Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Mkopo Tanzania uliopata huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26.
Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama wasio-wazalendo wanavyopotosha.
Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu.
- Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020);
- mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025).
- mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028)
Maana yake ni kwamba , 2024 tumechukua Mkopo, 2060 ndio tutaanza kulipa na 2064 tuwe tumemaliza.
Rais atakayekuja kulipa huu mkopo Yupe Darasa la Sita shule ya Msingi, na waziri Fedha wa wakati huo huenda hajazaliwa.
Wazungu wanaona mbali kuliko Tai, wanakupa mkopo wa muda mrefu, wanakopesha nchi tofauti tofauti na marejesho miaka tofauti tofauti maana yake wanawahakikishia watoto wao, wajukuu zao na vitukuu vyao hata visipofanya kazi, hata wakiinhgia vita na Korea kaskazini kwa miaka 20 mfulilizo bado wana maokoto toka nchi zilizokopeshwa.
WANYONGE WANAWAZA ILA HAWASEMI HAYA :-
Viongozi/Marais 48 Korea-Africa Summit. Kwanini wanakubali kuitwa na mtu mmoja tu wakati sisi tuna umoja wa Afrika, huyo aliyewaita si angeweza kuja kwenye makao makuu ya African Union?