Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wananzengo, habari?
Disemba ndio hiyo tunaikaribia, ikiambatana na sikukuu mbali mbali za mwisho wa mwaka.
Mimi niliyetangulia huku kijijini, shamra shamra ni nyingi sana; nipo huku na mama watoto tukiangalia mimea ilivyochanua huku ikiangusha maua yake, kwa mbali milio mbali mbali ya ndege ikituburudisha.
Kweli maisha ya huku kijijini ni raha, ni kama tuko kwenye bustani ya edeni; kula mapapai bure, machungwa bure, parachichi bure, yaani kila tunda ni bure.
Achilia mbali, watu wa huku wana hofu ya Mungu; hawana lugha za utapeli utapeli kama wa huko mjini, hakuna kupigana mizinga wala kuhonga.
Haloo, mimi sirudi mjini, na mwezi wa disemba ukifika sitopatikana kwenye simu wananzengo, nitakuwa bize kwenye kucheza sindimba..
Karibuni kijijini.