Siri za Miujiza Feki: Jinsi Manabii na wachungaji Wanavyowatapeli waumini wao.

Siri za Miujiza Feki: Jinsi Manabii na wachungaji Wanavyowatapeli waumini wao.

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Hivi unajua kuwa unapoona mtu anatapika "nyoka" kanisani au kiwete anatembea ghafla, mara nyingi hushuhudii nguvu za Mungu, bali unatazama mchezo wa kuigiza uliosukwa kwa ustadi na nguvu za giza (Occultism)? Je, unajua kuwa sekta hii imekuwa biashara kubwa inayovuna mabilioni kwa kutumia maagano ya siri na saikolojia ya umati?

Ule muujiza wa kipofu kuona ghafla au kilema kutupa magongo mara nyingi ni biashara ya mtaji na faida iliyopangwa nyuma ya pazia.
Waigizaji wa Kukodi: Kuna mtandao mkubwa wa watu maskini wanaolipwa fedha kusafiri mikoani kufanya kazi ya "kuigiza kupona." Kiwete anayepona leo Mwanza, ndio atakuwa bubu anayefumbuliwa ulimi kesho kule Mbeya.

Kupitia sauti ya mamlaka na muziki mzito wa keyboard wenye midundo maalum (Ambient pads), akili za waumini huingia kwenye hali ya kupoteza fahamu ya muda (Trance state). Mtu anasukumwa kidogo tu na walinzi, anadondoka akiamini ni upako, kumbe ni saikolojia ya umati (Crowd psychology).

Huu si mchezo wa kiakili tu; kuna mahali ushirikina na nguvu za giza zinahusika kwa 100% ili kupata utajiri na mamlaka.
Kusafiri Kupata "Dawa": Manabii wengi feki wanasafiri hadi misitu ya mbali nje ya nchi kufanya matambiko mazito. Huko wanapewa vitu kama pete au mafuta yaliyochanganywa na nguvu za kishirikina (Occult items) ili kupata sumaku ya kuvuta umati.
Wizi wa Bahati: Kupitia maagano haya ya siri, miujiza ile inafanya kazi kama mtego. Badala ya kukupa baraka, nabii anavuta nyota, afya, na bahati za waumini na kuzihamishia kwake ili azidi kuwa tajiri, huku waumini wakizidi kuwa maskini na tegemezi. Kama huamini hapa muulize Yule mwimbaji wa nyimbo za injili aliyepewa gari na yule Nabii.

Hapa ndipo akili inapotakiwa kuchemka na kuhoji kwa kina:

Kama miujiza hii ni ya kweli na inatoka kwa Mungu anayejali maskini, kwanini manabii hawa hawaendi wodini Hospitali ya Bugando au Muhimbili kuwaponya wagonjwa wote wa saratani na figo bure, badala ya kusubiri watu waliolipa "kiingilio cha VIP" kwenye kumbi zao za mikutano? Inakuwaje nchi yenye makanisa mengi ya miujiza ndio inayozidi kuwa na umaskini na ujinga wa kiwango cha juu?

Nani wa kulaumiwa hapa: ni huyu "nabii" mjanja anayetumia shida zako kupiga pesa, au ni wewe uliyetawaliwa na uvivu wa kufanya kazi na kutaka miujiza ya haraka ya kupata utajiri kwenye sahani ya dhahabu?
 

Attachments

  • FB_IMG_1782726140730.jpg
    FB_IMG_1782726140730.jpg
    85.2 KB · Views: 19
Back
Top Bottom