Sisi hatukulelewa kama wao

Sisi hatukulelewa kama wao

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Tulifunzwa kula kile kilichowekwa mezani na kukithamini, tukafunzwa kuridhika na vile vichache ambavyo vilipatikana majumbani mwetu. Tukakua tukivaa nguo ambazo wazazi wetu walimudu kuzinunua. Tukafunzwa kuridhika na maisha, tukaonywa kulilia vitu ambavyo havikuwa ndani ya uwezo wa wazazi wetu.

Licha ya kwamba hali ya maisha ilikuwa ya kawaida sana, lakini wazazi wetu hawakusahau kutufunza kutopokea zawadi na misaada ambayo tunapewa kwa masimango. Tena tukakanywa kukubali kufedheheka kisa tu shida ya siku moja.

Tukalelewa katika maadili sahihi zaidi, maadili ambayo yalitanguliza sana heshima na utu kuliko kiburi na dharau. Tukaonywa kutamani maisha ya watu ambao hatukujua historia za maisha yao. Wazazi wetu wakatusisitiza kuwa wapole na kujishusha mbele ya wanadamu wa dunia hii ambao kwao sifa ni kuonekana bora zaidi ya wengine.

Tukakomazwa kiakili kuelewa kuwa shida ni moja ya sehemu ya maisha, hivyo tusiziogope kabisa. Maana hakuna mteremko pasi na mpando. Wazazi wetu wakajitahidi sana kutoa chuki mioyoni mwetu, wakatuondolea mbali dhana potofu wakasema kwamba tusife mioyo pale tunapoona wenzetu wakifanikiwa, maana maisha yetu sisi binadamu ni kama maua yaani kila ua litachanua kwa wakati wake.

Basi tukaishi kwa kupendana, kila mtu akamthamini na kumjali mwenzie.

Hakika sisi hatukulelewa kama wao.

Ahsante kwa kusoma,
Wako katika kalamu,
Amani Dimile
 
Huu utandawazi umefanya maisha yawe ya kusikitisha sana...
 
Tulifunzwa kula kile kilichowekwa mezani na kukithamini, tukafunzwa kuridhika na vile vichache ambavyo vilipatikana majumbani mwetu. Tukakua tukivaa nguo ambazo wazazi wetu walimudu kuzinunua. Tukafunzwa kuridhika na maisha, tukaonywa kulilia vitu ambavyo havikuwa ndani ya uwezo wa wazazi wetu.
Licha ya kwamba hali ya maisha ilikuwa ya kawaida sana, lakini wazazi wetu hawakusahau kutufunza kutopokea zawadi na misaada ambayo tunapewa kwa masimango. Tena tukakanywa kukubali kufedheheka kisa tu shida ya siku moja. Tukalelewa katika maadili sahihi zaidi, maadili ambayo yalitanguliza sana heshima na utu kuliko kiburi na dharau. Tukaonywa kutamani maisha ya watu ambao hatukujua historia za maisha yao. Wazazi wetu wakatusisitiza kuwa wapole na kujishusha mbele ya wanadamu wa dunia hii ambao kwao sifa ni kuonekana bora zaidi ya wengine.
Tukakomazwa kiakili kuelewa kuwa Shida ni moja ya sehemu ya maisha, hivyo tusiziogope kabisa. Maana hakuna mteremko pasi na mpando. Wazazi wetu wakajitahidi sana kutoa chuki mioyoni mwetu, wakatuondolea mbali dhana potofu wakasema kwamba tusife mioyo pale tunapoona wenzetu wakifanikiwa maana maisha yetu sisi binadamu ni kama maua yaani kila ua litachanua kwa wakati wake. Basi tukaishi kwa kupendana, kila mtu akamthamini na kumjali mwenzie ..

HAKIKA SISI HATUKULELEWA KAMA WAO ..

Ahsante kwa kunisikiliza,

Wako katika kalamu Amani Dimile
Huo ndio ustaarabu wa Mwafrika.
 
Dunia ingekuwa mahala salama sana. [emoji1431]
 
Back
Top Bottom