Hii Inawakilisha uumbaji mmoja na upanuzi, na asili ya mzunguko wa maisha. Ili vitu vifanane, lazima chanzo cha nishati kiwe kimoja.

- Mtetemo (Vibration)
Mtetemo unahusu kasi ambayo nishati husafiri. Kila kiumbe hai na kisicho hai kina mtetemo wake wa kipekee. Mizunguko inayopatikana mara kwa mara katika asili inashiria upatanisho na mtetemo wa msingi wa ulimwengu, ikionesha kwamba vitu vyote vimeunganishwa katika mtetemo mmoja.

- Masafa (Frequency)
Kama kipimo cha mtetemo, masafa yanaweza kuonekana katika asili ya kurudiarudia na ulinganifu, Iwe ni ukuaji wa mmea, maendeleo ya kiini husika, au uundaji wa kiasili, kila kitu kinaathiriwa na mitetemeko ya kimsingi au masafa ambayo yanaumba mfumo mmoja wa maisha.

Katika engo ya kiroho (spirituality) picha hizi zinawakilisha jiometri takatifu ya maisha, zikionyesha jinsi nishati, mtetemo, na masafa yanavyojitokeza katika maumbo yanayo fanana na kuonyesha umoja wa uumbaji. Hii ni ishara kwamba kazi ya Uumbaji imefanywa na Mungu mmoja, kwa kipimo kimoja chenye usahihi na utakatifu.

“If you want to find the secrets of the universe, think in terms of energy, frequency, and vibration."
- Nikola Tesla

Picha zenye vitu na maumbo mengine ambayo pia yana Energy, Vibration na frequency Moja.👇

Pia soma: The flow of creative Energy, Aura and Emotions
Maada nzuri sana
 
Labda mimi ndio ningepaswa kukuuliza ilikuaje ukawa theist wakati kila mtu alizaliwa ni atheist?
Common way ni mtu kuzaliwa kakuta mfumo na anaendeleza lakini kuna hatua unafika ukomavu wa akili unaweza changanua mwenyewe kama unafata dini sahihi ndo mana watu wanabadilisha. Je ulibadilisha au ulikuta?

Mfano uko peke yako jangwani umetembea kwa umbali mrefu sana bila kuona mtu ghafla unaona coin au chupa kwenye mchanga, fikra ya kwanza utasema mtu aliiacha hapo mana unajua ni kitu hakiwezi kujitengeneza kamwe wala kujifikisha apo.

Kwa maoni yako uliumbwaje mkuu mana kila kilichopo kina muumbaji (Creator) si ndio, yani genesis ya binadam nn.
 
Kumbe na Huyo Mungu nae ana muumbaji?
 
Hii ntaielezea kihistoria ukichunguza historia ya mataifa yote kuna stage kote zinafanana yaan hapa tulipo sisi wakenya wqshapita na namna tutajichomoa ni ile ile na iko hivo kila mahali
 
Hii ntaielezea kihistoria ukichunguza historia ya mataifa yote kuna stage kote zinafanana yaan hapa tulipo sisi wakenya wqshapita na namna tutajichomoa ni ile ile na iko hivo kila mahali
Vitu na mambo mengi sana yanafanana, hii ni ishara kwamba sisi wote ni wamoja, chanzo kimoja na tuna muelekeo mmoja.
 
Sherehe au Tafrija ya kumpokea Tena Boi yai uraiani itafanyika wapi jioni ya Leo?
 
Labda mimi ndio ningepaswa kukuuliza ilikuaje ukawa theist wakati kila mtu alizaliwa ni atheist?
Hakuna mtu atheist duniani - watu mnajiita hivo mkifanya reference ya ubishi kwa uwepo wa Mungu anayesemwa sana au anayetambulika sana - huyu Mungu wa Wakristo, Waislam n.k
Lkn kwa ndani kuna vitu mnaviamini - hata kuamini katika nothing - kwamba nothing inapush kila kitu tayari ni imani - Hakuna mwanadamu ambaye haamini katika -u - superbeing wowote - HAYUPO na ndo maana hata kabla ya Wazungu na Waarabu kutuletea dini za kisasa au utaratibu wa kisasa wa kumuabudu Mungu...mababu tayari walikuwa na utaratibu wao na imani zao kuhusu hiyo nguvu..
Thus wote tunatambua kuna kitu kina - nguvu kipo - tunabishana ni kitu gani au nguvu gani tu hapo ndo hatuelewani: Mwanadamu na curiosity yake hawezi kutulia kamwe - hata huo ubishi wa atheism ni katika kutafuta ukweli.
 
Kwamba ?
 
Back
Top Bottom