Sirudi mjini tena

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wananzengo, habari?

Disemba ndio hiyo tunaikaribia, ikiambatana na sikukuu mbali mbali za mwisho wa mwaka.

Mimi niliyetangulia huku kijijini, shamra shamra ni nyingi sana; nipo huku na mama watoto tukiangalia mimea ilivyochanua huku ikiangusha maua yake, kwa mbali milio mbali mbali ya ndege ikituburudisha.

Kweli maisha ya huku kijijini ni raha, ni kama tuko kwenye bustani ya edeni; kula mapapai bure, machungwa bure, parachichi bure, yaani kila tunda ni bure.

Achilia mbali, watu wa huku wana hofu ya Mungu; hawana lugha za utapeli utapeli kama wa huko mjini, hakuna kupigana mizinga wala kuhonga.

Haloo, mimi sirudi mjini, na mwezi wa disemba ukifika sitopatikana kwenye simu wananzengo, nitakuwa bize kwenye kucheza sindimba..

Karibuni kijijini.

 
Kuanzia tarehe 3 januari, watu huwa kama wamechanganikiwa; mambo yanakuwa mengi, mara ada, kulipa kodi ya pango, kufukuzwa kazi n.k Ila huku kijijini kuna unafuu mkubwa.​
Ndio nakuambia mjini utarudi tu na usiporudi utarudishwa
 
Nataka kuoa mke wa tatu..
Kuna wanawake wenye hali nzuri (wasiotumika sana)??
Maana huku mjini wengi wametumika hadi ladha ya papuchi hakuna tena..
 
Hakuna wasiojulikana
 
Nataka kuoa mke wa tatu..
Kuna wanawake wenye hali nzuri (wasiotumika sana)??
Maana huku mjini wengi wametumika hadi ladha ya papuchi hakuna tena..
Unaweza kubahatisha ukitembelea kijiji cha wagagagigikoko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…