Uchaguzi 2020 Sirro: Msitumie shida za vijana kama sababu ya kuwatumia kuanzisha fujo

Uchaguzi 2020 Sirro: Msitumie shida za vijana kama sababu ya kuwatumia kuanzisha fujo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya baadhi ya wanasiasa nchini kuacha kuwatumia vibaya wananchi hususan vijana hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2020 na kuwaingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.

IGP Sirro amesema hayo akiwa Musoma mkoani Mara kwenye kikao kilichowahusisha viongozi wa kisiasa wakiwemo wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu waliopo mkoani humo ambapo aliwataka wagombea hao kutumia majukwaa ya kampeni kuhubiri amani.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Bunda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ester Bulaya, amesema katika kipindi hiki cha wiki mbili kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu lazima vyama vishikamane na kuwa makini sambamba na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri.
 
Kila siku anaimba mapambio hayo hayo wakati kutimiza wajibu wao kama pilisi hawataki, msafara wa Lissu umeshambuliwa huko Chato halafu bado anaongea pumba tu bila aibu yoyote, Sirro amejisahau sana ameshakuwa mwanasiasa.

Lissu amefunga barabara huko hataki kusikia tena huu ujinga wako.
 
Kama hajasema hatua gani itachukuliwa dhidi ya wale polisi wa nyamongo basi waseme ni hatua gani itachukuliwa
 
Tunashukuru Mungu uchaguzi mpaka hatua hii umeenda vizuri bila vurugu zozote.
Tunaomba Mungu hali iendelee hivihivi mpaka mwisho wa uchaguzi na kuundwa kwa serikali na Bunge.
Mungu Ibariki Tanzania...
 
Siro hamaanishi anachokisema. CCM wanashambulia msafara wa Lisu polisi wake wanaangalia tu.

Siro nikuonye, Lisu akidhurika utapata taabu sana.

tabu gan sasa, tayar ashavunjwa mguu saaahv anavaa kiatu na nyongeza ya soli, kwanza yeye ndo mstari wa mbele kuita mapolisi majinga, sasa avumilie polisi wakijibu
 
Nisome tena, itakuwa umekurupuka.

"Wanaoshabikia ccm ni mbumbumbu"...Twaweza.

wacha mambumbumbu tuwaonyesha sasa kwenye kura, jamaa wenu kapigwa mawe chato daaah mara ya tatu sasa anapigwa mawe na wananchi
 
Anahubiri amani huku nyuma ameficha upanga? Waache kuibeba CCM waone kama watu watafanya vurugu!
 
Ninamsikiliza IGP anaongea utumbo hapa. Ruge amemwambia Chadema wamekuwa wakifuatilia ratiba kwa DED bila mafanikio kwa hiyo wakaamua kufanya kampeni. Siro anasema watumie busara wasifanye kampeni bila ratiba balada yake wafuatilie ratiba
 
wacha mambumbumbu tuwaonyesha sasa kwenye kura, jamaa wenu kapigwa mawe chato daaah mara ya tatu sasa anapigwa mawe na wananchi
Watu wanapiga wenzao mawe wewe unaona ni mashujaa? Kwa hiyo wa Njombe wakiwaita waliomuua kada wa CCM mashujaa mtawaona wabaya?
 
Kazi ya polisi wake imekuwa ni kukamata wapinzani,kuwatesa na kuwaambukiza kesi za kijinga kinga tu,wala hana lolote la maana anapofanya.
Angalia hii hapa chini
Screenshot_20201013-113315.jpg
 
Ni aibu sana kwa Siro kuongea kama mjinga na anayefukiri watanzania ni wajinga!
Watu wenye akili wameishajua kabisa kuwa anatumika kama kitengo cha propaganda na kuumiza wapinzani!

Kuendelea kuongea ujinga wakati watu wameisha jua na wewe umeishajua kuwa wanajua huo ni ujinga... ni utaahira!
 
Watu wanapiga wenzao mawe wewe unaona ni mashujaa? Kwa hiyo wa Njombe wakiwaita waliomuua kada wa CCM mashujaa mtawaona wabaya?

as a human no, but on the other hand alistahili, kuna uwezekano violence ikatokea kubwa zaidi hata ya hii kwa sababu jamaaa anatukkana sana, hizi ndo kauli zake: HAYA MAPOLISI MAJINGA SANA, sasa akirushiwa bomu nan wa kulaumu?
 
wacha mambumbumbu tuwaonyesha sasa kwenye kura, jamaa wenu kapigwa mawe chato daaah mara ya tatu sasa anapigwa mawe na wananchi
Mawe yakupangwa na wahuni wa ccm hayaumizi. Lkn kukataliwa na wananchi kama ilivyokuwa kwa Magufuli kule Bunda, Busega na Kagera hakika imemkatisha sana tamaa Magufuli. Atakuwa na gundu la kunguni ama fungo huyu mzee.

Anashindwaje umaarufu na mgonjwa aliyekuwa hospitali, hajanunua hata msumari wa kujengea zahanati?

Kajenga Sana vitu lkn bado wananchi hawampendi.
 
Kila siku anaimba mapambio hayo hayo wakati kutimiza wajibu wao kama pilisi hawataki, msafara wa Lissu umeshambuliwa huko Chato halafu bado anaongea pumba tu bila aibu yoyote, Sirro amejisahau sana ameshakuwa mwanasiasa.

Lissu amefunga barabara huko hataki kusikia tena huu ujinga wako.

Sirro amepewa kibarua cha kuhakikisha ccm inashinda kwa vyovyote hata kwa mauaji. Inaonekana dhamira yake inakataa lakini madaraka matamu. Hivyo anajikuta akitoa vitisho ili wapinzani wakubali kuporwa kura zao. Anajua fika iwapo wapinzani watasimamia ushindi wa haki lazima aagize mauaji. Kikombe hiki anataka kimuepuke lakini kaamua kumtumikia shetani hivyo hana jinsi.
 
Ni kweli vijana wanashida mpaka utosini, Sirro na familia yake hawana shida sasa watuache, wakichakachua matokeo Polisi inabidi waajiriwe wengine maana hawatatosha kudhibiti umma
 
Back
Top Bottom