displayname
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 1,972
- 1,085
Mkuu Hao wanaotengeneza Dawa za (product za Forever) ni sawa sawa na Dawa za kizungu vidonge. Ukiona Dawa ya Mitishamba imeandikwa hivi (date of production and Expire Date) ujuwa hiyo dawa ina sumu ndani yake Dawa nzuri ni dawa ya mitishamba iliyokuwa haina hayo maandishi.Iweje Mti uwe na tarehe ya mwisho wa kutumia? tangu lini Chungwa au embe au kitunguu saumu kikawa na Tarehe ya mwisho kutumika? Ukiona chungwa au Embe au kitunguu Saumu kina tarehe ya mwisho kutumika ujuwe hayo sio matunda Orignal ni matunda feki.
View attachment 372704 View attachment 372705
Angalia hapo Herufi za MFG: Tarehe 04/09/2014 hiyo ndio Tarehe iliyo tengenezwa hiyo Cheese (jubini) na Tarehe ya mwisho ya kutotumika ni hii hapa Tarehe 04/09/2017 sasa hicho chakula ni feki kwa mujibu wa hizo tarehe hakifai kuliwa kina sumu ndani yake chakula kizuri kisicho kuwa na Tarehe za aina yoyote ile. Na angalia hilo Yai linatumika mwaka 2015? kwanini Yai liwe pia na Tarehe ya mwisho ya kulitumia? ukiona hivyo Yai lina tarehe ya mwisho kulitumia ujuwe ni Yai feki sio yai la kuku wa kienyeji.
Ahsante Mkuu...ila mashaka yangu kidogo vitu visivyo feki huwa vinapitwa na wakati kwamaana ya kuharibika pia... mfano Yai ambalo halina maandishii tufanye Yai kuku wa kienyeji...lisipo tumika kwa muda mrefu linakuwa halifai tena kwa matumizi ya binadamu. Vivyo hivyo kwa vitunguu swaumu, embe, chungwa na matunda yeyote yale....hupitwa na muda na kuoza ama kuharibika. Tofauti yao ni moja tu kibandiko cha tarehe ya mwisho. Vingine vina mwisho wa matumizi japo havina tarehe.