malichandix
Member
- Aug 15, 2022
- 5
- 1
"SIRI ZILIZOJIFICHA KWA KIJANA MSOMI"
KIJANA:
Wengi wetu tunamfahamu kama binadamu mwenye jinsia ya Kike au kiume, na alie na umri wa kuanzia miaka 18 mpaka 45.
KIJANA MSOMI:
Hapa tunamchukulia kama kijana mwenye elimu ya chuo na aliyetoka sehemu ya mbali(anatokea sehemu/
Mikoa/Vijiji viilivyoshamiri sana kilimo na hakuna uhaba wa Ardhi kama vile; Mpanda,
Sumbawanga, Kigoma,nk) na kwenda kusomea kwenye miji au majiji makubwa kama Daressalaam (sehemu zisizoshamiri kilimo na Kuna uhaba mkubwa wa Ardhi"Land scarcity"). Kwasababu, Ardhi hiyo Kwa kiasi kikubwa imekaliwa au imechukuliwa na watu "imekuwa occupied".
ARDHI;
Ni eneo la chini ambalo hutumika Kwa matumizi mbalimbali ie.Kilimo, usafirishaji, ujenzi (wanyumba za kuishi, za viwanda, taasisi nk). Ardhi pia inachukuliwa na watu kama, zawadi ya asili na mali ya kipekee isiyo hamishika na inayoweza kumilikiwa na mtu yeyote yule bila kujali jinsia, wadhifa wa mtu, elimu ya mtu, lakini pia uchumi wa mtu. Kwasababu, Ardhi hiyohiyo inaweza kumilikiwa kwa kupitia njia nyingi kwamfano; kwa kununua, kurithi nk.
Lakini pia, kama ilivyofafanuliwa kwenye fungu la 2 la Sheria ya Ardhi namba nne (4) ya 1999, "Ardhi inajumuisha uso wa dunia na chini ya uso wa dunia, na vitu vyoote isipokuwa madini na mafuta(petroli) ambavyo ni sehemu ya uso wadunia au chini yake, vitu vinavyoota juu yake, majengo na vyote vilivyopo juu ya ardhi ambavyo haviwezi kuhamishika".
KIJANA MSOMI NA ARDHI.
Licha ya kuwa, Ardhi inachukuliwa kama kitu cha thamani sana na inaweza kutumika katika kazi au matumizi mbalimbali na kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja, jamii fulani au nchi nzima kwa ujumla. Lakini, Ardhi hiyohiyo imekuwa ikisahaurika (haipewi kipaumbele sana na vijana walio wengi hasa vijana wasomi) kama ni jenzo na fursa muhimu kwao ya kujiajiri na inayoweza kuwawezesha kujikwamua kimaisha. Na imekuwa ikichukuliwa kama mbadala wa mwisho kabisa pale
wanapokosa ajira au kushindwa kujikwamua "kutoboa" kimaisha wanapokuwa mijini baada ya kumaliza masomo yao.
Yapo mambo mawili(2)muhimu yanayo wakumba vijana wasomi juu ya Ardhi:-
i. Wasomi wengi wamekuwa wakimaliza vyuo na kubaki mijini(miji/majiji makubwa) na kutotaka kabisa kurudi makwao/vijijini kwao au katika mikoa yao ili kwenda kuendeleza kazi walizokuwa au wanazozifanya wazazi/walezi wao. Kwa kisingizio kwamba, wanabaki kutafuta Ajira "michongo" na huko walikotoka
hamna fursa nyingine zaidi ya kilimo. Ambacho maranyingi huchukua muda mrefu mpaka kupata mafanikio. Nilijaribu kuzungumza na mmoja wa vijana
wasomi aliemaliza masomo yake ya chuo kikuu mwaka 2019, na akabaki Daressalaam, alisema yafuatayo:-
''Nilipomaliza chuo sikutamani kabisa kurudi nyumbani mapema, nilitamani nitafute kazi
kwanza ili niweze kujikwamua kimaisha. Sikutaka kurudi kwasababu, kule bado
hakujachangamka na hamna fursa nyingi zaidi ya kulima tu kama wazazi wanavyofanya.
Hatahivyo, kilimo huchukua muda mrefu sana mpaka kupata faida ambapo huo muda Kwa huku ningekuwa nimepata pesa kwa muda mfupi kwa kujishikiza tu mahali"
ii. Pia wasomi wengi wamekuwa hawapendi kurudi mikoani kwao ili kwenda kuendeleza kazi za wazazi wao, kama ilivyo katika nchi za wenzetu weupe zilizoendelea. Wamekuwa wakiamini kuwa, mafanikio yanapatikana mijini (kwenye miji/majiji makubwa) tu na wamekuwa na fikra kwamba inakuwa ni vigumu mno kufanikiwa ukirudi ulikotoka na ukafanya kazi wanazozifanya wazazi au walezi wako.
SIRI NYINGI ZISIZOJULIKANA AMBAZO NI SULUHU KATIKA MAONO YA VIJANA WASOMI:
*Kutokana na sababu mbili zilizoorodheshwa hapo juu, vijana wengi wanaamini kwamba kutokurudi makwao ndio kunaweza kuwafanya wakafanikiwa kwa urahisi na inakuwa vigumu kwao kurudi na kufanya kazi wanazozifanya wanzazi/walezi wao kwasababu wanaamini kufanikiwa inakuwa ni vigumu.
SULUHU:-
Itakuwa ni jambo jema sana, kama vijana woote wasomi hasa
wasio na ajira mjini wakirudi makwao/vijijini/mikoani kwao nakwenda kuendeleza kazi za wazazi wao, ambazo zimekuwa zikionekana hazina manufaa tena, hasa wakiitumia elimu yao katika kazi hizo. Kwasababu, inaaminika kuwa wazazi wa wasomi wengi wamekuwa wakifanya kazi zisizo za thamani mbele ya matajiri na wasomi wengi. Ambazo maranyingi huchukuliwa au huonekana Kama kazi za walala hoi ikiwemo; uvuvi, ukulima
mdogomdogo, ufugaji nk.
Ni wazi kwamba, vijana hao wakiitumia elimu waliyonayo kwenye kazi za wazazi wao kama, kutumia elimu walizonazo katika kuwekeza kwenye kilimo. Kwamfano; kutumia nyenzo za kisasa badala ya jembe la mkono katika kilimo, kulima kilimo cha umwagiliaji kinachochukua kipindi kifupi bila kusubiri msimu wamvua. Hivohivo, hata kwenye uvuvi na ufugaji. Hiyo inaweza ikawa njia sahihi mno ya kujiinua kiuchumi kuliko kubaki kwenye miji ya watu na kuisubiri ajira.
*Lakini pia mbali na kurudi makwao kuendeleza kaziza wazazi/walezi wao, hao hao vijana wamekuwa wakiitazama "ARDHI" Kwa namna tofauti ambayo ni hasi. Kwamba wakirudi hamna fursa nyingine zaidi ya Ardhi iliyopo kwaajil ya "KILIMO" tu na inakuwa ngumu "kutoboa"kupitia Ardhi ya kilimo.
Tunaweza tukafikiria, wazazi wetu waliacha maeneo mengi kwaaajili ya KILIMO. Kwasababushughuri yao kubwa ya kiuchumi ilikuwa ni kilimo, lakini tatizo linakuja pale watoto(wasomi)hao, hawaioni thamani ya Ardhi na wanaiona Kwa sura moja tu(kilimo tu)na wengi wao huishia kuiuza Ardhi waliyoachiwa
na wazazi wao.
SULUHU:-
Ni vizuri kama vijana wasomi wakaitazama Ardhi kwa namna
tofauti ambayo ni chanya zaidi. Kwa kutamani kuwekeza kwenye Ardhi, wakiwa naimani kwamba Ardhi inazo fursa nyingi mno zaidi ya kilimo. Pia,
isiwe mbadala wa mwisho kwao bali ipewe kipaumbele kwa kuzitambua
fursa nyingi zilizopo kwenye Ardhi na sio "KILIMO" tu kama wanavyoamini.
Zipo fursa nyingi mno kama vijana wasomi wakibadili fikra zao na kuwekeza kwenye Ardhi, zifuatazo ni baathi ya fursa hizo;-
i. Badala ya kwenda ziwani/mtoni kufanya uvuvi wa samaki, Ardhi inaweza kutumiwa katika ujenzi wa bwawa la samaki nyumbani na kufanya kilimo cha samaki, tena kwa kuanza na ufugaji wa kienyeji kabisa ie;kutengeneza
bwawa la kienyeji ambalo litatumia gharama ndogo mno hasa kwa vijana wasio na mtaji au mtaji mkubwa. Kama inavyoonesha kwenye picha
ifuatayo;-
Chanzo:MuugwanaBLOG.
ii.Ardhi pia inaweza tumika kwaajili ya kufugia wanyama mbalimbali kama ng'ombe, mbuzi, sungura, nguruwe nk. Ambapo baada ya muda fulani kijana anaweza akafaidika kupitia huo ufugaji.
Chanzo: Taifa leo

iii. "KIJANA" pia anaweza akafanya biashara ya Ardhi kwa kununua kipande au vipande vya Ardhi, kwa maana ya mashamba na viwanja(hasa vilivyo pimwa). Akakaa navyo kwa muda na kuviuza baada ya muda fulani
ambapo bei itakuwa imepanda. Kwasababu, Ardhi huwa inapanda thamani kadri
muda unavyokwenda. Hata siku moja Ardhi haikuwai kushuka thamani.
Chanzo: Wikipedia
iv. Ardhi hiyohiyo inaweza kutumiwa katika ujenzi wa nyumba za kupangisha (nyumba za makazi nk) au nyumba za kuuza kulingana na mtaji wa mtu.
Chanzo: PinClipart
HITIMISHO:
Vijana ndio nguzo na tegemeo la taifa la kesho. Kwaio,ni vizuri
tukaithamini zawadi ya asili(Ardhi)tuliyopewa na Mwenyezi Mungu na kuweza kubadilimtazamo wetu juu ya Ardhi. Kwamba, Ardhi ni mbadala wa mwisho. Lakini pia tuwe kama
nchi za wenzetu wanaoweza kuwarithisha watoto wao vipaji
na kazi wanazozifanya. Kwaio vijana inatakiwa tuzitazame kazi za wazazi wetu kama fursa na sio kuzitazama kwa namna
mbaya isiyoweza kuleta maendeleo.
"KAMA VIJANA WOTE TUKIKIMBILIA
KUISHI NA KUFANYA KAZI KWENYE MIJI MIKUBWA ILIYOKWISHA KUENDELEA TAYARI, NANI ATAENDELEZA KIJIJINI AU MKOANI KWENU?.

Upvote
2