Pamoja na kwamba siujui huu mchakato ulivyokwenda lakini kwa maelezo ya Baraka Kizuguto naona hajaweka suala hili vizuri na kuna kitu kipya ameongeza hapa kwamba
Iliyopitisha Kanuni Hii ni Kamati ya Utendaji sababu ina mandate na kumbe si Bodi ya Ligi
Kwamba wadau walioridhia wapo wengi na akasema dhana ya wadau wa mpira ni pana sana
Kwamba Kanuni za Ligi zinaweza kupitishwa na mdau yoyote mradi awe wa mpira au chombo maalum?
anajiuliza ni kwa nini ni Yanga tu wanaokomalia suala hili, mchezo dhidi ya Standi hawakukata rufaa kadhalika mchezo dhidi ya Prison Yanga hawakukata rufaa hivyo wanachodai ni malalamiko tu
kwamba mabadiliko ya kanuni hiyo yalienda sambamba na uundwaji wa chombo cha kuendesha ligi ambacho kimeshatoa adhabu kwa wachezaji kama akina Aggrey Mrris na Juma Said Nyoso na kwa nini timu zisilalamikie adhabu hizo