matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Kama kuna hatari unaweza kumsababishia ndugu, rafiki, kiongozi au yeyote unayemuhusudu ni kumsifia na kumtegemea kupitiliza.
Mungu mwenye wivu huwa anawasaidia wanadamu wanaowategemea kupitiliza wenzao tena kuwapa sifa kinafiki au kihalali kwa kuwapumzisha makaburini mapema wategemewa hao.
Hii ndio sababu kuna malalamiko mengi mbona huyu mpendwa, mchungaji, kiongozi, ndugu amendoka mapema jamani. Tena wengine wanalaumu kwa nini asingeondoka flani ambaya anaonekana hana faida?
Mungu huwa anataka kuwafundisha wanadamu wajue upumbavu wao wa kumtegemea na kumpa sifa za kiungu binadamu ambaye ni kiumbe wa mpito, maisha yake ni kama majani hunyauka ma kusinyaa muda wowote. Huwa anatumia hilo tukio kama funguo ya kiakili na kiroho kuwa Yupo wa kutegemewa halisi ambaye hapatikani na mauti.
Lakini usugu na ukichwangumu wa watu umepelekea kuendelea kuabudu sanamu na mawazo ya maiti hao kama mbadala wa kitokuwepo kwao. Dini nyingi za jadi,kiislam,Kibudha/Hindu kikristo zinaabudu sanamu za mawazo na mbao/chuma za waliwahusudu.
Hili lilimpata Isaya, Alimuelewa Mungu vizuri baada ya Mjomba wake Mfalme uzia kuwa amefariki. ISAYA 6.
Hili lilimpata Mwanasiasa Herode kwa kufia jukwaani na kukumbiwa na wasifiaji wake.
Hili lilimpata Bibi yangu mmoja aliyepata strock kwa Mungu kumchukua mtoto wake tegemezi na aliyesifiwa kama Mungu mpaji. Baadae bibi huyo hiyo Strock ikamuondoa. Hakukubaliana ma maamuzi ya Mungu.
UFANYE NINI SASA.
Usipende kuwapa sifa watu na utukufu wa kiungu uliopitiliza. Hata kama ni kinafiki utawasababishia matatizo kama wao hawatakuwa na hekima ya kuzikwepa sifa hizo.
Usipende kutaka kubugia kila sifa na utukufu unaopewa na watoto, wafuasi, wafanyakazi wenza, au ukoo. Zikizidi zitakuondoa.
Kuwa mnyenyekevu.
No hilo tu